BUSTANI YA WATU WEMA
وَعَنْ أَنَسٍ رَضِي اللَّهُ عَنْهُ قَالَ : مَرَّ النَّبِيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم بِامْرَأَةٍ تَبْكِي عِنْدَ قَبْرٍ فَقَال : «اتَّقِي الله وَاصْبِرِي » فَقَالَتْ : إِلَيْكَ عَنِّي ، فَإِنِّكَ لَمْ تُصَبْ بمُصِيبتى، وَلَمْ تعْرفْهُ ، فَقيلَ لَها : إِنَّه النَّبِيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، فَأَتتْ بَابَ النَّبِّي صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، فلَمْ تَجِد عِنْدَهُ بَوَّابينَ ،فَقالتْ : لَمْ أَعْرِفْكَ ، فقالَ : « إِنَّما الصَّبْرُ عِنْدَ الصَّدْمَةِ الأولَى » متفقٌ عليه
وفي رواية لمُسْلمٍ : « تَبْكِي عَلَى صَبيٍّ لَهَا
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: “Alipita Mtume ﷺ akamuona mwanamke akilia mbele ya kaburi. Akamwambia: [Mche Mwenyezi Mungu na usubiri.] Yule mwanamke akasema: “Niondokee, kwani hujapatwa na msiba kama wangu!” Wala hakumjua. Akaambiwa: Huyo alikuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ, akaenda hadi kwenye mlango wa Mtume ﷺ na hakuwakuta walinzi, akamwambia (Mtume ﷺ): “Nilikuwa sijakujua kama ni wewe.” Mtume ﷺ akamwambia: [Hakika subira ni mwanzo wa kupatwa na msiba.] [Imepokewa na Bukhariy na Muslim]
Na katika Riwaya nyingine ya Muslim imesema: [Alikuwa akimlilia mwanawe.]