0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MATESO YALIYO WAKUMBA BAADHI YA MASWAHABA BAADA YA KUSILIMU KWAO

AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Tuangalie hali yao kwa undani zaidi. Abu Jahl aliposikia kusilimu kwa mtu mkubwa mwenye marafiki wenye nguvu, alitoa kashfa na kukebehi uwezo wake wa akili, kubeza maamuzi yake na kumpa vitisho vya kuogofya, endapo alikuwa mfanya biashara. lkiwa aliyesilimu alikuwa mtu wa chini katika jamii, humpiga sana na kumpa mateso yasiyoelezeka.?

Ammi yake ‘Uthman bin ‘Affan alikuwa akimviringishia ‘Utnman mkeka uliosukwa kwa majani ya mtende na kuwasha moto chini yake. (1)

Umrn Mus’ab bin ‘Umair aliposikia mwanawe amesilimu, alimnyima chakula na akamfukuza nyumbani kwake. Kabla ya kusilimu aliishi maisha ya starehe lakini baada ya kuteswa, ngozi yake ilisinyaa na wajihi wake ulibadilika kwa makovu. 

Bilal, mtumwa wa Umayyah bin Khalaf, alipigwa sana na bwana wake baada ya kufahamika kuwa aliingia katika Uislamu. Baadhi ya nyakati alifungwa shingoni kwa kamba na watoto mtaani waliambiwa wamburure katika mitaa, na wakati mwingine juu ya vilima vya Makka. Wakati mwingine alinyimwa chakula na maji kwa kipindi kirefu, pia alifungwa na kulazwa juu ya mchanga wenye joto la jua na kubebeshwa mawe mazito. Alifanyiwa mateso ya aina mbalimbali ili arejee kwenye ukafiri. Yote hayo hayakufua dafu kwani aliendelea na Imani ya Mungu Mmoja. Siku moja Abubakar (r.a) atipita na kumwona akiteswa, alimnunua na kumkomboa kutoka kwenye utumwa. (2)

Muathirika mwingine wa mateso ya Makuraishi alikuwa Ammar bin Yasir aliyeachwa huru na Bani Makhzum, Yeye pamoja na mama na baba yake walisilimu siku za mwanzo za Uislamu, Waliteswa kwa kulazimishwa kulala juu ya mchanga wenye joto na walipigwa sana, ‘Ammar aligaragazwa juu ya makaa ya moto. Mtume alihuzunishwa sana na yale yaliyowasibu, Ammar na familia yake. Wakati wote aliwaliwaza na aliwaombea dua na kusema; 

[صبراً آل ياسر فإن موعدكم الجنة]

[Yuieni subira familia ya Yassir, bila shaka makazi yenu yatakuwa Peponi.]

Yasir alikufa kutokana na mateso. Mama yake ‘Ammar, Bi Sumayyah, alichomwa kwa kisu na Abu Jahl, mpaka akafa.Mama huyu ndiye aliyekuwa shahidi wa kwanza mwanamke katika Uislamu.  

Ammar alikabiliwa na aina tofauti ya mateso na alitishiwa kuendelea kuteswa kama asingemkashifu Muhammad (s.a.w) na kurejea kwa Al-Lata na Uzza. Kuna wakati alizidiwa na machungu akatamka nene la kurejea kwenye ushirikina japo moyo wake haukutetereka. Alikwenda kwa Mtume  ambaye alimliwaza kwa maumivu aliyoyapata na kuithibitisha Imani yake. Baadaye kidogo aya ifuatayo illteremshwa:

مَن كَفَرَ بِاللَّهِ مِن بَعْدِ إِيمَانِهِ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ وَلَٰكِن مَّن شَرَحَ بِالْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِّنَ اللَّهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ

[Anaye mkataa Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake – isipo kuwa aliye lazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya Imani ]   [16:106]  (3)

Abu Fakih (Aflah) aliyeachwa huru na Bani Abd-Dar alikuwa mhanga wa tatu. Wakandamizaji walikuwa wakimfunga miguu kwa kamba na kumbururaiw katika mitaa ya Makka.

Khabbab bin Al-Arrat ni mhanga mwingme aliyefanyiwa vitendo vya kikatili. Aliteswa sana, kuonewa na kudhulumiwa. Mushirikina wa Makka walikuwa wakimvuta nywele na kuizungusha shingo yake na kumlazimisha kulala juu ya makaa ya moto, huku jiwe kubwa likiwekwa juu yake ill asiweze kusimama.

Baadhi ya Waislamu wenye vyeo na hadhi waliviringishwa kwenye ngozi mbichi ya ngamia na kutupwa kwenye jangwa, wakati wengine waliwekwa juu ya mchanga uliokuwa ukiungua kwa jua kali la Arabia. 

Wanawake waliosilimu hawakusalimika, kwani nao waliteswa. Orodha yao ni ndefu hapa tutawataja baadhi yao tu: Zanirah, An-Nahdiyah na Binti yake, na Umm ‘Ubais hawa ni wajakazi waliosilimu. Akasilimu mjakazi mwengine wa Bani Ma’mal (katika Banu Adiy) naye aliteswa sana na Umar bin Al-Khattab, kabla ya kusilimu kwake. Umar akichoka kumtesa alikuwa akisema, “Nakuacha kukupiga kwa sababu tu nimechoka.” (4)

Abubakar (r.a) muumini tajirl, aliwanunua na kuwaacha huru watumwa wa kike kama alivyowafanyia Bilal na Amin bin Fuherah.

Washirikina wa Makka walikuwa wakiwafunga masahaba nyuma ya ngamia na ng’ ombe, kisha kuwaburuza jangwani katika mchanga wa joto kali. Wengine wakiwavalisha Deraya kisha kuwatupa jangwani kwenye joto kali.(5)


1) Rahmatun Li! ‘Alamin, Juzuu 1, Uk. 57.

2) Rahmatun Lil ‘Alamin, Juzuu 1, Uk. 57. Talqiyh Fuhum Ahlul AtIuu, Uk. 61.

3) lbn HisJuzm, Juzuu 1, Uk. 319-320. Muhammad al-Ghazali, Fiqhi SiTa, Uk. 

82. MulhtsIsar Sim, Uk. 92.

4) Rahmatun Lil ‘Alamin, Juzuu 1, Uk. 57. 100 Hisham, [uzuu 1, Uk. 319

5) 168 Rahmatun Lil ‘Alamin, juzuu 1, Uk, 58


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.