0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

030. Riyadhu Swalihina Mlango wa Subira Hadithi ya 06


BUSTANI YA WATU WEMA


وَعَنْ صُهَيْبٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قَالَ : « كَانَ مَلِكٌ فيِمَنْ كَانَ قبْلَكُمْ، وَكَانَ لَهُ سَاحِرٌ ، فَلَمَّا كَبِرَ قَالَ لِلْمَلِك : إِنِّي قَدْ كَبِرْتُ فَابعَثْ إِلَيَّ غُلاَماً أُعَلِّمْهُ السِّحْرَ ، فَبَعَثَ إِلَيْهِ غُلاَماً يعَلِّمُهُ ، وَكَانَ في طَريقِهِ إِذَا سَلَكَ رَاهِبٌ، فَقَعَدَ إِلَيْهِ وَسَمِعَ كَلاَمهُ فأَعْجَبهُ ، وَكَانَ إِذَا أَتَى السَّاحِرَ مَرَّ بالرَّاهِب وَقَعَدَ إِلَيْه ، فَإِذَا أَتَى السَّاحِرَ ضَرَبَهُ ، فَشَكَا ذَلِكَ إِلَى الرَّاهِبِ فقال : إِذَا خَشِيتَ السَّاحِر فَقُلْ : حبَسَنِي أَهْلي ، وَإِذَا خَشِيتَ أَهْلَكَ فَقُلْ: حَبَسَنِي السَّاحرُ .
فَبيْنَمَا هُو عَلَى ذَلِكَ إذْ أتَى عَلَى دابَّةٍ عظِيمَة قدْ حَبَسَت النَّاس فقال : اليوْمَ أعْلَمُ السَّاحِرُ أفْضَل أم الرَّاهبُ أفْضلَ ؟ فأخَذَ حجَراً فقالَ : اللهُمَّ إنْ كان أمْرُ الرَّاهب أحَبَّ إلَيْكَ مِنْ أَمْرِ السَّاحِرِ فاقتُلْ هَذِهِ الدَّابَّة حتَّى يمْضِيَ النَّاسُ ، فرَماها فقتَلَها ومَضى النَّاسُ، فأتَى الرَّاهب فأخبَرهُ . فقال لهُ الرَّاهبُ : أىْ بُنيَّ أَنْتَ اليوْمَ أفْضلُ منِّي ، قدْ بلَغَ مِنْ أمْركَ مَا أَرَى ، وإِنَّكَ ستُبْتَلَى ، فإنِ ابْتُليتَ فَلاَ تدُلَّ عليَّ ، وكانَ الغُلامُ يبْرئُ الأكْمةَ والأبرصَ ، ويدَاوي النَّاس مِنْ سائِرِ الأدوَاءِ . فَسَمعَ جلِيسٌ للملِكِ كانَ قدْ عمِىَ، فأتَاهُ بهداياَ كثيرَةٍ فقال : ما ههُنَا لك أجْمَعُ إنْ أنْتَ شفَيْتني ، فقال إنِّي لا أشفِي أحَداً، إِنَّمَا يشْفِي الله تعَالى، فإنْ آمنْتَ بِاللَّهِ تعَالَى دعوْتُ الله فشَفاكَ ، فآمَنَ باللَّه تعَالى فشفَاهُ اللَّهُ تَعَالَى ، فأتَى المَلِكَ فجَلَس إليْهِ كما كانَ يجْلِسُ فقالَ لَهُ المَلكُ : منْ ردَّ علَيْك بصَرك؟ قال : ربِّي . قَالَ: ولكَ ربٌّ غيْرِي ؟، قَالَ : رَبِّي وربُّكَ الله ، فأَخَذَهُ فلَمْ يزلْ يُعذِّبُهُ حتَّى دلَّ عَلَى الغُلاَمِ فجئَ بِالغُلاَمِ ، فقال لهُ المَلكُ : أىْ بُنَيَّ قدْ بَلَغَ منْ سِحْرِك مَا تبْرئُ الأكمَهَ والأبرَصَ وتَفْعلُ وَتفْعَلُ فقالَ : إِنَّي لا أشْفي أَحَداً ، إنَّما يشْفي الله تَعَالَى، فأخَذَهُ فَلَمْ يزَلْ يعذِّبُهُ حتَّى دلَّ عَلَى الرَّاهبِ ، فجِئ بالرَّاهِبِ فقيل