0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

NEEMA YA PEPO NA ADHABU YA MOTO

NEEMA YA PEPO NA ADHABU YA MOTO

Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Ambaye Ameumba pepo na moto. Mwenye kufanya wema ataingizwa peponi, na Mwenye kufanya mabaya ataingizwa motoni.
Ni nini neema? kila linalo takiwa na kupendeza huitwa neema. Lakini neema ya uhakika ni kufaulu Akhera na kuingia peponi. Pepo ni nyumba ilyo andaliwa watu wema ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala), ndani kuna majumba na mashamba yaliyo na miti tofauti, na mito aina mbali mbali.
Ndugu muislamu katika makala haya mafupi tutaelezea juu ya bidhaa iliyo ghali haipati bidhaa hiyo ila aliye rehemewa na Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Wanaikimbilia biashara hiyo kila mmoja wetu sawa akiwa mume au mke, ni bidhaa iliyo na thamani kubwa inatafutwa na kila mtu. walienda mbio waliopita katika Waislamu na mpaka Waislamu wa sasa kwa lengo la kupata bidhaa hiyo. Na bidhaa hiyo si nyingine bali ni PEPO, iliyo andaliwa wale wote wenye vitendo vyema. Kama pepo ilivyo andaliwa kwa watu wema, vile vile Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)akauandaa moto kwa makafiri na wanafiki na kila anayemuasi Mwenyezi Mungu. Na pepo ni ya wanaomcha Mwenyezi Mungu, na moto ni ya wanaomuasi Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

{وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ}   آل عمران:133

[Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu]    [Al-Imran:133].

Na Akasema tena Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

{فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا وَلَن تَفْعَلُوا فَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ ۖ أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ }    البقرة:24

[Na mkitofanya – na wala hamtofanya kamwe basi uogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe walio andaliwa hao wanao kanusha]   [Al-Baqarah : 24]

Hakika pepo ni nyumba ya wachaji Mungu. Nyumba iliyo neemeshwa imeandaliwa watu wema miongoni mwa Mitume na wa kweli na mashahidi pepo inayo pita chini yake mito, na nyumba ambazo kuta zake ni dhahabu na fedha, ndani yake mna wake wema walio wazuri, ndani yake watu wanakula wala hawaendi haja, kunao ndani ya pepo walio neemeshwa wana furaha siku zote wala hawapati huzuni wanacheka na wala hawalii watakuwa hai siku zote na wala hawatokufa. Nyuso zao zina furaha, ndani yake mna Hurul-‘Ain. Bali watu wa peponi wana neema zaidi na zaidi kwenye pepo mna mambo jicho halijaona wala sikio halijasikia. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

{فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَّا أُخْفِيَ لَهُم مِّن قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ}      السجدة:17

[Nafsi yoyote haijui waliyo fichiwa katika hayo yanayo furahisha macho – ni malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda.]   [Assajdah : 17]

NEEMA ZA PEPO KATIKA HADITHI ZA MTUME ﷺ

Na Hadithi nyingi za Mtume ﷺ zimebainisha hayo. Imepokewa na Abi Hurayra, Akipokea kutoka kwa Mtume ﷺ Anasema: Mwenyezi Mungu alie mshindi na mwenye nguvu:

[أَعْدَدْتُ لِعِبَادِي الصَّالِحِينَ مَا لَا عَيْنٌ رَأَتْ وَلَا أُذُنٌ سَمِعَتْ وَلَا خَطَرَ عَلَى قَلْبِ بَشَرٍ ذُخْرًا بَلْهَ مَا أُطْلِعْتُمْ عَلَيْهِ]    رواه البخاري ومسلم

[Nime waandalia waja wangu wema neema ambao jicho halijaona na wala sikio halijasikia na wala haipiti fikra katika moyo wa mwanadamu]       [Imepokelewa na Bukhari na Muslim]

Vile vile imekuja katika Hadithi za Mtume ﷺ Ameipokea Abu Hurayra Amesema Mtume ﷺ:

أول زمرة يدخلون الجنة على صورة القمر ليلة البدر ، والذين يلونهم على صورة أشد كوكب دري في السماء إضاءة ، لا يبولون ، ولا يتغوطون ، ولا يتفلون ولا يمتخطون ، أمشاطهم الذهب ، ورشحهم المسك ، ومجامرهم الألوة ، وأزواجهم الحور العين ، أخلاقهم على خلق رجل واحد ، على صورة أبيهم آدم ، ستون ذراعا في السماء      رواه البخاري ومسلم

