الأصول الثلاثة
الأَصْلُ الثَّالِث: مَعْرِفَةُ نَبِيِّكُمْ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:وَهُوَ مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللهِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ بْنِ هَاشِمٍ، وَهَاشِمٌ مِنْ قُرَيْشٍ، وَقُرَيْشٌ مِنَ الْعَرَبِ، وَالْعَرَبُ مِنْ ذُرِّيَّةِ إِسْمَاعِيلَ بْنِ إِبْرَاهِيمَ الْخَلِيلِ عَلَيْهِ وَعَلَى نَبِيِّنَا أَفْضَلُ الصَّلاةِ وَالسَّلامِ، وَلَهُ مِنَ الِعُمُرِ ثَلاثٌ وَسِتُّونَ سَنَةً، مِنْهَا أَرْبَعُونَ قَبْلَ النُّبُوَّةِ، وَثَلاثٌ وَعِشْرُون َفى النبوة. نُبِّئَ ب (إقْراء) ، وَأُرْسِلَ ب (الْمُدَّثِّرْ)، وَبَلَدُهُ مَكَّةُ. بَعَثَهُ اللهُ بِالنِّذَارَةِ عَنِ الشِّرْكِ، وَبالَدْعُوة إِلَى التَّوْحِيدِ
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
{يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ قُمْ فَأَنذِرْ وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ وَلَا تَمْنُن تَسْتَكْثِرُ وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ}
وَمَعْنَى {قُمْ فَأَنذِرْ} يُنْذِرُ عَنِ الشِّرْكِ، وَيَدْعُو إِلَى التَّوْحِيدِ
{وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ} أَيْ: عَظِّمْهُ بِالتَّوْحِيدِ
{وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ} أَيْ: طَهِّرْ أَعْمَالَكَ عَنِ الشِّرْكِ}
{وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ} الرُّجْزَ: الأَصْنَامُ، وَهَجْرُهَا: تَرْكُهَا، وَالْبَرَاءَةُ مِنْهَا وَأَهْلُهَا}
أَخَذَ عَلَى هَذَا عَشْرَ سِنِينَ يَدْعُو إِلَى التَّوْحِيدِ، وَبَعْدَ الْعَشْرِ عُرِجَ بِهِ إِلَى السَّمَاءِ، وَفُرِضَتْ عَلَيْهِ الصَّلَواتُ الْخَمْسُ، وَصَلَّى فِي مَكَّةَ ثَلاثَ سِنِينَ، وَبَعْدَهَا أُمِرَ بالْهِجْرَةِ إِلَى الْمَدِينَةِ، وَالْهِجْرَةُ الانْتِقَالُ مِنْ بَلَدِ الشِّرْكِ إِلَى بَلَدِ الإِسْلامِ
وَالْهِجْرَةُ فَرِيضَةٌ عَلَى هَذِهِ الأُمَّةِ مِنْ بَلَدِ الشِّرْكِ إِلَى بلد الإِسْلامِ، وَهِيَ بَاقِيَةٌ إِلَى أَنْ تَقُومَ السَّاعَةُ
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚ قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا إِلَّا الْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلًا فَأُولَـٰئِكَ عَسَى اللَّـهُ أَن يَعْفُوَ عَنْهُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَفُوًّا غَفُورًا
وَقَوْلُهُ تَعَالَى:
{يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ أَرْضِي وَاسِعَةٌ فَإِيَّايَ فَاعْبُدُونِ} العنكبوت:56}
قَالَ الْبُغَوِيُّ (رَحِمَهُ اللهُ) :نزلت هَذِهِ الآيَةِ فِي المُسْلِمِينَ الَّذِينَ بِمَكَّةَ ولَمْ يُهَاجِرُوا، نَادَاهُمُ اللهُ بِاسْمِ الإِيمَانِ
وَالدَّلِيلُ عَلَى الْهِجْرَةِ مِنَ السُّنَّةِ، : قَوْلُهُ صلى الله عليه وآله وسلم
[لاَ تَنْقَطِعُ الْهِجْرَةُ حَتَّى تَنْقَطِعَ التَّوْبَةُ، وَلا تَنْقَطِعُ التَّوْبَةُ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِهَ]
فَلَمَّا اسْتَقَرَّ فِي الْمَدِينَةِ أُمِرَ بِبَقِيَّةِ شَرَائِعِ الإِسْلامِ، مِثلِ: الزَّكَاةِ، وَالصَّوْمِ، وَالْحَجِّ، وَالأَذَانِ، وَالْجِهَادِ، وَالأَمْرِ بِالْمَعْرُوفِ وَالنَّهْيِ عَنِ الْمُنْكَرِ، وَغَيْرِ ذَلِكَ مِنْ شَرَائِعِ الإِسْلامِ، أَخَذَ عَلَى هَذَا عَشْرَ سِنِينَ، وَتُوُفِّيَ ـ صَلواتُ اللهِ وَسَلامُهُ عَلَيْهِ ـ وَدِينُهُ بَاقٍ. وَهَذَا دِينُهُ، لا خَيْرَ إِلا دَلَّ الأُمَّةَ عَلَيْهِ، وَلا شَرَّ إِلا حَذَّرَهَا مِنْهُ، وَالْخَيْرُ الَّذِي دَلَّهَا عَلَيْهِ التَّوْحِيدُ، وَجَمِيعُ مَا يُحِبُّهُ اللهُ وَيَرْضَاهُ، وَالشَّرُ الَّذِي حَذَّرَهَا مِنْهُ الشِّرْكُ، وَجَمِيعُ مَا يَكْرَهُ اللهُ وَيَأْبَاهُ. بَعَثَهُ اللهُ إِلَى النَّاسِ كَافَّةً، وَافْتَرَضَ طَاعَتَهُ عَلَى جَمِيعِ الثَّقَلَيْنِ الْجِنِّ وَالإِنْسِ