لَهُ : ارجَعْ عنْ دِينكَ، فأبَى ، فدَعا بالمنْشَار فوُضِع المنْشَارُ في مفْرقِ رأْسِهِ، فشقَّهُ حتَّى وقَعَ شقَّاهُ ، ثُمَّ جِئ بجَلِيسِ المَلكِ فقِلَ لَهُ : ارجِعْ عنْ دينِكَ فأبَى ، فوُضِعَ المنْشَارُ في مفْرِقِ رَأسِهِ ، فشقَّهُ به حتَّى وقَع شقَّاهُ ، ثُمَّ جئ بالغُلامِ فقِيل لَهُ : ارجِعْ عنْ دينِكَ ، فأبَى ، فدَفعَهُ إِلَى نَفَرٍ منْ أصْحابِهِ فقال : اذهبُوا بِهِ إِلَى جبَلِ كَذَا وكذَا فاصعدُوا بِهِ الجبلَ ، فـإذَا بلغتُمْ ذروتهُ فإنْ رجعَ عنْ دينِهِ وإِلاَّ فاطرَحوهُ فذهبُوا به فصعدُوا بهِ الجَبَل فقال : اللَّهُمَّ اكفنِيهمْ بمَا شئْت ، فرجَف بِهمُ الجَبَلُ فسَقطُوا ، وجَاءَ يمْشي إِلَى المَلِكِ ، فقالَ لَهُ المَلكُ : ما فَعَلَ أَصحَابكَ ؟ فقالَ : كفانيهِمُ الله تعالَى ، فدفعَهُ إِلَى نَفَرَ منْ أصْحَابِهِ فقال : اذهبُوا بِهِ فاحملُوه في قُرقُور وَتَوسَّطُوا بِهِ البحْرَ ، فإنْ رَجَعَ عنْ دينِهِ وإلاَّ فَاقْذفُوهُ ، فذَهبُوا بِهِ فقال : اللَّهُمَّ اكفنِيهمْ بمَا شِئْت ، فانكَفَأَتْ بِهِمُ السَّفينةُ فغرِقوا ، وجَاءَ يمْشِي إِلَى المَلِك . فقالَ لَهُ الملِكُ : ما فَعَلَ أَصحَابكَ ؟ فقال : كفانِيهمُ الله تعالَى . فقالَ للمَلِكِ إنَّك لسْتَ بقَاتِلِي حتَّى تفْعلَ ما آمُركَ بِهِ . قال : ما هُوَ ؟ قال : تجْمَعُ النَّاس في صَعيدٍ واحدٍ ، وتصلُبُني عَلَى جذْعٍ ، ثُمَّ خُذ سهْماً مِنْ كنَانتِي ، ثُمَّ ضعِ السَّهْمِ في كَبدِ القَوْسِ ثُمَّ قُل : بسْمِ اللَّهِ ربِّ الغُلاَمِ ثُمَّ ارمِنِي ، فإنَّكَ إذَا فَعَلْتَ ذَلِكَ قَتَلْتنِي . فجَمَع النَّاس في صَعيدٍ واحِدٍ ، وصلَبَهُ عَلَى جذْعٍ ، ثُمَّ أَخَذَ سهْماً منْ كنَانَتِهِ ، ثُمَّ وضَعَ السَّهمَ في كبِدِ القَوْسِ، ثُمَّ قَالَ : بِسْم اللَّهِ رَبِّ الغُلامِ ، ثُمَّ رمَاهُ فَوقَعَ السَّهمُ في صُدْغِهِ ، فَوضَعَ يدَهُ في صُدْغِهِ فمَاتَ . فقَالَ النَّاسُ : آمَنَّا بِرَبِّ الغُلاَمِ ، فَأُتِىَ المَلكُ فَقِيلُ لَهُ : أَرَأَيْت ما كُنْت تحْذَر قَدْ وَاللَّه نَزَلَ بِك حَذرُكَ . قدْ آمنَ النَّاسُ . فأَمَرَ بِالأخدُودِ بأفْوَاهِ السِّكك فخُدَّتَ وَأضْرِمَ فِيها النيرانُ وقالَ : مَنْ لَمْ يرْجَعْ عنْ دينِهِ فأقْحمُوهُ فِيهَا أوْ قيلَ لَهُ : اقْتَحمْ ، ففعَلُوا حتَّى جَاءتِ امرَأَةٌ ومعَهَا صَبِيٌّ لهَا ، فَتقَاعَسَت أنْ تَقعَ فِيهَا ، فقال لَهَا الغُلاَمُ : يا أمَّاهْ اصبِرِي فَإِنَّكَ عَلَي الحَقِّ »     روَاهُ مُسْلَمٌ .


