0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAKURAISHI WAMWENDEA TENA ABU-TALIB

AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM

Makuraishi walipoona kuwa Mjumbe wa Allah () bado anashikilia msimamo wake wa kulingania na kutambua kuwa Abu Talib hatomtelekeza mpwa wake, japo hili lingeongeza uadui wao.

Baadhi yao walikwenda kumwona kwa mara nyengine, wakifuatana na aitwaye Amrah bin Al-Walid bin Al MughiIah na wakamwambia, “Ewe Abu Talib! Tumekuletea kijana mtanashati ambaye yuko katika kilele cha ujana, tumia akili na nguvu zake na mchukue kama mwanao kwa kubadilishana na mpwa wako; ambaye anapingana na dini yako, ambaye ameleta mtafaruku katika jamii, na kuikosoa njia yako ya maisha, hivyo tutamwua ili kukuondolea udhia usio na mwisho, sasa mtu kwa mtu” Majibu ya Abu Talib yalikuwa:  Hili ni muhali, mnanipa mtoto wenu nimlee, nami niwape mtoto wangu mumwue! Naapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu,. jambo hili haliwezi kuwal!”
Al-Mut’iim bin Adi, mjumbe wa Makuraishi alisema kumwambia Abu Talib, ”WaIlahi, Ewe Abu Talib Watu wako wamekufanyia uadilifu na wako sahihi katika maamuzi yao kwa sababu wanataka kukuondoshea chanzo cha matatizo, lakini nakuona wataka kukataa Ihsani”

Abu-Talib akamjibu “Wallahi hamukunifanyia uadilifu, mnataka kunidhalilisha, (akawapa changa moto) fanyeni mtakalo.

Kumbukubu za kihisroria hazitupatii tarehe kamili ya mkutano hiyo na Abu-Talib.Inaymkinika ilitokea kwatika mwaka wa sita wa Utume.


 Arraheeq Al Makhtuum Uk 168-169


Begin typing your search above and press return to search.