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
{قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا}
وَكَمَّلَ اللهُ بِهِ الدِّينَ؛ وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
{الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا}
:وَالدَّلِيلُ عَلَى مَوْتِهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وآله وَسَلَّمَ) قَوْلُهُ تَعَالَى
{إِنَّكَ مَيِّتٌ وَإِنَّهُم مَّيِّتُونَ ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عِندَ رَبِّكُمْ تَخْتَصِمُونَ }
وَالنَّاسُ إِذَا مَاتُواْ يُبْعَثُونَ
الدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
{مِنْهَا خَلَقْنَاكُمْ وَفِيهَا نُعِيدُكُمْ وَمِنْهَا نُخْرِجُكُمْ تَارَةً أُخْرَىٰ}
وقَوْلُهُ تَعَالَى:
{وَاللَّـهُ أَنبَتَكُم مِّنَ الْأَرْضِ نَبَاتًا ثُمَّ يُعِيدُكُمْ فِيهَا وَيُخْرِجُكُمْ إِخْرَاجًا}
وَبَعْدَ الْبَعْثِ مُحَاسَبُونَ وَمَجْزِيُّونَ بِأَعْمَالِهِمْ
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
{وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ أَسَاءُوا بِمَا عَمِلُوا وَيَجْزِيَ الَّذِينَ أَحْسَنُوا بِالْحُسْنَى}
وَمَنْ كَذَّبَ بِالْبَعْثِ كَفَرَ
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
{زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن لَّن يُبْعَثُوا ۚ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ ۚ وَذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ}
وَأَرْسَلَ اللهُ جَمِيعَ الرُّسُلِ مُبَشِّرِينَ وَمُنْذِرِينَ
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
{رُّسُلًا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّـهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ}
وَأَّولُهُمْ نُوحٌ (عَلَيْهِ السَّلامُ)، وَآخِرُهُمْ مُحَمَّدٌ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وآله وَسَلَّمَ) وَهُوَ خَاتَمُ النَّبِيِّينَ
وَالدَّلِيلُ عَلَى أَنَّ أَوَّلَهُمْ نُوحٌ قَوْلُهُ تَعَالَى:
{إِنَّا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ كَمَا أَوْحَيْنَا إِلَىٰ نُوحٍ وَالنَّبِيِّينَ مِن بَعْدِهِ}
وَكُلُّ أُمَّةٍ بَعَثَ اللهُ إِلَيْهِا رَسُولا مِنْ نُوحٍ إِلَى مُحَمَّدٍ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وآله وَسَلَّمَ) يَأْمُرُهُمْ بِعِبَادَةِ اللهِ وَحْدَهُ، وَيَنْهَاهُمْ عَنْ عِبَادَةِ الطَّاغُوتِ
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
وَافْتَرَضَ اللهُ عَلَى جَمِيعِ الْعِبَادِ الْكُفْرَ بِالطَّاغُوتِ وَالإِيمَانَ بِاللهِ
قَالَ ابْنُ الْقَيِّمِ (رَحِمَهُ اللهُ): مَعْنَى الطَّاغُوتِ مَا تَجَاوَزَ بِهِ الْعَبْدُ حَدَّهُ مِنْ مَعْبُودٍ أَوْ مَتْبُوعٍ أَوْ مُطَاعٍ. وَالطَّوَاغِيتُ كَثِيرُونَ وَرُؤُوسُهُمْ خَمْسَةٌ: إِبْلِيسُ لَعَنَهُ اللهُ، وَمَنْ عُبِدَ وَهُوَ رَاضٍ، وَمَنْ دَعَا النَّاسَ إِلَى عِبَادَةِ نَفْسِهِ، وَمَنْ ادَّعَى شَيْئًا مِنْ عِلْمِ الْغَيْبِ، وَمَنْ حَكَمَ بِغَيْرِ مَا أَنْزَلَ اللهُ.
