AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Mipango yote ya Makuraishi na njama zao zilishindwa, sasa waliamua kurejea kwenye njia zao za zamani za kutesa na kuua Waislam, njia za kikatili ambazo kwazo hawakuwahi kuzitumia kabla. Aidha walianza kufanya maandalizi ya kumwua Mtume (ﷺ). Kinyume na matarajio yao, njia yao hii mpya na fikra hii kwa hakika ilisaidia kuimarisha Da’wa ya Uislamu na ukapata kuungwa mkono kwa kusilimu kwa watu wawili imara na mashujaa wa Makka, nao ni Hamza bin Abdul Muttwalib na ’Umar bin Al-Khattab (Radhi za Allah ziwe juu yao).
Utayba bin Abi Lahab alikwenda kwa Mtume (ﷺ) na akampigia ukelele kwa ufedhuli na kwa sauti kali, akisema
يا محمد إني كافر بالنجم إذا هوى وبالذي دنا فتدلى
Ewe Muhammad mimi namkufu kwa yule alitemsha (Naapa kwa nyota zinapoanguka, na kisha akakurubia (kwa Mtume) na akateremka” (53:8). Kwa maneno mengine: ”Siamini chochote ndani ya Qur’an.”
Kisha akaanza kumfanyia ufedhuli Muhammad (ﷺ), akamshika kwa shari, akampasulia shati lake, na akamtemea mate, lakini hayakufikia uso Mtakatifu wa Mtume (ﷺ). Wakati huo huo Mtume (ﷺ) aliomba ghadhabu ya Allah imwangukie ‘Utayba. Akaomba dua ifuatayo:
اللهم سلط عليه كلباً من كلابك
“Ewe Mwenyezi Mungu msaliti naye mbwa katika mbwa wako.”
Mwenyezi Mungu (s.w.t) Aliijibu dua ya Muhammad (ﷺ). Yafuatayo yalitokea Siku moja ‘Utayba akiwa na wénzake miongoni mwa Makuraishi walikuwa wanaelekea Syria na walilala Az-Zarqa. Simba alilisogelea lile kundi huku ’Utayba akiwa na hofu, alikumbuka maneno ya dua ya Muhammad (ﷺ) na alisema, ”Majonzi kwa ndugu yangu! Kwa hakika huyu simba atanirarua kama Muhammad (ﷺ) alivyoomba.
“Kwa hakika ameniuwa nikiwa Syria wakati yeye yuko Makka.” Simba aliruka kama radi akamnyakua ‘Utayba kutoka katika kundi la watu na akamkata shingoni na kumwua. (1)
Imeripotiwa pia kuwa bazazi mwabudu masanamu katika Makuraishi jina lake ’Uqbah bin Abi Mu’ait siku moja alivyoga shingo ya Mtume (ﷺ), alipokuwa amesujudu wakati akisali, mpaka macho yakatokeza nje (2)
Ibn Ishaq alielezea kwa urefu juu ya ushahidi wa vitendo vya vyenye dhamira ya kumw‘ua Mtume (ﷺ). Abu Jahal, adui mkubwa wa Uislamu wakati mmoja aliwahutubia washirika wenzake: ”Enyi Makureishi, inaelekea Muhammad amedhamiria kuéndelea kuikosoa dini yetu, kuwavunjia heshima mababu zetu, kuidhalilisha njia yetu ya maisha na kuwakashifu miungu wetu. Naapa kwa Iina la Mungu wangu, nitabeba jiwe zito na kumponda nalo Muhammad kichwani, wakati akisujudu ili nikuondoleeni kero. Sijali hatua zitakazochukuliwa na ukoo wake, Banu Abd Manafi. Hadhira ile iliyochanganyikiwa iliafiki mpango ule na wakamshajiisha ayafasiri maneno yake kwa vitendo maridhawa.”
Siku iliyofuata asubuhi, Abu Iahal aliweka mtego akisubiri kuwasili kwa Mtumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) kuja kusali. Makuraishi walikuwa ndani ya nyumba ya mkutano wakisubiri khabari.
Mtume (ﷺ) aliposujudu, Abu Jahal huku amebeba jiwe kubwa alielekea alipokuwa Mtume (ﷺ) ili kutimiza lengo lake. Kabla ya kumsogelea Mtume (ﷺ), uso wake ulisawajika na mikono yake ilitetemeka na
jiwe likadondoka. Wakati huo huo, watu waliokuwa wakitizama walikuja haraka na kutaka kujua kilichotokea. Aliwajibu, ”Alinisongeleaa, ngamia-dume mwenye umbile lisilo la kawaida akifuatana na mbwa wanaotisha walikatiza mbele yangu na karibu wanitafune.”
