SOMO LA MIRATHI
Sababu za kurithi katika sharia ya kiislamu ni tatu kama zifuatazo :-
1. Ndoa :
Makusudio yake ni ndoa ilio sahihi kama ilivyo katika sharia ya kiislamu ,hata kama haikupatikana ndani yake tendo la ndoa. Ndoa ni sababu yakurithiana kati ya mume na mke. Na ikitokea mume kumuacha mke na eda ikaisha basi imekwisha sababu ya kurithiana isipokua akimuacha mkewe akiwa katika hali ya maradhi inao mpelekea kufariki kwa lengo la kumkosecha mirathi basi hapo mkewe atastahiki kurithi na baadhi ya wanazioni wanasema mke atastahiki kurithi hata kama ameolewa na mume mwengine.
2. uhusiano wa kizazi (Jamii) :
Nasaba kiufipi ni muiwano na ukuruba wa kizazi sawa kwa umbali au kwa ukaribu sawa iwe ni kwa upande wa mama au kwa baba au kwa wote.
Nasaba huganyika katika hali tatu kama zifuatavyo :-
a) Uasili:- Nao ni baba wa marehemu na babu wa marehemu na kuendelea.vile vile mama wa marehemu au nyanya wa marehemu na kuendelea.
b) Watoto :- nao ni watoto wa marehemu ,wajuku, vitukuu na vilembekezwa na kuendela.
c) Undugu :- Nao ni ndugu au dada wa marehemu pamoja na watoto wao ,na baba mdogo wa marehemu ,na watoto wa baba mdogo wa marehemu na kuedelea.
Na hii ndio sababu ya nguvu katika kurithiana.
3. Utumwa:
Mtu akimuacha mtumwa huru anastahiki kumrithi mtumwa wake .
Hizi ndizo Sababu za kurithiana ambazo wanachuoni wameafikana,na nisababu zinazo afikiana na akili na maumbile ya binadamu kuwa ni sababu ya kurithiana.