RIWAYA ZA UONGO KUHUSU KABURI LA HUSSEIN(ALLAH AMRIDHIE)
• Mashia ni miongoni mwa watu walio waongo mno na vuka mipaka katika kutukuza na Kuwakwenza watu, zifuatazo ni baadhi tu ya RIWAYA(Hadithi ) za Uongo na zakutunga kuhusu Fadhila za Kuzuru Kaburi la Hussen Bin Ali (Allah awaridhie), Riwaya hizi zina toka katika Vitabu vinavyo tegemewa kwao Mashia (Raafidhwa), Miongoni Riwaya hizo :
1. “إن زيارة قبر الحسين تعدل عشرين حجة، وأفضل من عشرين عمرة وحجة”
“Hakika Kuzuru Kaburi la Hussen ni Sawa na Hija ishirini, na ni bora kuliko Umra na Hija Ishirini”.
Rejea :
فروع الكافي: ١/٣٢٤، ابن بابويه/ ثواب الأعمال: ص٥٢، الطوسي/ تهذيب الأحكام: ٢/١٦، ابن قولويه/ كامل الزيارات: ص١٦١، الحر العاملي/ وسائل الشيعة: ١٠/٣٤٨
MAELEZO :
• Msingi wa maneno haya yaani Kuzuru Kaburi la Hussen(Allah mridhie) kwa Mtazamo na Itikadi ya Kishia ni bora kuliko Hija ambayo ni nguzo ya tano ya Uislamu. Bila shaka hii ghuluu ilio pititiliza Kwa mjukuu wa Bwana Mtume Muhammad (Salla Allah alayhi wasallam), na hii sio Itikadi Sahihi ya Uislamu aliyo ifundisha Bwana Mtume Muhammad (Salla Allah alayhi wasallam).
“من أتى قبر الحسين عليه السلام عارفا بحقه كان كمن حج مائة حجة مع رسول الله صلى الله عليه وسلم”
“Mtu yeyote ambae amekwenda katika Kaburi la Hussen (Allah mridhie) hali yakuwa ana jua haki yake anakuwa kama Mtu alie hiji Hija Mia moja pamoja na Bwana Mtume Muhammad (Salla Allah alayhi wasallam)”.
Rejea :
ثواب الأعمال: ص٥٢، وسائل الشيعة:١٠/٣٥٠
MAELEZO :-
• Ndugu yangu Muislamu tazama Uongo wa watu hawa, na Uvukaji mipaka katika kuwatukuza watu hadi kuwapa Daraja wasizo stahiki.
“فلا يبقى أحد يوم القيامة إلا تمنى يومئذ أنه كان من زوار الحسين عليه السلام”.
“Siku ya Kiyamah hakuna mtu ila atatamani Siku hiyo kuwa alikuwa (Duniani) ni miongoni mwa watu wanao zuru Kaburi la Hussen(Allah mridhie)”.
Rejea :
كامل الزيارات ص١٤٣، وسائل الشيعة: ١/٣٥٣، بحار الأنوار: ١٠١/١٨
MAELEZO :-
• Tazama Uongo huu eti Siku ya Qiyaamah watu watajuta kwanini hawakuwa wanakwenda Karbala kwa ajili ya Kuzuru Kaburi la Hussen! Bila shaka huu ni Uzushi wa hali ya juu dhidi ya Mjukuu wa Bwana Mtume Muhammad (Salla Allah alayhi wasallam) na wala hii sio Itikadi ya Kiislamu hata kidogo.
“إن الله يبدأ بالنظر إلى زوار قبر الحسين بن علي عشية عرفة قبل نظره إلى أهل الموقف”
” Hakika Allah (Azza Wajalla) ana anza kuwatizama watu wenye Kuzuru Kaburi la Hussen usiku wa Arafa kabla ya kuwatizama watu walio simama Arafa”.
Rejea :
الفيض الكاشاني/ الوافي/ المجلد الثاني: ٨/٢٢٢
MAELEZO
• Msingi wa maneno haya ni kuwa Kuzuru Makaburi la Hussen ni Bora kuliko Kisimamo cha Arafa kwa Mahujaji,Hivyo kwa itikaadi ya Kishia ni bora uende Karbala kuzuru Kaburi la Hussein(Allaah amridhie)kuliko uende Hijja.
“من أحب الأعمال زيارة قبر الحسين”
“Miongoni mwa Matendo bora zaidi (Kwa Allah) ni Kuzuru Kaburi la Hussen”.
Rejea :
كامل الزيارات ص١٤٦، بحار الأنوار: ١٠١
MAELEZO :-
• Msingi wa maneno haya ni kuwa Kuzuru Kaburi la Hussen ni miongoni mwa mambo bora mno mbele ya Allah (Azza Wajalla) kuliko hata Hijjah. Bila shaka haya sio mafundisho sahihi ya Uislamu.
“من خرج من منزله يريد زيارة الحسين كتب الله له بكل خطوة حسنة”
” Mtu yeyote ambae ametoka nyumbani kwake kwa ajili ya Kuzuru Kaburi la Hussen Allah ana muandikia mtu huyo kila hatua moja Thawabu moja”.
Rejea-
الطوسي/ تهذيب التهذيب: ٢/١٤، ابن قولويه/ كامل الزيارات: ص١٣٢، ثواب الأعمال: ص٥١، وسائل الشيعة: ١٠/ ٣٤١-٣٤٢
(٣) كامل الزيارات: ص١٣٢، وسائل الشيعة: ١٠/ ٣٤٢، وانظر: ثواب الأعمال ص٥١
MAELEZO :
• Kwa Itikaadi za Kishia kuzuru Kaburi la Hussein kila hatua Moja una lipwa Thawabu , Hizi ni Baadhi tu ya Riwaya na Maelezo ya Uongo na Uzushi kuhusu Kaburi la Hussen bin Ali (Allah awaridhie) ambao Mashia hueneza Uongo huu kuwa eti ni Dini!Bila Shaka hii sio Itikadi ya Uislamu aliyo ifundisha Bwana Mtume Muhammad (Salla Allah alayhi wasallam) wala huyo Hussen wala Ali haja watuma kufanya Ghuluu kwa Kiwango hiki, Hii ni Itikadi ya Abdillah bin Sabai (Myahudi) Muanzilishi wa Itikadi ya Kishia.
Wabillah Taufiiq
Muandishi:-
Ally Yahya Al Qusheiry
Dar es Salaam, Tanzania
+255652082775