0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MLANGO WA 11 KUWEKA NADHIRI KWA ASIYEKUWA MWENYEZI MUNGU NI SHIRKI

KITAAB AT-TAWHIID

باب (11) من الشرك: النذر لغير الله
وقول الله تعالى: {يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْماً كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيراً}   الإنسان:7

وقوله: {وَمَا أَنْفَقْتُمْ مِنْ نَفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُمْ مِنْ نَذْرٍ فَإِنَّ اللَّهَ يَعْلَمُهُ}    البقرة:270
وفي الصحيح عن عائشة رضي الله عنها: أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: [من نذر أن يطيع الله فليطعه ; ومن نذر أن يعصي الله فلا يعصه]      رواه البخاري
فيه مسائل:
الأولي: وجوب الوفاء بالنذر
الثانية: إذا ثبت كونه عبادة الله، فصرفه إلى غيره شرك
الثالثة: أن نذر المعصية لا يجوز الوفاء به

MLANGO WA 11 KUWEKA NADHIRI KWA ASIYEKUWA MWENYEZI MUNGU NI SHIRKI

Na kauli ya Mwenyezi Mungu ﷻ:

[Wanatimiza ahadi,na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana,]  [Al-Insaan: 7]

Na kauli Yake ﷻ :

[Na chochote mnacho toa au nadhiri mnazo weka basi hakika Mwenyezi Mungu anajua.]    [Al-Baqarah: 270]

Na katika Asw-Swahihi: Imepokelewa kutoka kwa ‘Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba Mtume ﷺ amesema: [Atakayeweka nadhiri kumtii Mwenyezi Mungu na amtii. Na atakayeweka nadhiri kumuasi Mwenyezi Mungu basi asimuasi]    [Imepokewa na Bukhari]

Masuala Muhimu Yaliyomo:

1. Uwajibu wa kutekeleza nadhiri.

2. Ikiwa imethibitika kuwa nadhiri Ibada ya Mwenyezi Mungu ﷻ, basi kumfanyia mwengine ni shirki.

3. Kwamba nadhiri ya masia haifai kutekeleza.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.