Ibn Ishaq amesema, maelezo ya Mtume (ﷺ) kuhusu kadhia hii, ni, “Yule alikuwa Jibril (Alayhi Assalam) na Iau Abu Jahal angesogea karibu zaidi, angeumwa ”(3)
Fikra ya Makuraishi ya kutaka kumwua Mtume (s.a.w) haikuwahi kutoweka katika nyoyo zao.
Ibn Ishaq amepokea kutoka kwa Abdillah bin Amri bin Al ‘As (La), kuwa alisema:
“Nilikuwepo wakati walipokutana baadhi ya Makuraishi katika Al- Hijr, wanamtaja Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) na kusema hatujawahi kuona mfano wa mtu huyu kwa jinsi tulivyomvumilia vitimbi vyake. Kwa hakika tumemvumilia sana. Wakati wakiwa katika mazingira hayo, ghafla Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akaingia mahala hapo, akafululiza moja kwa moja mpaka kwenye nguzo iliyokuwemo humo ndani na kuishika, kisha akaanza kuizunguka Al-Ka’aba. Walianza kumkonyéza na kumwambia
mameno ya kejeli, lakini yéye hakujibu kitu, kwa mara zate mbili, kisha akawapita tena kwa mara ya tatu, wakamdhihaki tena. Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alisimama nu kuanza kuwaeleza: ”Enyi Makuraishi, Napa kwa Allah Ambaye Mkononi Mwake ipo roho yangu, kuwa iko siku Mtachinjwa na kukatwa vipande vipande. “
Baada ya Mtume (ﷺ) kutamka neno la kuchinja, wote ‘walisimama wamepigwa na butwaa, na wakawa wanazungumza kwa sauti ya kutetema kwa hofii huku wakijaribu kutuliza hasira zake na huku wakimfariji kwa kusemar ‘Unaweza kuondoka Abul-Qasim kwani hujawahi kuwa mpumbavu”.
Siku iliyofuata walikutana na wakaendelea kumsema na mara Mtume (ﷺ) akatokea, kwa pamoja wakamshika na kumzingira, nilimuona mmoja katika wao akishika nguo yake ilhali, Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake)-akiwa amesimama nyuma yake na’ hali huku akilia na kusema: “Hivi mnamuua mtu kwa kusema tu kuwa Mala wangu ni Mwenyezi Mungu (Subhna wataala)?. Waliposikia kayo wakamzmchia; Bin ‘Amru akasema, “Hakika sijawahi kuona adhabu kubwa kama hii waliyompa .” (4)
Katika upokezi wa Bukhari kutoka kwa ‘Urwah bin’ Az- Zubair (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisemi: ’”Nilimwu!izn Amr bin Al Aa’s anieleze jumbo baya kabisa ambalo Mushirikina waliwahi kumfanyia Mtume (ﷺ).’ Akasema Ipo siku Mtume (ﷺ) alikuwa akisali katika kikuta cha Al-Kaaba, ghafla alitokea “Uqba- bin AI-Mu’ait akaizungusha ngua yake juu ya shingo ya Mtume (ﷺ) akijaribu kumnyonga kwa nguvu. Abubakar (Radhia za Allah ziwe juu yake) alitokea na kumkamata bega lake na kuiondaa ile ngua kutoka kafika shingo ya Mtume (ﷺ) na Akasema: “Hivi mnataka kumwua mtu kwa sababu ya kusema tu kuwa Mola wangu ni AIIah.? ” (5) ‘
Na katika hadithi ya Asmaa inaelezwa: “‘Akatokea ‘mtu kumueleza Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) yaliyomsibu sahibu yake, baada ya kusikia hivyo nae akaharakisha na kufika pale alipo Mtume (ﷺ) na Akasema: Unataka kumwua mtu kwa kusema kwake tu kuwa Mala wake : ni Allah .?’ ” (6) *
1) Tafhiimul Qur’ani Juzuu 6, Uk 522. Mukhtasar Sira Uk 135
2) Ibid Uk 113
3) Ibnu Hisham Juuzu1, Uk 298-299
4) Ibnu Hisham Juuzu1, Uk 289-290
5) Sahihil Bukhari Juuzu1, Uk 544
6) Mukhtasar Siratu Rrasul, Uk 133
*) Arrahiq Al Makhtuum, Uk 169-173