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



   2 تتمة الحديث



 3 تتمة الحديث



 4 تتمة الحديث



 5 تتمة الحديث



 6 تتمة الحديث



 7 تتمة الحديث



 8 تتمة الحديث



 9 تتمة الحديث



Kutoka kwa Swuhayb Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume ﷺ : [Alikuwepo mfalme kabla ya zama zenu. Alikuwa anae mchawi, yule mchawi alipozeeka alimwambia mfalme: “Mimi nimezeeka, niletee kijana nitakaemfunza uchawi.” (mfalme) akampelekea kijana ili amfunze. Alikuwa (yule kijana) katika njia anayoelekea kuna Rahibu (mtawa mwanaume). Akakaa kumsikiliza, akapendezewa na maneno yake, na alikuwa akitaka kumuendea mchawi yule hupita kwa Rahibu yule na kukaa naye na kumsikiliza, anapomwendea mchawi, humpiga. Jambo hili akamshitakia yule mtawa. (Mtawa) akamwambia: “Utakapomuendea mchawi mwambie: ‘Nimezuiliwa na watu wangu,’ na unapowarudia watu wako, waambie: Nimezuiliwa na mchawi.” Alipokuwa akiendelea katika hali hiyo, kwa ghafla akaona mnyama mkubwa aliyezuia watu. Akasema: “Leo ndiyo nitajua kati ya mtawa na mchawi nani aliye bora.” Akachukua jiwe na akasema: “Ewe Mola, ikiwa jambo la yule Mtawa linapendeza Kwako kuliko jambo la yule mchawi, basi muuwe mnyama huyu ili watu waweze kupita.” Akamrushia (jiwe) na akamuua, watu wakapita. Akamuendea Mtawa na kumueleza habari ile. Yule Mtawa akamwambia: “Ee mwanangu leo hii wewe ni bora kulikoni mimi, jambo lako limefikia jinsi ninavyoliona, kwa yakini utapata mtihani; basi utakapopata mtihani, usimjulishe yoyote yule kwangu.” Yule kijana akaanza kuwaponya waliozaliwa vipofu, wenye ukoma na akiwatibu watu kila aina ya maradhi. Rafiki wa mfalme aliyekuwa amepofoka, akasikia habari hii. Akampelekea zawadi nyingi, akamwambia: “Mimi sina uwezo wa kumponya yoyote, hakika Anaeponya ni Allaah . Ukimuamini Allaah nitamuomba Naye Atakuponya.” Akamuamini Mwenyezi Mungu, Na Mwenyezi Mungu Akamponya. Akaenda kwa mfalme na kukaa nae kama anavyokaa nae (kila siku). Mfalme akamuuliza: “Ni nani aliyekuponya macho yako?” Akajibu: “Ni Mola wangu.” Akamuuliza: “Unae Mola asiyekuwa mimi?” Akamjibu: “Mola wangu na Mola wako ni Mwenyezi Mungu.” Akamchukua na akamuadhibu mpaka akamtaja yule kijana. Yule kijana akaletwa mbele ya mfalme, akamuuliza: “Ee kijana wangu, uchawi wako umefikia kiwango cha kuwaponya vipofu na wenye ukoma, na unafanya kadhaa na kadhaa?” Akamwambia: “Mimi sina uwezo wa kumponya yoyote yule, kwa yakini Anaeponya ni Allaah . ” Akamchukua na kumuadhibu mpaka akamtaja yule Mtawa. Mtawa akaletwa, akaambiwa: “Acha dini