0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

VIJANA SITA KUTOKA YATHRIB


AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Katika msimu wa Hijja katika mwaka wa Kumi na Moja wa Utume sawasawa na mwezi Julai mwaka 620 C.E. ulingano wa Kiislamu ulipata mbegu njema na kwa kasi ya ajabu. Mbegu hizo zikageuka na kuwa miti mirefu, Waislamu walijikinga katika vivuli vyake vilivyokuwa vipana dhidi ya joto la dhulma na uovu uliokuwa umedumu kwa miaka mingi.

Kwa kuzingatia shida na vikwazo alivyokuwa akivipata Mtume (ﷺ) katika kufikisha ujumbe wake kutoka kwa watu wa Makka, kwa hekima yake alibadili mkakati na akawa akiwaendea watu wa makabila katika nyakati za usiku ili mtu yeyote, miongoni mwa watu wa Makka waliokuwa Washirikina, asiweze kumzuia kufikisha ujumbe wake. Siku moja usiku akiwa na Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) na Ali (Radhi za Allah ziwe juu yake) alipita katika majumba ya Dhuhal na Shayban bin Tha’alaba, akawalingania juu ya Uislamu na ulipita mjadala kati ya Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) na mtu mmoja kutoka katika kabila la Dhuhal, na watu wa kabila la Banu Shayban walijibu kwa majibu ambayo yalitia matumaini kuwa huenda wakasilimu, lakini walisita kusilimu. (1)

Kisha Mtume wa Allah (s.w.t.) alipita katika Aqabah huko Mina akasikia sauti za watu wakizungumza, aliwaendea na kukutana nao, walikuwa ni vijana sita wafuatao, kutoka kabila la Khazraji:-

1. Asad bin Zurarah (kutoka kabila la Banu-Najjar)

2. Aufi bin Harith bin Rifaa Ibn Afraa (kutoka kabila la Banu-Najjar)

3. Rafii bin Malik bin Al-Ajlani (kutoka kabila la Banu Zuraiq)

4. Qutbah bini ’Amir bin Hadida (kutoka katika kabila la Banu Salamah)

5. ’Uqbah bin ’Aamir bin Nabi (kutoka katika kabila la Banu Hiram bin Ka’ab)

6. Jabir bin Abdillah bin Riab (kutoka katika kabila la Banu ‘Ubayd bin Ghunam)

Sababu moja ya mafanikio ya watu wa Yathrib ni kuwa walikuwa wakisikia kutoka kwa marafiki zao Wayahudi wa Madina kuwa yupo Mtume katika Mitume atakaetumwa katika zama hizi, atakapofika tutamfuata na tutawaueni tukiwa pamoja naye kama walivyokuwa watu wa ‘Aad na Iram.(2)

Alipokutana nao Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) aliwauliza, “Ni akina nani nyinyi?.” Wakajibu; ”Watu kutoka katika kabila la Banu Khazraji”; Akawauliza; ”Ni katika marafiki wa Mayahudi?” Wakajibu; ‘Ndiyo’; Akawauliza; ‘Hivi huwa hawakai na kuzungumza na nyinyi?.’ Wakauliza; ’Kwa nini?’; Wakakaa pamoja naye na akawawekea wazi ukweli kuhusu Uislamu na wito wake na akawalingania kwa Mwenyezi Mungu Mwenye Kushinda Mwenye Utukufu na akawasomea Qur’an. Baada ya wao kuisikia Qur’an wakasemezana, kwa hakika huyu ni Mtume ambaye wamekuwa wakimtaja Mayahudi, basi wasitutangulie, tufanye haraka kujibu wito wake na tuingie katika Uislamu. Watu wenye akili miongoni mwa watu wa Yathrib waliokuwa wamechoshwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilikuwa vimepita karibuni na ambavyo bado athari zake zikionekana, wakapata matuunaini kuwa huenda wito wake ukawa ndio sababu ya kuvimaliza vita hivyo. Walisema kumwambia Mtume (ﷺ), “Kwa hakika sisi tumewaacha jamaa zetu na hakuna watu walio na uadui kati yao kama jamaa zetu. Tunatarajia Allah (s.w.t) Awaunganishe kupitia kwako. Tutakaporudi nyumbani tutakwenda na kuwafahamisha hili jambo lako, Dini hii, na iwapo Mwenyezi Mungu (s.w.t) Atawakusanya kwako basi hakuna aliyemtukufu kuliko wewe.” Walirejea Madina na ujumbe wa Uislamu na kuutangaza katika kila nyumba ya mji huo, mpaka haikubakia nyumba yoyote katika nymnba za Al-Answar isipokuwa ndani yake kulikuwa na utajo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ). (3)


1) Mukhtnsar Siratu Rmsul, Uk. 150-152.
2) Zaad Ma’ad, Juzuu 2, uk. 50. Ibn Hisham, juzuu 1, Uk. 429, 541
3) Talqiyh Ahlul Athar, Uk. 10. Sahihil Bukhari, Iuzuu 1, Uk. 551. 247
*) Arrahiq Al-Makhtuum Uk 5-247

Begin typing your search above and press return to search.