0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MWAKILISHI WA MAKURAISH KWA MTUME ﷺ


AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Baada ya kusilimu hawa mashujaa wawili watukufu, Hamza bin Abdil Mutwalib na ‘Umar bin al-Khattab (Radhi za Allah ziwe juu yao), mawingu ya udhalimu na mateso dhidi ya Waislamu yalianza  kutanzuka na Mushirikina wa Makka walianza kuona kuwa hakuna maana tena ya kuendelea kuwatesa Waislamu. Washirikina wakaanza kubadilisha mbinu za mapambano na kuanza kujadiliana na Mtume () kwa kupinga hoja zake. jambo ambalo lilikuwa gumu nmo kwao. Yote haya waliyafanya kwa lengo la kutaka kumzuia kufanya kazi ya Da’awa na kufikisha ujumbe aliotumwa Mwenyezi Mumgu {).

Kwa ujinga wao, hawakuwa wakifahamu maskini kuwa walikuwa wakishindana na mtu ambaye kamwe wasingeweza kumshinda, na kuwa Alichokikusudia Mwenyezi Mungu () ndicho kitakachokuwa. Hata baada ya juhudi zote walizofanya hawakuweza kufanikiwa na hawakuambulia kitu. Wakashindwa katika lile ambalo walikuwa wamelikusudia.

Ibnu Is’haq alisema kuwa, alipokea kutoka kwa Yazidi bin Ziadi aliyepokea kutoka kwa Muhammad bin Kaab Al- Quradhy, alisema; ”Nimeelezwa kuwa ’Utbah bin Rabia (miongoni mwa watukufu wa Kikuraish), alisemaz ”Siku moja wakati akiwa kafika Jumba la mikutano la Makuraishi, na Mtume () akiwa amekaa msikitini peke yake, alisema: ”Enyi jamaa miongoni mwa Makuraishi!, hivi sisi tunashindwa kweli kupata njia ya kumdhibiti Muhammad na harakafi zake? Enyi Makuraishi! mnaonaje kama nikimuendea Muhammad na kuzungumza nae na kujaribu kumpendekezea mambo kadhaa ambayo natumai kuwa atayaridhia baadhi yake na kumuahidi kumpa chochote akitakacho ili mradi aache kuhubiri khabari za Mungu wake?.”

Jambo hili lilifanyika wakati aliposilimu Hamza (Radhi za Allah ziwe juu yake) na Mushirikina kuona kuwa Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu () wanazidi kuongezeka idadi yao na kuwa wengi. Wakasema; ”Bila shaka Abul Wahid, nenda uzungmze nae.” Hapo ndipo ’Utbah aliposimama na kwenda mpaka alipomfikia Mtumbe wa Mwenyezi Mungu () na kusema: “Ewe mtoto wa ndugu yangu, kwa hakika wewe unajua daraja kubwa na cheo ulichonacho miongoni mwetu kwa uzao wako na nasabu yako. Kwa hakika umewaletea jamaa zako jambo kubwa sana, na kwa jambo hilo umeutenganisha mkusanyiko wao. Umedharau mwendo wao wa fikra na umeharibu ndoto zao. Umeaibisha kwa jambo hili miungu yao, dini yao, na kwa jambo lako hili umewakufurisha pia waliopita katika baba zao. Nisikilize, nitawasilisha kwako mapendekezo ambayo ninataka uyachunguze, na huenda ndani yake ukakubali baadhi yake.” Mtume wa Mwenyezi Mungu () akasema, ”Sema ewe Abdul-Walid, ninakusikiliza” akasema: “Ewe mtoto wa ndugu yangu, kwa hakika hakuna jambo jingine isipokuwa utueleze kuhusu hili ulilokuja nalo, kama unataka ‘Mali ili uliache tutakukusanyia mali zetu ‘na kukufanya kuwa tajiri kuliko mtu yeyote miongoni mwetu, na kama kwa jambo hili unataka utukufu basi tutakufanya Bwana wetu kiasi cha kutopitisha uamuzi wowote bila ya idhini yako, na ikiwa unataka utawala tutakufanya uwe Mfalme wetu, na kama hili linalokujia ni jini unaloliona na huwezi kulifukuza likawa mbali na nafsi yako tutakutafutia mganga na sisi tutatoa mali zetu katika jambo hili mpaka tukuponye.”

