0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

UMUHIMU WA SWALA

UMUHIMU WA SWALA

Dini ya kiislamu ambayo Mwenyezi Mungu ameitukuza na kuridhia nayo, na ameweka malipo makubwa kwa vile vinavyotamani nafsi na uislamu umejengwa na misingi na hatosalimika anaekeuka misingi hiyo na adhabu iumizayo, na atakae fuata misingi hayo atapata utukufu na heshima hapa duniani na kesho akhera, na miongoni mwa misingi hayo ni swala, swala ambao ni msingi wa dini na nguzo ya pili baada ya kutamka shahada mbili, na swala ina fadhila kubwa ambapo Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ Amesema:

[الصلاة خير موضوع فمن استطاع أن يستكثر فليستكثر]     رواه الطبراني

[Swala ni amali bora, na atakae weza kuzidisha basi na azidishe]     [Imepokewa na Al-Twabaraniy]
Swala ni nguzo ya pili katika uislamu. Imepokewa na Anas akisema Mtume ﷺ:

[حبب إلي من الدنيا النساء والطيب، وجعلت قرة عيني في الصلاة]   رواه الترمذي

[Nimependezwa na Dunia na wanawake mafuta mazuri, na nikajaaliwa kuwa swala ndio kitulizo cha macho yangu]    [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy]
Na ni ibada ya kwanza aliyofaradhisha Mwenyezi Mungu, na ndio amali ya kwanza atakayohisabiwa mwanadamu, na ndio wasia wa mwisho ambao Mtume ﷺ ameusia umma wake akisema:

[الصلاة وما ملكت أيمانكم]    رواه إبن ماجة

[Swala, swala na watumwa wenu]    [Imepokewa na Ibnu Maajah]
Na ndio mwanzo itakayopotea na ikipotea imepotea dini.

UMUHIMU WA SWALA

Na kuonyesha umuhimu wa swala ni kkufaradhishwa katika mbingu ya saba, na ndio inaowekwa mafungamano kati ya mja na mola wake, na inakataza maovu. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

 {إِنَّ الصَّلاةَ تَنْهَى عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنْكَرِ وَلَذِكْرُ اللَّهِ أَكْبَرُ وَاللَّهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ}   العنكبوت/45

[Hakika Swala humzuilia huyo mwenye kusali na mambo machafu na maovu]   [Al-Ankabuut:45]
Wengi miongoni mwa watu wanaswali swala ya ghurabu (kudonoa), hawana utulivu, wala hawamtaji Mwenyezi Mungu ila kwa uchache, kugeuka katika swala kujikuna, mfanya biashara kufikiria mali yake anaposwali.
Hadithi iliopokewa kutoka kwa Mtume ﷺ akimuambia mtu ambae hakua na utulivu katika swala

[ارْجِعْ فَصَلِّ , فَإِنَّك لَمْ تُصَلِّ]

[Rejea ukaswali kwani hujaswali]

MAMBO YANAOSAIDIA KUWA NA UTULIVU KATIKA SWALA

Mambo ambayo husababisha kuhudhurisha moyo ni kujua unacho kizungumza au unachokifanya, mfano:
Unapotoa Takbir na kuinua mikono miwili hii inamaanisha kumtukuza Mwenyezi Mungu.
Na ukiweka mkono wa kulia juu ya kushoto ni kujidhalilisha mbele ya Mwenyezi Mungu.
Na ukirukuu inamaanisha kumuadhimisha Mwenyezi Mungu.
Na ukisujudu ni kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu.
Anaposema: “Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu” anaitikia Mwenyezi Mungu amenishukuru mja wangu, na anaposema “ Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na neema ndogo ndogo” anasema Mwenyezi Mungu: amenisifu mja wangu, na anaposema mwenye kumiliki siku ya mwisho, anasema Mwenyezi Mungu: amenitukuza mja wangu., anaposema kwako wewe nakuabudu na kwako wewe nataka msaada, anasema Mwenyezi Mungu: haya ni kati yangu na mja wangu.
Anaposema ametakasika Mola wangu aliekua mkubwa, na ukisema ametakasika mola wangu alie juu, Mwenyezi Mungu anasikia hata kama ni kwa sauti ya chini,
Kumuomba Mwenyezi Mungu usaidizi wa kufanya amali nzuri, imepokewa na Mtume ﷺ akisema:

[اللهم أعني على ذكرك وشكرك وحسن عبادتك]     أخرجه أحمد وأبوداود والنسائي

[Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie katika kukutaja na kukushukuru, na kufafanya uzuri ibada yako]     [Imepokewa na Ahmad na Abuu Daud na Al-Nnasai]
Vile vile ni muhimu sana Kujua kuwa unyenyekevu ndio roho ya swala, Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

{قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ (1) الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ}   المؤمنون 1-2

[HAKIKA wamefanikiwa Waumini Ambao katika Sala zao huwa ni wanyenyekevu.]   [ Al-Mu’minuun: 1-2]

WITO WAKUHIFADHI SWALA

Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

 {حافظوا على الصلوات والصلاة الوسطى وقوموا لله قانتين}   البقرة:238

[Zilindeni Sala, na khasa Sala ya katikati, na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kuqunuti (kunyenyekea)]     [ AL-Baqarh: 238]

Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

{الَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَوَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ أُولَٰئِكَ هُمُ الْوَارِثُونَ الَّذِينَ يَرِثُونَ الْفِرْدَوْسَ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ}   المؤمنون 9-11

[Na ambao Sala zao wanazihifadhi, Hao ndio warithi, Ambao watairithi Pepo ya Firdausi, wadumu humo.]   [Al-MU’MINUUN:9-11]

KWA FAIDA ZAIDI SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH YUSUF ABDI

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.