June 22, 2021
0 Comments
TAFAUTI KATI YA AINA TATU ZA IBADA YA HIJA
Tafauti ilioko kati ya Aina Tatu ya Ibada ya hija
| Tamattu | Qiraan | Ifraad |
| Anahirimia mara mbili, ya kwanza kwa ajili ya ‘Umra kisha atahalalika baada ya hapo, kisha anahirimia kwa ajili ya Hijja | Atahirim hijja na umra kwa pamoja | Atahirimia hija mara moja pekeyake |
| Anapohirimia kwa ajili ya Hijja anasema: “Nimekuitikia ewe Mola wangu Hijja” au anasema: “Nimekuitikia ewe Mola wangu ‘Umra na nitapumzika kwayo hadi Hijja” | Atasema wakati wa kuhirimia (Naitikikia umra na hijja) | Atasema wakati wa kuhirimia (Naitikia hijja) |
| Inawajibika kuchinja | Inawajibika kuchinja | Hawajibiki kuchinja |
| Kuna twawafu mbili, ya kwanza kwa ajili ya ‘Umra na ya pili kwa ajili ya Hijja | Inalazimu twawafu moja nayo ni twawafu ya hajji | Inalazimu twawafu moja nayo ni twawafu ya hajji |
| Kuna sai’ mbili, ya kwanza kwa ajili ya ‘umra na ya pili kwa ajili ya Hijja | Ina sai moja peke nayo ni sai ya hijja | Ina sai moja peke nayo ni sai ya hijja |