0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

ZAKA ZA FITRI MAANA YAKE NA HUKMU YAKE

SOMO LA FIQHI

MAANA YA ZAKA ZA FITRI
Zaka ya fitri
Zaka aliyoifaradhisha Mtume ﷺ wakati wa kufungua katika kumalizika kwa mwezi wa Ramadhan.

Na imeitwa Zaka ya fitri kwasababu inawajibika pale mtu anapofungua kwa kumalizika mwezi wa Ramadhani.

HUKMU YA ZAKA YA FITRI 

Zaka ya Fitri ni lazima kwa kila Muislamu anayemiliki siku ya Idi na usiku wake pishi ya chakula cha ziada ya chakula chake cha siku na cha familia yake (nayo ni karibia kilo mbili na nusu).

Na yamlazimu mwenye kutoa Zaka ajitole Zaka nafsi yake, na mke wake, na wale ambao ni jukumu lake kuwalisha, hata mtoto alioko kwenye tumbo la mamake. Na dalili ya kuwajibika kwake ni ilivyopokewa kutoka kwa  Ibn Umar radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie asema:

فرض رسول الله صلى الله عليه وسلم زكاة الفطر من رمضان صاعاً من تمر، أو صاعاً من شعير على العبد والحر، والذكر والأنثى، والصغير والكبير من المسلمين

[Amefaradhisha Mtume ﷺ Zaka ya Fitri Mwezi wa Ramadhani Pishi moja ya tende, au Pishi moja ya Shayir (aina ya nafaka) kwa mtumwa na muungwana, na mume na mke, na mdogo na mkubwa katika waislamu.]  [Imepokewa na bukhari na muslim.]

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.