وعن أبي عبد الله جابر بن عبد الله الأنصاري – رضي الله عنهما – قال: كنا مع النبي صلي الله عليه وسلم في غزاة فقال: [إن بالمدينة لرجالاً ما سرتم مسيراً ولا قطعتم وادياً إلا كانوا معكم؛ حبسهم المرض] وفي رواية: [إلا شركوكم في الأجر] رواه مسلم
ورواهُ البُخَارِيُّ عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ :رَجَعْنَا مِنْ غَزْوَةِ تَبُوكَ مَعَ النَّبِيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فَقَالَ: “إِنَّ أَقْوَامَاً خلْفَنَا بالمدِينةِ مَا سَلَكْنَا دشِعْباً وَلاَ وَادِياً إِلاَّ وَهُمْ مَعَنَا ، حَبَسَهُمْ الْعُذْرُ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
BUSTANI YA WATU WEMA
Kutoka kwa Jabir bin Abdillah Al Answary radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume ﷺ katika vita fulani akasema: [Hakika Madina kuna watu ambao nyinyi hamukwenda mwendo wowote, wala hamukupita jangwa lolote isipokuwa wao wako na nyinyi, wamezuiliwa na ugonjwa” na katika Riwaya ngine Amesema [Isipokuwa wameshirikiana nanyi katika Ujira] [Imepokelewa na Muslim]
Na amepokea Imamu Al Bukhari Kutoka kwa Anas radhi za Allah ziwe juu yake asema:
Tulirudi kutoka katika vita vya Tabuuk pamoja na Mtume ﷺ akasema: [Hakika kuna watu nyuma yetu Madina hatukufuata njia ya mawe wala jangwa ila wao wako pamoja nasisi ,wamezuiliwa na udhuru].
SIKILIZA SHEREHE YA HADITHI HII NA DR.ISLAM