0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

NIWAKATI GANI MTU ANAFAA KUTAYAMAMU

SOMO LA FIQHI

1. YANAPOKOSEKANA MAJI

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

{فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا}     المائدة:6

[Na mkitopata maji tayamamuni]   [5: 6].

Na mtu haambiwi kuwa amekosa maji iwapo hakuyatafuta.

2. KUSHINDWA KUYATUMIA MAJI
Kama mgonjwa au mkongwe asiyeweza kutembea, na akawa hana wa kumsaidia kutawadha.

3. WAKATI WA KUCHELEA MADHARA KWA KUTUMIA MAJI
Miongoni mwa hayo:

a) Mgonjwa ambaye angeyatumia maji ugonjwa wake utazidi.

b) Mtu aliye mahali penye baridi kali na asiwe na kitu cha kupasha maji moto na akawa na yakini lau ataoga atapatikana na ugonjwa.

Hii ni kwa hadithi iliyothubutu kuwa Mtume   alimkubalia ‘Amr bin al-’Asw alipowaswalisha wenzake hali akiwa ametayamamu kwa sababu ya baridi kali   [Imepokewa na Abu Daud.].

c) Awapo mahali mbali na hana maji isipokuwa kidogo ambayo anayahitajia kwa kunywa na hawezi kuleta mengine.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.