0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MLANGO WA 18 SABABU YA WANADAMU KUKUFURU, NA KUACHA DINI YAO NI KUVUKA MIPAKA KATIKA KUWATUKUZA WAJA WEMA

KITAAB AT-TAWHIID

باب ما جاء أن سبب كفر بني آدم وتركهم دينهم هو الغلو في الصالحين

وقول الله عز وجل: { يا أهل الكتاب لا تغلوا في دينكم}

وفي الصحيح عن ابن عباس رضي الله عنهما في قول الله تعالى: {وقالوا لا تذرُنَّ آلهتكم ولا تذرُنَّ ودا ولا سواعا ولا يغوث

ويعوق ونسرا} ، قال: [هذه أسماء رجال صالحين من قوم نوح، فلما هلكوا أوحى الشيطان إلى قومهم أن انصبوا إلى مجالسهم التي كانوا يجلسون فيها أنصابا وسموها بأسمائهم، ففعلوا، ولم تعبد، حتى إذا هلك أولئك ونسي العلم، عبدت]. وقال ابن القيم: قال غير واحد من السلف: لما ماتوا عكفوا على قبورهم ثم صوروا تماثيلهم، ثم طال عليهم الأمد فعبدوهم. وعن عمر أن رسول الله ﷺ قال: [ لا تطروني كما أطرت النصارى ابن مريم، إنما أنا عبد، فقولوا: عبدالله ورسوله] أخرجاه. وقال: قال رسول الله ﷺ: [ إياكم والغلو، فإنما أهلك من كان قبلكم الغلو]. ولمسلم عن ابن مسعود أن

رسول الله ﷺ قال: [ هلك المتنطعون] قالها ثلاثا.

فيه مسائل:

الأولى: أن من فهم هذا الباب وبابين بعده، تبين له غربة الإسلام، ورأى من قدرة الله وتقليبه للقلوب العجب

الثانية: معرفة أول شرك حدث على وجه الأرض أنه بشبهة الصالحين

الثالثة: أول شيء غيّر به دين الأنبياء، وما سبب ذلك مع معرفة أن الله أرسلهم

الرابعة: قبول البدع مع كون الشرائع والفطر تردها

الخامسة: أن سبب ذلك كله مزج الحق بالباطل، فالأول: محبة الصالحين، والثاني: فعل أناس من أهل العلم والدين شيئا أرادوا

به خيرا، فظن من بعدهم أنهم أرادوا به غيره

السادسة: تفسير الآية التي في سورة نوح

السابعة: جبلة الآدمي في كون الحق ينقص في قلبه، والباطل يزيد

الثامنة: فيه شاهد لما نقل عن السلف أن البدعة سبب الكفر

التاسعة: معرفة الشيطان بما تؤول إليه البدعة ولو حسن قصد الفاعل

العاشرة: معرفة القاعدة الكلية، وهي النهي عن الغلو، ومعرفة ما يؤول إليه

الحادية عشرة: مضرة العكوف على القبر لأجل عمل صالح

الثانية عشرة: معرفة النهي عن التماثيل، والحكمة في إزالتها

الثالثة عشرة: معرفة عظم شأن هذه القصة، وشدة الحاجة إليها مع الغفلة عنها

الرابعة عشرة: وهي أعجب وأعجب، قراءتهم إياها في كتب التفسير والحديث، ومعرفتهم بمعنى الكلام، وكون الله حال بينهم وبين

قلوبهم حتى اعتقدوا أن فعل قوم نوح هو أفضل العبادات، واعتقدوا أن ما نهى الله ورسوله عنه، فهو الكفر المبيح للدم والمال

الخامسة عشرة: التصريح أنهم لم يريدوا إلا الشفاعة

السادسة عشرة: ظنهم أن العلماء الذين صوروا الصور أرادوا ذلك

السابعة عشرة: البيان العظيم في قوله ﷺ: [لا تطروني كما أطرت النصارى ابن مريم] فصلوات الله

وسلامه على من بلغ البلاغ المبين

الثامنة عشرة: نصيحته إيانا بهلاك المتنطعين

التاسعة عشرة: التصريح بأنها لم تعبد حتى نسي العلم، ففيها بيان معرفة قدر وجوده ومضرة فقده. العشرون: أن سبب فقد العلم موت العلماء

MLANGO WA 18 SABABU YA WANADAMU KUKUFURU, NA KUACHA DINI YAO NI KUVUKA MIPAKA KATIKA KUWATUKUZA WAJA WEMA 

Ni neno  lake Mwenyezi Mungu ﷻ:

[Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu,]  [An-Nisaa: 171]

Na katika Sahihi ya (Bukhari) kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhi za Allah ziwe juu yake) Amesema kuhusu neno lake Mwenyezi Mungu: [Wakasema: “Msiwaache waabudiwa wenu; na wala msimwache Waddaa, na wala Su’waa’a, na wala Yaghuwtha, na Ya’uwqa, na Nasraa]  [Nuwh1: 23] Akasema: [Haya ni majina ya waja wema miongoni mwa kaumu ya Nuuh. Walipofariki Shetani aliwashawishi watu wawaweke kama Masanamu kuwaheshimu na wakawaweka katika mabaraza yao waliyokuwa wakikaa. Wakawaita majina yao hao waja wema waliofariki. Hapo mwanzoni hawakuwa wakiwaabudu, hadi watu hao walipofariki, na iliposahauliwa asili yake masanamu hayo yakaanza kuabudiwa]

Ibn Al-Qayyim (Mungu amrahamu) Amesema: “Aghlabu ya As-Salaf wamesema: “Baada ya kufariki (waja wema) wakawawekea mipaka makaburini mwao na wakaweka masanamu yao na baada ya muda kupita wakaanza kuyaabudu.”

