0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

DARAJA YA PILI: IMANI

الأصول الثلاثة


الْمَرْتَبَةُ الثَّانِيَةُ: الإِيمَانُ

وَهُوَ:

[بِضْعٌ وَسَبْعُونَ شُعْبَةً، فَأَعْلاهَا قَوْلُ لا إلٰه إِلا اللهُ، وَأَدْنَاهَا إِمَاطَةُ الأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ، وَالْحَيَاءُ شُعْبَةٌ مِنْ الإِيمَانِ]

وَأَرْكَانُهُ سِتَّةٌ كما فى الحديث:

أَنْ تُؤْمِنَ بِاللهِ، وَمَلائِكَتِهِ، وَكُتُبِهِ، وَرُسُلِهِ، وَالْيَوْمِ الآخِرِ، وَتُؤْمِنَ بِالْقَدَرِ خَيْرِهِ وَشَرِّهِ]    رواه مسلم]

وَالدَّلِيلُ عَلَى هَذِهِ الأَرْكَانِ السِّتَةِ قَوْلُهُ تَعَالَى:

لَّيْسَ الْبِرَّ أَن تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ}    البقرة:177}

ودليل القدر قَوْلُهُ تَعَالَى:

{إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ}   القمر:49}

Daraja Ya Pili: Imani

Nayo ni:

[Ina tanzu (matawi) Sabiini na kitu. Ya juu yake ni kauli ya “Laa ilaaha illa-Allaah” [hapana Muabudiwa wa haki ila Mwenyzi Mungu], na ya chini yake kabisa ni kuondosha uchafu njiani.Na kuona hayaa ni utanzu [tawi] katika tanzu za Imani]   (1)

Na nguzo zake ni sita kama ilivyo kuja katika Hadithi:

[Ni kumwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Mitume Wake na Siku ya Mwisho, na kuamini Qadari kheri yake na shari zake].  [Imepokewa na Muslim]

Na dalili ya hizi nguzo sita ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:

[Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Bali wema ni wa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii,]   [Al-Baqara:177]

Na dalili ya Al-Qadr (majaaliwa) ni kauli ya Mwenyezi Mungu ﷻ:

[Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo.]     [Al-Qamar:49]

1) Hii ni Hadithi iliopokewa na Muslim kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.