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
{لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ ۚ فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ}
وَهَذَا هُوَ مَعْنَى لا إلٰه إِلا اللهُ
[وَفِي الْحَدِيث: [رَأْسُ الأَمْرِ الإِسْلامِ، وَعَمُودُهُ الصَّلاةُ، وَذِرْوَةُ سَنَامِهِ الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ]
وَاللهُ أَعْلَمُ. وَصَلَّى اللهُ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعلى آلٰه وَصَحْبِهِ وَسَلَّمَ
Msingi Wa Tatu: Kumjua Mtume wenu Muhammad ﷺ
Naye ni Muhammad bin ‘Abdillaah bin ‘Abdil-Muttwalib bin Haashim. Na Haashim ni kutoka katika (kabila la) la Quraysh. Na Quraysh ni katika Waarabu. Na Waarabu ni kutokana na kizazi cha Ismaail bin Ibraahim Al-Khaliyl (Swalaa na salamu bora kabisa ziwafikie yeye na Nabiy wetu). Naye alikuwa na umri wa miaka Sitini na tatu, miongoni mwa miaka hiyo miaka Arubaini kabla ya kutumilizwa, na miaka Ishirini na tatu akiwa Mtume. Akapewa Unabii kwa kuambiwa: (Iqraa) -Soma na akatumilizwa kufikisha ujumbe kwa kuteremshiwa (sura ya) Al-Muddath-thir – (mwenye kujigubika). Na mji wake ni Makkah. Mwenyezi Mungu Amemtuma kuonya kuhusu shirki na kulingania katika Tawhiyd.(kumpekesha Mwenyezi Mungu)
Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Ewe uliye jigubika! Simama uonye!Na Mola wako Mlezi mtukuze! Na nguo zako, zisafishe Na yaliyo machafu yahame! Wala usitoe kwa kutaraji kuzidishiwa.Na kwa ajili ya Mola wako Mlezi, subiri!] [Al-Muddaththir:1-7]
Na maana ya [Simama na uonye]: Aonye kuhusu shirki na alinganie katika Tawhiyd.
[Na Mola wako mlezi mtukuze] : Yaani Muadhimishe kwa kumpwekesha.
[Na nguo zako zisafishe] Yaani: Toharisha ‘amali zako kutokana na shirk.
[Na yalio machafu (masanamu) yahae] Uchafu au najsi ni masanamu. Na kuyahama ni kuepukana nayo kabisa na kujiweka mbali nayo na watu wake.
Amesimamia haya miaka kumi akilingania katika Tawhid. Na baada ya miaka kumi, alipandishwa mbinguni (Mi’iraaj) na akafaridhishwa Swala tano, akaswali Makkah miaka mitatu, na baada ya hapo akaamrishwa kugura kwenda Madina. Na hijrah ni kuhama kutoka nchi ya shirki kwenda katika nchi ya Kiislamu.
Na hijrah ni faradhi kwa Umma huu kuhama kutoka katika nchi ya shirki kwenda nchi ya Kiislamu. Nayo itaendelea kubakia hadi itakaposimama Qiyama.
Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Hakika Malaika watawaambia wale ambao wamewafisha nao wamejidhulumu nafsi zao: Mlikuwa vipi? Watasema: Tulikuwa tunaonewa. Watawaambia: Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa na wasaa wa kuhamia humo? Basi hao makaazi yao ni Jahannamu, nayo ni marejeo mabaya kabisa.Isipo kuwa wale walio kuwa wanyonge miongoni mwa wanaume na wanawake na watoto wasio na uweza wa hila ya kuongoza njia ya kuhama.Basi hao huenda Mwenyezi Mungu akawasamehe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa maghfira] [An-Nisaai:97-99]
Na kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Enyi waja wangu mlio amini! Kwa hakika ardhi yangu ina wasaa. Basi niabuduni Mimi peke yangu.] [Al A’nkabut:56]
Amesema Al-Baghaawiy (Mungu amrahamu): “Aya hii imeteremshwa kwa sababu ya Waislamu waliokuwa Makkah ambao hawakuhama. Mwenyezi Mungu Amewaita kwa jina la Waumini.