yako.” Akakataa. Akaitisha msumeno akauweka utosini mwake, akampasua vipande viwili vikaanguka (akamgawanya pande mbili). Halafu akaletwa jalisi wa mfalme. Akaambiwa: “Acha dini yako.” Akakataa. Msumeno ukawekwa utosini mwake, akapasuliwa pande mbili zikaanguaka. Kisha akaletwa yule kijana. Akaambiwa: “Wacha dini yako.” Akakataa. Akamkabidhi kwa askari wake, akawaambia: “Nendeni naye katika jabali kadhaa wa kadhaa, mtakapofika katika kilele chake na akawa ameiwacha dini yake, basi muacheni, ikiwa hakuacha basi mtupeni chini.” Wakaenda nae na wakapanda nae juu ya jabali. Yule kijana akaomba: “Ewe Mola! Nitosheleze na shari yao namna Upendavyo.” Lile jabali likatikisika wakaanguka. Akarudi kwa mfalme huku akitembea. Mfalme akamuuliza: “Wamekuaje watu wako?” Akamwambia: Allaah Amenitosheleza.” Akamkabidhisha kwa kundi (lingine) la maaskari wake. Akawaambia: “Mpelekeni na mumpandishe jahazi ndogo hadi katikati ya bahari, akiwacha dini yake muacheni, akikataa basi mtoseni.” Wakaenda naye, akaomba: “Ewe Mola! Nitosheleze na shari yao namna Upendavyo.” Jahazi likapinduka wakazama. Akarudi kwa mfalme akitembea. Mfalme akamuuliza: “Wamekuaje watu wako?” Akamwambia: “Allaah Amenitosheleza.” Akamwambia mfalme: “Hakika huwezi kuniua mpaka ufanye nitakalokuamuru.” Akamuuliza: “Ni jambo gani hilo utakaloniamuru?” Akamwambia: “Wakusanye watu katika uwanja ulio wazi, halafu unisulubishe juu ya gogo, halafu uchukue mshale utakaokuwa katika ziaka yangu, kisha utauweka mshale katika upinde, halafu useme: “Kwa jina la Allaah, Rabb wa kijana huyu”. Kisha unirushie. Hakika ukifanya hivyo, utafanikiwa kuniua.” Yule mfalme akawakusanya watu katika uwanja mmoja, akamtundika juu ya gogo, halafu akachukua mshale kutoka katika ziaka yake, kisha akauweka mshale katikati ya upinde, halafu akasema: “Kwa jina la Allaah, Rabb wa kijana huyu,” kisha akamrushia ule mshale ukaingia katika panda lake uso, akauweka mkono wake katika panda lake na akafa. Watu wakasema: “Tumemuamini Rabb wa kijana huyu.” Mfalme akaendewa na kuambiwa: “Je, umeliona ulilokuwa ukilitahadhari? Wa-Allaahi limekuwa ulilolikataa, watu wamekuwa na iymaan.” Akaamuru kuchimbwe mahandaki barabarani, mioto ikawashwa humo. Akasema: “Ambae hatoacha dini yake mtupeni humo.” Au huambiwa: “Jitoseni wenyewe.” Wakafanya hivyo. Akaletwa mwanamke aliye na mtoto wake. Akasimama na akafanya uoga kuingia humo, yule mtoto wake akamwambia: “Ee mama yangu, subiri hakika wewe upo katika haki!]      [Imepokewa na Muslim]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.