0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MIONGONI MWA HUKUMU ZA KUMFUATA IMAMU

SOMO LA FIQHI

MIONGONI MWA HUKUMU ZA KUMFUATA IMAMU

1. Haisihi kwa mtu aliye nyumbani kwake kumfuata imamu kupitia kusikia sauti yake kwa kipaza sauti au kupitia kusikiliza redio.

2. Inafaa kumfuata imamu kutoka nje ya msikiti iwapo safu zimeungana.

3. Inasihi kwa maamuma kumfuata imamu hata kama wako juu ya sakafu ya msikiti au wakawa chini ya imamu iwapo wanasikia sauti yake.

4. Inafaa kwa mwenye kuswali faradhi kumfuata mwenye kuswali sunna au kinyume chake, mfano wa mwenye kuswali swala ya Isha nyuma ya mwenye kuswali Tarawehe, au kuswali pamoja na aliyepitwa na Swala ili apate thawabu ya Swala ya jamaa. Jabir bin Abdillah Radhi za Allah ziwe juu yake  amepokewa akisema kwamba “Mu’aadh alikuwa akiswali pamoja na Mtume ﷺ kisha akiwajia watu wake akiwaswalisha” [Imepokewa na Bukhari.].

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.