Imepokelewa kutoka kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ Amesema: [Msinitukuze kama Manaswara walivyomtukuza mwana wa Maryam, hakika mimi ni mja kwa hiyo semeni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Na Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ Amesema: [Tahadharini na upindukiaji mipaka ya Dini, kwani waliokuwa kabla yenu waliangamia kwa sababu ya uvukaji mipaka ya Dini]    [ Imepokwa na Ahmad, An-Nasaaiy, Ibn Maajah, Ibn Khuzaymah, Al-Haakim na Adh-Dhahabiy kaiwafiki kuwa ni Swahiyh]

Na katika Sahihi Muslim Amepokea kutoka kwa Ibn Mas’uwd (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ Amesema: [Wameangamia wapindukiaji mipaka] Amesema mara tatu. [Muslim]

Masuala Muhimu Yaliyomo:

1. Yeyote anayeelewa mlango huu na milango miwili inayofuatia, atadhihirikiwa upekee wa Uislamu na atafahamu uwezo wa Mwenyezi Mungu wa kuzibadlisha nyoyo.

2. Kujua kuwa shirki ya kwanza kabisa ilyozuka duniani ilihusu waja wema (kudhania kuwa wana sifa na uwezo kama wa Mwenyezi Mungu).

3. Jambo la kwanza kubadilishwa katika dini ya Mtume na kilichosababisha hivyo, juu ya kujulikana kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye aliyewatuma.

4. Kutambua sababu ya kuikubali bid’ah licha ya kuwa ni kinyume na Shariy’ah (ya Dini) na maumbile.

5. Sababu ya yote haya ni kuchanganya haki na batili. Mwanzo ilikuwa kuwatukuza waja wema. La pili ni baadhi ya watu wa elimu walikuwa walikifanya kwa niah njema, lakini vizazi vilivyokuja baadaye walikusudia vinginevyo.

6. Tafsiri ya Ayah katika Suratun-Nuuh [71: 23]

7. Maumbile ya mwanadamu, haki hupungua moyoni mwake, na hapo upotofu huongezeka (isipokuwa ambaye Mwenyezi Mungu Amemteremshia rahmah Yake).

8. Inathibitisha kauli za Salaf kuwa bid’ah ni sababu ya kufuru, nayo inapendwa mno na Ibliys kuliko maasia, kwa sababu mtu hutubia maasi, ama bid’ah hatubii (kwa kuwa anadhania ni ‘amali njema).

9. Ufahamu wa shetani wa natija ya mwisho kuhusu bid’ah inavyopelekea (katika upotofu) hata kama niyyah ya mtu ilikuwa ni safi.

10. Kujifunza kanuni ya kijumla nayo ni kukatazwa kupindukia mipaka na kufahamu inapelekea wapi.

11. Madhara ya ziara ndefu makaburini hata ikiwa ni kwa niyyah ya kufanya ‘amali njema.

12. Kukatazwa masanamu na hekima ya kuyavunjulia mbali.

13. Kujua umuhimu wa kisa hiki, na kusisitiza kupata mafunzo yake na kutokughafilika nacho kwa kuwa ni jambo linalopuuzwa.

14. Ni ajabu kubwa, wanalisoma hilo katika vitabu vya Tafsiyr na Hadiyth, na wanaelewa maana yake, lakini juu ya hivyo, Mwenyezi Mungu Ameziwekea vikwazo nyoyo zao hadi wakaitakidi kuwa matendo ya kaumu Nuwh (kuwatukuza waja wema waliofariki na makaburi yao) ni aina bora ya ‘ibaadah na wakaamini Alivyovikataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake ﷺ ni kufru inayohalalisha damu na mali ya wakanushao.

15. Ufafanuzi kuwa wao kwa matendo yao walikusudia Shafaa’ah tu.

16. Waliamini kuwa wenye elimu waliochonga masanamu walikuwa na niah hiyo hiyo.

17. Ufafanuzi wa neno lake (Mtume ﷺ) : [Msinitukuze kama Manaswara walivyomtukuza mwana wa Maryam]. Mwenyezi Mungu Amshushie rahmah na amani kwa kubalighisha ujumbe wake waziwazi.

18. Onyo lake ((Mtume ﷺ) kwetu kwamba kupindukia mipaka ya Dini inapeleka katika maangamizi.

19. Maelezo kwamba masanamu hayakuabudiwa isipokuwa baada ya elimu ya asili yake kupotea. Hii inatambulisha thamani ya Elimu ya historia na madhara ya kukosekana kwake.

20. Sababu ya kupotea Elimu ni kufariki kwa Wanachuoni.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.