0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

020. Riyadhu Swalihina Mlango wa Tawba Hadithi ya 08


BUSTANI YA WATU WEMA


وعنْ أبي سعِيدٍ سَعْد بْنِ مالك بْنِ سِنانٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه أَن نَبِيَّ الله صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قَال : « كان فِيمنْ كَانَ قَبْلكُمْ رَجُلٌ قتل تِسْعةً وتِسْعين نفْساً ، فسأَل عن أَعلَم أَهْلِ الأَرْضِ فدُلَّ على راهِبٍ ، فَأَتَاهُ فقال : إِنَّهُ قَتَل تِسعةً وتسعِينَ نَفْساً ، فَهلْ لَهُ مِنْ توْبَةٍ ؟ فقال : لا فقتلَهُ فكمَّلَ بِهِ مِائةً ثمَّ سألَ عن أعلم أهلِ الأرضِ ، فدُلَّ على رجلٍ عالمٍ فقال: إنهَ قَتل مائةَ نفسٍ فهلْ لَهُ مِنْ تَوْبةٍ ؟ فقالَ: نَعَمْ ومنْ يحُولُ بيْنَهُ وبيْنَ التوْبة ؟ انْطَلِقْ إِلَى أَرْضِ كذا وكذا ، فإِنَّ بها أُنَاساً يعْبُدُونَ الله تعالى فاعْبُدِ الله مَعْهُمْ ، ولا تَرْجعْ إِلى أَرْضِكَ فإِنَّهَا أَرْضُ سُوءٍ ، فانطَلَق حتَّى إِذا نَصَف الطَّريقُ أَتَاهُ الْموْتُ فاختَصمتْ فيهِ مَلائكَةُ الرَّحْمَةِ وملاكةُ الْعَذابِ . فقالتْ ملائكةُ الرَّحْمَةَ : جاءَ تائِباً مُقْبلا بِقلْبِهِ إِلى اللَّهِ تعالى ، وقالَتْ ملائكَةُ الْعذابِ : إِنَّهُ لمْ يَعْمَلْ خيْراً قطُّ ، فأَتَاهُمْ مَلكٌ في صُورَةِ آدمي فجعلوهُ بيْنهُمْ أَي حكماً فقال قيسوا ما بَيْن الأَرْضَين فإِلَى أَيَّتهما كَان أَدْنى فهْو لَهُ، فقاسُوا فوَجَدُوه أَدْنى إِلَى الأَرْضِ التي أَرَادَ فَقبَضْتهُ مَلائكَةُ الرَّحمةِ »     متفقٌ عليه.
وفي روايةٍ في الصحيح : « فكَان إِلَى الْقرْيَةِ الصَّالحَةِ أَقْربَ بِشِبْرٍ ، فجُعِل مِنْ أَهْلِها »   وفي رِواية في الصحيح : « فأَوْحَى اللَّهُ تعالَى إِلَى هَذِهِ أَن تَبَاعَدِى، وإِلى هَذِهِ أَن تَقرَّبِي وقَال : قِيسُوا مَا بيْنهمَا ، فَوَجدُوه إِلَى هَذِهِ أَقَرَبَ بِشِبْرٍ فَغُفَرَ لَهُ » . وفي روايةٍ : « فنأَى بِصَدْرِهِ نَحْوهَا » 


Kutoka kwa Abuu Sa’iyd bin Maalik bin Sinaan Al-Khudriyy Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume amehadithia :[Kulikuwepo mtu kabla yenu aliua watu tisini na tisa akaulizia aliye mjuzi zaidi katika watu katika nchi ile. Akajulishwa mtawa (miongoni mwa Bani Israaiyl). Akamwendea, akamuuliza: “Nimeua watu tisini na tisa, je, nina Tawba?” Akamjibu: “Hapana!” Akamuua, akawa mtu wa mia. Kisha akauuliza mjuzi zaidi katika watu katika nchi ile. Akafahamishwa kuhusu Mwanachuoni. (akamwendea) Akamuuliza: “Nimeua watu mia. Je, nina Tawba?” Akamjibu: “Ndio, ni nani atakayezuia baina yako na Tawba? Nenda katika nchi fulani, huko kuna watu wanaomuabudu Mwenyezi Mungu ﷻ basi nenda ukamuabudu Mwenyezi Mungu pamoja nao wala usirejee katika nchi yako, kwani hiyo ni nchi ya maovu.” Akaenda, hata alipofika nusu ya njia, alifikwa na mauti. Malaika wa rahmah wakaanza kuvutana na Malaika wa adhabu. Malaika wa rahmah wakasema: “Alikuja hali ya kutubia na ameelekea moyo wake kwa Mwenyezi Mungu ﷻ Malaika wa adhabu wakasema: “Yeye hakutenda khayr katu!” Akaja Malaika (mwengine) katika sura ya mwanadamu, wakamfanya ndiye hakimu baina yao. Akawaambia: “Pimeni baina ya nchi mbili, katika nchi yoyote iliyopo karibu naye, atakuwa ni wa huko.” Wakapima, wakamkuta kuwa yupo karibu zaidi na nchi anayokusudia kwenda. Malaika wa rahmah wakamchukua.]    [Imepokelewa na Bukhariy na Muslim]

Na katika Riwaya nyingine ya Swahihi Al-Bukhariy, imesema: [Akawa katika kijiji cha watu wema yu karibu nacho kwa shubiri moja. Akajaaliwa ni wa huko.]

Na Riwaya nyingine ya Swahihi Al-Bukhariy, imesema: [Mwenyezi Mungu Akakiambia kijiji alichotoka: “Kuwa mbali!” na kijiji anachoenda: “Kuwa karibu!” Na Akawaambia pimeni baina yake.” Wakampata kuwa yupo karibu zaidi ya kijiji anachokwenda kwa shubiri moja; akasamehewa.]

Na Riwaya nyingine inasema: [Akakaribia kwa kifua chake upande ule.]


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.