Mtume wa Mwenyezi Mungu () alimsikiliza ’Utbah kwa makini mpaka alipomaliza, na kisha akamuuliza, ”UmemaIiza ewe Abul-Walid?” Naye akajibu: ndiyo.  Mtume () akaanza kusoma

حمٓ (1) تَنزِيلٞ مِّنَ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ (2) كِتَٰبٞ فُصِّلَتۡ ءَايَٰتُهُۥ قُرۡءَانًا عَرَبِيّٗا لِّقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ (3) بَشِيرٗا وَنَذِيرٗا فَأَعۡرَضَ أَكۡثَرُهُمۡ فَهُمۡ لَا يَسۡمَعُونَ (4) وَقَالُواْ قُلُوبُنَا فِيٓ أَكِنَّةٖ مِّمَّا تَدۡعُونَآ إِلَيۡهِ وَفِيٓ ءَاذَانِنَا وَقۡرٞ وَمِنۢ بَيۡنِنَا وَبَيۡنِكَ حِجَابٞ فَٱعۡمَلۡ إِنَّنَا عَٰمِلُونَ (5)

Bismillahir Rahmanir Rahiim ” Han Mym. Uteremsho huu umetoka kwa Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu Hichi ni Kitabu kilicho pambanuliwa Aya zake, cha kusomwa kwa Kiarabu kwa watu wanao jua.Kitoacho khabari njema, na chenye kuonya. Lakini wengi katika wao wamepuuza; kwa hivyo hawasikii.Na wakasema: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa hayo unayo tuitia, na masikio yetu yana uziwi, na baina yetu na wewe lipo pazia. Basi wewe tenda, nasi tunatenda. ”   (41:1-5)

Mtume (() aliendelea kumsomea kutoka Sura hiyo, ’Utbah Alinyamaza na kusikiliza kwa makini ilhali mikono yake ameiweka nyuma akiwa ameegemea. Mtume wa Mwenyezi Mungu () aliendelea mpaka katika aya iliyohimiza sijida, akasujudu kisha akamwabia’ Utbah, “Umeyasikia majibu yangu hivyo una  hiari; kufanya utakalo,” ’Utbah alisimama kurudi kwa wenzaké.

Walipomuona jinsi alivyosawajika, baadhi yao waliwaambia wenzi wao tunaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu (), kwa hakika Abul-Waljd anawajieni katika hali sio ile aliyoondoka nayo. Aipofika walimuhoji kwa kumuuliza, Ni jambo gani lililokusibu Ewe Abul-Wa.lid?  Naye akawajibu kwa kusema; “Mimi nimesikia maneno ambayo Ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu () sijawahi kusikia mfano wake kabla ya leo. Ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu (), maneno hayo siyo mashairi, wala siyo uchawi na wala si maneno ya kuhani. Enyi jamaa zangu Makuraishil, ninakuombeni acheni hayo na mwacheni na mambo yake na jivueni nae. Kwa hiyo kaeni mbali naye. Ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu (), kwa hakika maneno ambayo nimeyasikia leo kwake yatakuwa na khabari kubwa sana iwapo Waarabu watamsikia na ikitokea kuwa watamdhuru hivyo itakuwa mumetoshelezwa na watu wengine. Lakini (Muhammad) akiwashinda Waarabu, ufalme wake utakuwa ni ufalme wenu na utukufu wake utakuwa ni utukufu wenu, na mtakuwa watu miongoni mwa watu walio na mafanikio makubwa kuliko watu wengine kwa sababu Yake. ”

Baada ya Makuraishi kumsikiliza Mjumbe wao, wakamwambia, ”Amekuroga!. Tunaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu, Ewe Abul-Walidl huyu amekuroga kwa ulimi wake”, naye akawajibu; “Haya ndiyo maoni yangu kwake kwa hivyo fanyeni lile ambalo mnaona linafaa. (1)

Katika mapokezi mengine inaelezwa kuwa ‘Utbah, aliendelea kusikiliza aya’ za Qur’ani ambazo Mtume () alikuwa akisoma mpaka alipofikia kwenye Kauli Yake Mwenyezi Mungu () Aliye Mtukufu:

فَإِنۡ أَعۡرَضُواْ فَقُلۡ أَنذَرۡتُكُمۡ صَٰعِقَةٗ مِّثۡلَ صَٰعِقَةِ عَادٖ وَثَمُودَ (13)

 “Basi wakipuuza wewe sema: Nakuhadharisheni adhabu mfano wa adhabu ya A’di na Thamudi,” (41:13) ‘Utbah akasimama hali ya kuwa ni mwenye kufadhaika na akauweka mkono wake juu ya mdomo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu () huku akisema, “Ninakuomba kwa jina la Mwenyezi Mungu () na kwa udugu na hilo ni kwa kuogopa kutoka katika lile ambalo limetahadharishwa (wasije wakangamia Makuraishi).” Akarudi kwa watu waliomtuma na akasema yale aliyoyasema. (2)


1) Ibnu Hishaam Juzaa 1, Uk 293-294
2) Tafsiri ibn Kathir Juzuu 6 Uk. 159-160-161,
3) Arrahiiq Al Makhtuum, Uk 184-189

Begin typing your search above and press return to search.