0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

029. Riyadhu Swalihina Mlango wa Subira Hadithi ya 05


BUSTANI YA WATU WEMA


وعنْ أبي زيْد أُسامَة بن زيد حَارثَةَ موْلَى رسُول الله صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم وحبَّهِ وابْنِ حبِّهِ رضـِيَ الله عنهُمَا ، قالَ : أَرْسلَتْ بنْتُ النَّبِيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : إنَّ ابْنِي قَدِ احتُضِرَ فاشْهدْنَا ، فأَرسَلَ يقْرِئُ السَّلامَ ويَقُول : « إن للَّه مَا أَخَذَ ، ولهُ مَا أعْطَى ، وكُلُّ شَيْءٍ عِنْدَهُ بأجَلٍ مُسمَّى ، فلتصْبِر ولتحْتسبْ » فأرسَلَتْ إِليْهِ تُقْسمُ عَلَيْهِ ليأْتينَّها. فَقَامَ وَمَعَهُ سَعْدُ بْنُ عُبادَةَ، وَمُعَاذُ ابْنُ جَبَلٍ ، وَأُبَيُّ بْنَ كَعْبٍ ، وَزَيْدُ بْنِ ثاَبِتٍ ، وَرِجَالٌ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ ، فَرُفِعَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم الصبيُّ ، فأقعَدَهُ في حِجْرِهِ ونَفْسُهُ تَقعْقعُ ، فَفَاضتْ عَيْناهُ ، فقالَ سعْدٌ : يَا رسُولَ الله مَا هَذَا ؟ فقالَ: « هَذِهِ رَحْمةٌ جعلَهَا اللَّهُ تعَلَى في قُلُوبِ عِبَادِهِ » وفي روِايةٍ : « في قُلُوبِ منْ شَاءَ مِنْ عِبَادِهِ وَإِنَّمَا يَرْحَمُ اللَّهُ منْ عِبَادِهِ الرُّحَمَاءَ »     مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَمَعْنَى « تَقَعْقَعُ » : تَتحَرَّكُ وتَضْطَربُ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى





Kutoka kwaAbuu Zayd, Usaamah bin Zayd bin Haarithah muachwa huru wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ, kipenzi chake na ni mwana wa kipenzi chake Radhi za Allah ziwe juu yao amesema: Binti mmoja wa Mtume alimpelekea salaamu (Mtume wa Mungu )  kuwa “Mwanangu amejiwa na umauti, basi njoo.” Naye akamtuma mtu akimpelekea salaamu na akamwambia: [Ni cha Mwenyezi Mungu anachokichukuwa na nichake anachotowa, na Kila kitu Kwake kina muda maalumu, basi asubiri na taraji malipo kwa Mwenyezi Mungu]. Akamtumia tena ujumbe akimuapia aende. Akasimama, pamoja naye alikuwepo Sa’ad bin Ubaadah, na Mu’aadh bin Jabal, na Ubayyi bin Ka’ab, na Zayd bin Thaabit na wengineo Radhi za Allah ziwe juu yao. Yule mtoto akapelekewa Mtume wa Mwenyezi Mungu , akamkalisha katika paja lake na nafsi ya yule mtoto ikiwa katika hali ya woga, macho ya Mtume yakabubujikwa na machozi, Sa’ad akauliza: “Una nini ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ?” Akamwambia: [Hii ni rahmah, ya Mwenyezi Mungu Amejaalia katika nyoyo za waja Wake.]

na katika Riwaya nyingine imesema: [Katika nyoyo za Anaowataka miongoni mwa waja Wake. Hakika Allaah Huwarehemu wenye huruma katika waja Wake.]

[Imepokewa na Bukhari na Muslim]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.