0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MLANGO WA 12 NI KATIKA USHIRIKINA KUOMBA KINGA KWA ASIYEKUWA MWENYEZI MUNGU

KITAAB AT-TAWHIID

باب (12) من الشرك: الاستعاذة بغير الله

وقول الله تعالى: {وَأَنَّهُ كَانَ رِجَالٌ مِنَ الْأِنْسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِنَ الْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقاً} سورة الجن: 6

وعن خولة بنت حكيم قالت: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: [من نزل منْزلا فقال: أعوذ بكلمات الله التامات من شر ما خلق، لم يضره شيء حتى يرحل من منْزله ذلك]     رواه مسلم
فيه مسائل:
الأولي: تفسير آية الجن
الثانية: كونه من الشرك
الثالثة: الاستدلال على ذلك بالحديث، لأن العلماء يستدلون به على أن كلمات الله غير مخلوقة. قالوا: لأن الاستعاذة بالمخلوق شرك
الرابعة: فضيلة هذا الدعاء مع اختصاره
الخامسة: أن كون الشيء يحصل به منفعة دنيوية، من كف شر أو جلب نفع، لا يدل على أنه ليس من الشرك


MLANGO WA 12 NI KATIKA USHIRIKINA KUOMBA KINGA KWA ASIYEKUWA MWENYEZI MUNGU ﷻ

Na kauli ya Mwenyezi Mungu ﷻ:

[Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi.]  [Surat Al-Jinn: 6]

Imepokelewa kutoka kwa Khawlah bint Hakiym (Radhi za Allah ziwe juu yake) Amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akisema: [Atakayefikia mahali kisha akasema: A’uwdhu bikalimati-LLaahit-taammati min sharri maa Khalaq’ “Najilinda kwa maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyotimia na shari ya Alichokiumba” hakuna kitakachomdhuru hadi atakapoondoka mahali pake hapo]    [Imepokewa naMuslim]

Masuala Muhimu Yaliyomo:

1. Tafsiri ya Aya katika Suwratul-Jinn.

2. Kuwa Kuomba ulinzi kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ﷻ ni shirki.

3. Kutolea ushuhuda juu ya hilo kwa Hadithi, kwa sababu Wanachuoni wanathibitisha kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu (yaani Qur’aan) kwa sababu kujikinga na Viumbe ni shirki.

4. Fadhila ya Du’a hii japokuwa ni fupi.

5. Kupata Manufaa ya kiduna Juu ya kitu, kama kuzuia Madhara au kupata Manufaa, hilo Halimanishi kuwa jamabo hilo si shirki.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.