[Hakika [Kundi la kwanza Litakaloingia peponi litaingia kama mwezi wa kumi na nne na wanaofuatia ni kama nyota iliyo mbinguni kwa muangaza wake hawakojoi wala hawaendi haja kubwa wala hawatemi mate wala makohozi vichana vyao ni vya dhahabu pafumu yao ni miski wake zao ni Hurul-‘Ain umbile lao ni moja kwa sura ya baba yao Adam dhiraa sitini kwenda juu.]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Amesema Mtume ﷺ:
[Anayeingia peponi atastarehe wala hangonjeki, wala nguo yake hairaruki wala hawi mzee]    [Muslim]

Vilevile katika kuonesha neema za peponi ni Hadithi ya Abu-Said Al-Khudhriyi na Abu Hurayrah wakipokea kwa Mume ﷺ Amesema:

يُنَادِي مُنَادٍ -يعني في أهل الجنة- : إِنَّ لَكُمْ أَنْ تَصِحُّوا فَلا تَسْقَمُوا أَبَدًا ، وَإِنَّ لَكُمْ أَنْ تَحْيَوْا فَلا تَمُوتُوا أَبَدًا ، وَإِنَّ لَكُمْ أَنْ تَشِبُّوا فَلا تَهْرَمُوا أَبَدًا ، وَإِنَّ لَكُمْ أَنْ تَنْعَمُوا فَلا تَبْأَسُوا أَبَدًا      رواه مسلم

[Atalingania mwenye kulingania Aseme: Hakika uzima ni wenu na hamtakuwa wagonjwa kabisa, na hakika ni wenu nyinyi uhai hamtokufa kabisa, na hakika ni wenu nyinyi ubarobaro hamtakuwa wazee kabisa, na hakika ni zenu nyinyi starehe hamtakuwa na shida kabisa.]    [Imepokewa na Muslim]
[Na wataitwa waambiwe hiyo ndiyo pepo mlio ridhishwa ni malipo yale mliyoyafanya].

MOTO NA WATU WAMOTONI

Baada ya kuzungumzia watu wa peponi na starehe zao. Kidogo tuizungumzie hali ya watu wa motoni na sifa zao na hali ya moto, ndani ya moto mna vinywaji vikali. Hakika moto ni nyumba ya watu wabaya, na ni nyumba ya adhabu kama Alivyosema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

{لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ}   الأنعام:70

[Wao watapata kinywaji cha maji ya moto kabisa, na adhabu chungu ]    [An-Aam : 70].

Na Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

{وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ}     يونس:4

[Na walio kufuru, wao watapata vinywaji vinavyo chemka, na adhabu chungu kwa sababu ya walivyo kuwa wakikufuru.]      [Yuunus : 4]

Kwa hivyo, Moto ni mahali pa watu wabaya wanaokosea amri ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Kama Alivyosema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

{هَٰذَا ۚ وَإِنَّ لِلطَّاغِينَ لَشَرَّ مَآبٍ جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا فَبِئْسَ الْمِهَادُ}    ص:55-56

[Ndio hivi! Na hakika wenye kuasi bila ya shaka watapata marudio maovu kabisa, Nayo ni Jahannamu! Wataingia humo. Nacho hicho ni kitanda kiovu mno cha kulalia]    [Saad : 55-56].
Na katika kukamilisha kuelezea habari ya moto na sifa zake ni Hadithi ya Shaqiq. Imetokana na shaqiq amepokea kwa ‘Abdillahi Akisema: Amesema Mtume ﷺ

[يؤتى بجهنم يوم القيامة لها سبعون ألف زمام مع كل زمام سبعون ألف ملك يجرونها]    رواه مسلم

[Utaletwa moto siku hiyo umefungwa vifungo sabini elfu na kila kifungo kimoja kina vutwa na Malaika sabini elfu, wanauburuza]   [Imepokewa na Muslim]
Tunamuomba Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Atuepushe na moto wa Jahannam Atujaalie ni katika wenye kusikia mema pamoja na kuyafuata.

SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH HASSAN SUGO

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.