SOMO LA FIQHI
1. HUKMU YA UVINDU NA UMANJANO
Mwanamke akiona damu ya manjano au iliyochanganyika baina ya umanjano na weusi, au akaona umajimaji tu, huwa ni moja ya hali mbili:
A). Ima aione wakati wa hedhi au imeungana na hedhi kabla ya utwahara:
Katika hali hii itapewa hukumu ya hedhi, kwa hadithi ya Aishah Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba wanawake walikuwa wakimtumia kibakuli ambacho ndani yake kuna pamba yenye dowa rangi ya manjano, na yeye akiwambia:
[انتظرن لا تعجلن حتى ترين القصة البيضاء]
[Ngojeni musifanye haraka mpaka muone paku leupe] akikusudia kwa hilo ndio kutwahirika na hedhi
B). Ima aione wakati wa twahara:
Katika hali hii huwa haizingatiwi kuwa ni kitu chochote, na haimpasi udhu wala kuoga, kwa hadithi ya Ummu Atiyyah kwamba alisema:
[كُنَّا لا نَعُدُّ الْكُدْرَةَ وَالصُّفْرَةَ بَعْدَ الطُّهْرِ شَيْئًا]
[Hatukuwa tukiizingatia damu iliyochafuka au iliyo manjano baada ya kujitwahirisha kuwa ni chochote] [Imepokewa na Abu Daud.].
2. HUKMU YA KUKATIKA KATIKA KWA HEDHI:
Mwanamke aonapo damu siku moja na kukatika siku moja na mfano wake, basi yeye ni mojawapo wa hali mbili
1. Hali hiyo iendelee na yeye kila wakati:
Basi hiyo ni damu ya istihadhah
2. Iwe yakatikakatika:
Kwa namna ya kwamba ikawa yamjia wakati mwingine na atwahirika wakati mwingine. Basi hukumu yake ni kama ifuatayo:
a. Kukatika damu kukipungua kwa siku moja, basi kipindi hiko kitahesabiwa kuwa ni katika kipindi cha hedhi.
b. Na akioona katika kipindi cha utwahara dalili za damu, kama kuona paku leupe, basi kipindi hiki ni cha utwahara, liwe ni dogo au kubwa, au liwe chini ya siku moja au zaidi.