Na dalili ya Kugura katika Sunna ni kauli yake Mtume ﷺ:
[Hijrah haikatiki mpaka ikatike Tawba. Na Tawba haikatiki mpaka jua lichomoze kutoka Magharibi] [Imepokewa na Ahmad na Abuu Dawuud]
Baada ya kutulia Madina aliamrisha Sheria za Kiislamu zilobakia kama; Zakah, Saumu, Hajj, Adhana, Jihaadi, kuamrisha mema na kukataza maovu na mengineyo ya Sheria ya Kiislamu. Amefanya hayo miaka kumi akafariki baada ya hapo, (Swala na salamu ziwe juu yake.) Na Dini yake imebaki. Na hii Dini yake, hakuna kheri isipokuwa kawaelekeza kwayo Umma, na hakuna shari ila amewatahadharisha nayo. Na kheri aliyowaongoza kwayo ni Tawhid (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) na yote Anayoyapenda Mwenyezi Mungu na Anayoyaridhia. Na shari ambazo amezitahadharisha ni shirki na yote yanayomchukiza Mwenyezi Mungu na Asiyoyaridhia. Mwenyezi Mungu Amemtuma kwa watu wote, na Amefaradhisha Viumbe viwili; majini na watu kumtii yeye (Mtume ﷺ).
Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote.] [Al-A’raaf:158]
Na Mwenyezi Mungu Ameikamilisha Dini hii kwa kupitia kwake. Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ
[Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini.] [Al-Maida:3]
Na dalili ya kifo chake (Mtume ﷺ) ni kauli yake Mwenyezi Mungu:
[Kwa hakika wewe utakufa, na wao watakufa. Kisha bila ya shaka mtagombana Siku ya Kiyama mbele ya Mola wenu Mlezi.] [Azzumar:30-31]
Na watu watakapokufa watafufuliwa.
Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Na mlipo sema: Ewe Musa! Hatutakuamini mpaka tumwone Mwenyezi Mungu waziwazi. Ikakunyakueni radi nanyi mnaangalia.] [Surat Ta’ha:55]
Na kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Na Mwenyezi Mungu amekuotesheni katika ardhi kama mimeaKisha atakurudsheni humo na atakutoeni tena.] [Surat Nuh’:18]
Na baada ya kufufuliwa watahesabiwa na watalipwa kwa Amali zao.
Na dalil ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, ili awalipe walio tenda ubaya kwa waliyo yatenda, na walio tenda mema awalipe mema.] [Annajm:31]
Na anayekadhibisha kufufuliwa amekufuru.
Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Walio kufuru wanadai kuwa hawatafufuliwa. Sema: Kwani? Naapa kwa Mola wangu Mlezi! Hapana shaka mtafufuliwa, na kisha hapana shaka mtaambiwa mliyo yatenda. Na hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu.] [Attaghaabun:7]
Na Mwenyezi Mungu Ametuma Mitume wote wakiwa ni wabashiriaji na waonyaji.
Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Mitume hao ni wabashiri na waonyaji, ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletewa Mitume] [An-Nisaai:165]
Na wa kwanza wao ni Nuuh (Alayhi Salaam) na wa mwisho wao ni Muhammad ﷺ naye ndiye Mtume wa mwisho.
Na dalili kwamba Nuuh ndie Nabii wa mwanzo wao ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Hakika Sisi tumekuletea wahyi wewe kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na Manabii walio kuwa baada yake.] [An-Nisaai:163]
Na kila Umma Mwenyezi Mungu Amemtumiliza Mtume kuanzia Nuuh hadi kwa Muhammad ﷺ. Akiwaamrisha kumwabudu Mwenyezi Mungu Pekee, na Akiwakataza kuabudu twaghuti
Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani.] [An Nahl:36].
Na Mwenyezi Mungu Akafaridhisha kwa waja wote wamkanushe twaghuti na kumwamini Mwenyezi Mungu (wamwabudu Yeye Pekee).
Ibnul Qayyim (Mungu amrahamu) amesema: “Maana ya twaghuti ni kila anachopindukia mja mipaka yake; ikiwa ni kinachoabudiwa, au kinachofuatwa au kinachotiiwa. Na matwaghuti ni wengi. Wakuu wao ni watano; Ibliis laana za Allaah ziwe juu yake, na anayeabudiwa hali ya kuwa yeye yuko radhi, na anayeita watu wamwabudu yeye, na anayedai kujua elimu ya ghayb (yaliofichika), na anayehukumu yale ambayo Hakuyateremsha Mwenyezi Mungu.”
Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet’ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.] [Al-Baqara:256]
Na hii ndio maana ya Laa ilaaha illa-Allaah (hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu ﷻ.
Na katika Hadithi:
[Msingi wa mambo ni Uislamu, na nguzo yake ni Swala na kilele cha nundu yake ni kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu] [65]
Na Allaah Anajua zaidi na rehma na amani zimfikie Mtume Muhammadi na Aali zake na Maswahaba wake.