0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

DARAJA YA TATU: IHSAAN

الأصول الثلاثة


الْمَرْتَبَةُ الثَّالِثَةُ: الإِحْسَانُ

رُكْنٌ وَاحِدٌ كما فى الحديث: [أَنْ تَعْبُدَ اللهَ كَأَنَّكَ تَرَاهُ، فَإِن لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فَإِنَّهُ يَرَاكَ ]

وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى

{إِنَّ اللَّهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ}    النحل:128}

وقَوْلُهُ تَعَالَى:

{وَتَوَكَّلْ عَلَى الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ وَتَقَلُّبَكَ فِي السَّاجِدِينَ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ}   الشعراء:217-220}

وقَوْلُهُ تَعَالَى:

{وَمَا تَكُونُ فِي شَأْنٍ وَمَا تَتْلُو مِنْهُ مِن قُرْآنٍ وَلَا تَعْمَلُونَ مِنْ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيْكُمْ شُهُودًا إِذْ تُفِيضُونَ فِيهِ}     يونس:64}

وَالدَّلِيلُ مِنَ السُّنَّةِ حَدِيثُ جِبْرِيلَ الْمَشْهُورُ

عَنْ عُمَرَ بنِ الْخَطَّابِ (رضي الله عنه) قَالَ: بَيْنَمَا نَحْنُ جُلُوسٌ عِنْدَ النَّبِيِّ ﷺ إِذْ طَلَعَ عَلَيْنَا رَجُلٌ، شَدِيدُ بَيَاضِ الثِّيَابِ، شَدِيدُ سَوَادِ الشَّعْرِ، لا يُرَى عَلَيْهِ أَثَرُ السَّفَرِ، وَلا يَعْرِفُهُ مِنَّا أَحَدٌ، فَجَلَسَ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وآله وسلم فَأَسْنَدَ رُكْبَتَيْهِ إِلَى رُكْبَتَيْهِ، وَوَضَعَ كَفَّيْهِ عَلَى فَخِذَيْهِ، وَقَالَ: يَا مُحَمَّدُ أَخْبِرْنِي عَنِ الإِسْلامِ فَقَالَ: [أَنْ تَشْهَدَ أَنْ لا إلٰه إِلا اللهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ، وَتُقِيمَ الصَّلاةَ، وَتُؤْتِيَ الزَّكَاةَ، وَتَصُومَ رَمَضَانَ، وَتَحُجَّ الْبَيْتَ إِنْ اسْتَطَعْتَ إِلَيْهِ سَبِيلا] .قَالَ: صَدَقْتَ. فَعَجِبْنَا لَهُ يَسْأَلُهُ وَيُصَدِّقُهُ. قَالَ: أَخْبِرْنِي عَنِ الإِيمَانِ. قَال: [أَنْ تُؤْمِنَ بِاللهِ، وَمَلائِكَتِهِ، وَكُتُبِهِ، وَرُسُلِهِ، وَالْيَوْمِ الآخِرِ، وَتُؤْمِنَ بِالْقَدَرِ خَيْرِهِ وَشَرِّهِ] قَالَ: صَدَقْتَ. قَالَ: أَخْبِرْنِي عَنِ الإِحْسَانِ. قَال: [أَنْ تَعْبُدَ اللهَ كَأَنَّكَ تَرَاهُ، فَإِنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فَإِنَّهُ يَرَاكَ] قَالَ: أَخْبِرْنِي عَنِ السَّاعَةِ. قَالَ: [مَا الْمَسْؤُولُ عَنْهَا بِأَعْلَمَ مِنَ السَّائِلِ] .قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنْ أَمَارَاتِهَا. قَالَ: [أَنْ تَلِدَ الأَمَةُ رَبَّتَهَا، وَأَنْ تَرَى الْحُفَاةَ الْعُرَاةَ الْعَالَةَ رِعَاءَ الشَّاءِ يَتَطَاوَلُونَ فِي الْبُنْيَانِ] .قَالَ: فَمَضَى، فَلَبِثْنَا مَلِيَّا، فَقَالَ: [يَا عُمَرُ أَتَدْرُونَ مَنِ السَّائِلِ؟] قُلْنَا: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: [هَذَا جِبْرِيلُ أَتَاكُمْ يُعَلِّمُكُمْ أَمْرَ دِينِكُم

Daraja Ya Tatu: Ihsaan

Nguzo yake ni moja kama katika Hadithi: [Ni kumwabudu Mwenyezi Mungu kama kwamba unamuona, na hata kama humuoni, basi Yeye Anakuona]   [Imepokewa na Muslim]

Na dalili ni kauli Yake Mwenyezi Mungu ﷻ:

[Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kumcha, na watendao mema]  [An Nahl:128]

Na kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:

[Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemuAmbaye anakuona unapo simama,Na mageuko yako kati ya wanao sujuduHakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.]  [Shu’araa: 217-220]

Na kauli yake Mwenyezi Mungu:

[Na huwi katika jambo lolote, wala husomi sehemu yoyote katika Qur’ani, wala hamtendi kitendo chochote ila Sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnapo shughulika nayo.]  [Yunus:64].

Na dalili katika Sunna ni Hadithi mashuhuri ya Jibril:

Kutoka kwa ‘Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: Siku moja tulikuwa tumekaa na Mtume ﷺ, hapo alitokea mtu ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama ya machofu ya safari na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi anaemjua. Alienda akakaa karibu na Mtume ﷺ akaweka magoti yake karibu na magoti yake (magoti ya Mtume ﷺ) na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake, kisha akasema; Ewe Muhammad! Niambie kuhusu Uislamu. Akasema (Mtume ﷺ): [Ni kushuhudia kwa kukiri kwa moyo na kushuhudia kwa ulimi kwamba hakuna Mola apasae Kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, kusimamisha Swala, kutoa Zaka, kufunga mwezi wa Ramadhani na kwenda kuhiji [Makkah] ukiweza] Akasema yule mtu: Umesema kweli. Tulipigwa na mshangao kwa kumuuliza kwake na kumsadikisha. Na akasema tena: Niambie kuhusu Imani. Akasema: [Ni kumwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu Vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, na kuamini Qadari kheri yake na shari yake] Akasema: Umesema kweli. Akasema: Hebu nielezee kuhusu Ihsaan. Akasema: [Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu kama vile unamuona na hata kama humuoni basi Yeye Anakuona]. Akasema: Niambie kuhusu Qiyama. Akajibu: [Hakuwa mwenye Kuulizwa ni Mjuzi zaidi kuliko aliye uliza] akasema basi Nijulishe alama zake: Akajibu: [Kijakazi atazaa bwana wake, na utaona waenda bila, wachungaji wenda uchi, wakishindana kujenga majumba ya fahari.]. Kisha akaondoka na nilitulia kidogo. Kisha Mtume ﷺ akasema: [Ewe ‘Umar! Je, mnamjua ni nani yule aliyekuwa akiuliza?] Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua zaidi. Akasema (Mtume ﷺ) : [Huyu ni Jibril, alikuja kuwafundisha Dini yenu]   [Imepokewa na Muslim]

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.