0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MLANGO WA 17 NENO LAKE MWENYEZI MUNGU [KWA HAKIKA WEWE HUMWONGOI UMPENDAE]


KITAAB AT-TAWHIID


باب 17 قول الله تعالى : {إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ

:قَوْلُ اَللَّهِ تَعَالَى

{إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ }

وَفِي اَلصَّحِيحِ، عَنْ اِبْنِ الْمُسَيَّبِ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: لَمَّا حَضَرَتْ أَبَا طَالِبٍ الْوَفَاةُ; جَاءَهُ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) وَعِنْدَهُ عَبْدُ اَللَّهِ بْنُ أَبِي أُمِّيَّةَ وَأَبُو جَهْلٍ فَقَالَ لَهُ: [يَا عَمِّ قُلْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ كَلِمَةً أُحَاجُّ لَكَ بِهَا عِنْدَ اَللَّهِ] فَقَالاَ لَهُ: أَتَرْغَبُ عَنْ مِلَّةِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ؟ فَأَعَادَ عَلَيْهِ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَأَعَادَا، فَكَانَ آخَرَ مَا قَالَ: هُوَ عَلَى مِلَّةِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، وَأَبَى أَنْ يَقُولَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ فَقَالَ اَلنَّبِيُّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((لأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ مَا لَمْ أُنْهَ عَنْكَ)). فَأَنْزَلَ اَللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: {مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ} وَأَنْزَلَ اَللَّهُ فِي أَبِي طَالِبٍ: {إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ


MLANGO WA 17 NENO LAKE MWENYEZI MUNGU [KWA HAKIKA WEWE HUMWONGOI UMPENDAE]

Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na Yeye ndiye anawajua zaidi waongokao]  [Al-Qasas: 56]

Katika Sahihi (Al Bukhari), kutoka kwa Ibn Musayyib amehadithia kutoka kwa baba yake: Mauti yalipomkaribia Abuu Twaalib, Mtume  wa Mwenyezi Mungu ﷺ alimwendea akamkuta ‘Abdullaah bin Abiy Umayyah na Abuu Jahl wakiwa pamoja naye. Mungu ﷺ akamwambia: [Ewe ‘ammi yangu! Sema laa ilaaha illa-Allaah, hivyo utaniwezesha kukuombea shafaa (uombezi) mbele ya Mwenyezi Mungu] Wawili hao wakamwambia: Utaacha dini ya [baba yako] ‘Abdul-Muttwalib?  Mtume wa Mungu ﷺ akakariri na wawili hao wakakariri nao vile vile. Ikawa neno la mwisho alosema ni kubakika katika dini ya ‘Abdul-Muttwalib. Akafariki akiwa amekataa kusema ‘Laa ilaaha illa-Allaah’. Mtume ﷺ akasema: [Nitaendelea kukuombea maghfirah madamu sijakatazwa kufanya hivyo]. Hapo Mwenyezi Mungu ﷻ Akateremsha Aya hii: [Haimpasii Nabii na wale walio amini kuwatakia msamaha washirikina, ijapo kuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni.] [At-Tawba: 113] Kisha Akateremsha kuhusu Abuu Twaalib: [Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na Yeye ndiye anawajua zaidi waongokao]  [Al-Qaswas: 56]

Masuala Muhimu Yaliyomo:

  1. Tafsiri ya Ayahkatika Suwrah Al-Qaswas: 56

[Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na Yeye ndiye anawajua zaidi waongokao]

2. Tafsiri ya Aya:

[Haimpasii Nabii na wale walio amini kuwatakia msamaha washirikina, ijapo kuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni.]  [At-Tawbah113].

3. Suala kubwa la tafsiri ya kauli yake Mtume ﷺ: [Sema, Laa ilaaha illaa Allaah] Inakinzana na madai ya wanodai kuwa wana ujuzi wa elimu ya Dini (kudai kwao kwamba kuitamka kwake inatosheleza kusamehewa juu ya kwamba wanawaomba na kuwaabudu mawalii wao).

4. Abuu Jahl na wenzake walijua kusudio la Mtume ﷺ alipomwambia Abuu Twaalib: [Sema ‘Laa ilaaha illaa Allaah)), Basi Mwenyezi Mungu ﷻ Amdhalilishe yeyote ambaye elimu yake juu ya asili ya Uislamu ni ndogo kuliko ile ya Abuu Jahl.

5. Hima ya Mtume ﷺ kutaka kumsilimisha ‘ammi yake.

6. Kukanushwa yeyote anayedai kuwa ‘Abdul-Muttwalib na baba zake walikuwa Waislamu.

7. Mtume ﷺ alimwombea ‘Ammi yake msamaha lakini hakusamehewa, na kuwa hilo limekatazwa.

8. Madhara ya kuandamana na waovu.

9. Madhara ya kuwatukuza kibubusa viongozi na wahenga (na hali ni washirikina).

10. Shubuha za wapotofu katika hilo ni hoja za ujaahiliyyah (kama Abuu Jahl alivyojitokeza).

11. Dalili kwamba ‘amali za mmja zinategemea mwisho wake, kwa sababu kama angeitamka laa ilaaha illa-Allaah, angeliokoka.

12. Zingatio la hoja hii ya mwisho katika nyoyo za wapotofu kujivunia dini na mila za mababu, kwa sababu kisa kinathibitisha kwamba hawakujadiliana naye isipokuwa kuhusu kuing’ang’ania dini au mila zao, japokuwa Mtume ﷺ aliendelea kumbembeleza Abuu Twaalib atamke shahaada, kwani angelishuhudia angeliokoka, lakini wao wakashikilia tu umuhimu wa kufuata dini ya wazazi wao.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.