0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

KUTUMIA MBINU ZA MATESO

AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Mushrikina walitumia mbinu mbalimbali ambazo tumezitaja kwa lengo la kutaka kuuzuia wito wa Mtume  baada ya kudhihiri kwake, mwanzoni mwa mwaka wa nne wa Utume. Waliendelea na harakati zao hizo majuma na miezi na hali ya kuwa wamebaki na mbinu hizo tu, hawana uwezo wa kubuni nyingine. Waliendelea kushikilia njia za ukandamizaji na kuadhibu. Walipoona kuwa mbinu hizi haziwaletei manufaa yoyote katika kuuzuia wito wa Kiislamu, walikutana tena kwa mara nyingine; safari hii wakaunda kamati, iliyokuwa na wajumbe ishirini na watano (25), miongoni mwa mabwana wa Kikuraishi. Kiongozi wao alikuwa Abu Lahab ammi ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu  . Kamati ikaamua kuwa juhudi za kuupinga Uislamu ziongezwe, waendelee kumuudhi Mtume na kuwaadhibu wote watakaomfuata na kuingia katika Dini yake, na kuwatayarishia kila aina ya mateso na maumivu. Wakaazimia kuyatekeleza hayo dhidi ya Waislamu, hasa wale waliokuwa wanyonge miongoni mwao, maana hilo ilikuwa jambo jepesi kwao. 

Ama kwa upande wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu  mambo yalikuwa tofauti kabisa, kwani alikuwa ni mwenye haki yenye busara na utukufu, mwenye shakhsia ya kipekee, marafiki na maadui wote walikuwa wakimuheshimu sana, kwa sifa ya kuwa haitabiriwi mfano wa shakhsia hiyo isipokuwa kwa heshima na utukufu, na hakuna aliyethubutu kumfanyia mambo yaliyoduni na maovu isipokuwa aliyekuwa duni miongoni mwa watu na mjinga wao. Pamoja na ukweli huu, pia alikuwa katika dhamana ya Abu Twalib, na Abu Twalib alikuwa ni mmoja kati ya watu wachache wa Makka mwenye kuheshimiwa sana miongoni mwa watu na kutukuzwa. Hakukuwa na mtu aliyeweza kuthubutu kufanya ujasiri wa kuvunja dhamana au himaya yake. Kwa hakika hali hii iliwakera mno Makuraishi, iliwafanya wasimame na wakae Subira iliwashinda. Wakazidisha uadui dhidi ya Mtume wakiongozwa na Abu Lahab. Kwani Abu Lahab alikuwa ameutangaza msimamo wake huu dhidi ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kuanzia siku ya kwanza hata kabla Makuraishi hawajakusudia kufanya hivyo. Tumekwisha taja baadhi ya mambo ambayo aliwahi kumfanyia Mtume, katika baraza la Banu Hashim, na lile ambalo alilifanya katika mlima wa Swafaa. wakiwaza, mpaka lini wataendelea kuwa na subira hii ndefn, mbele ya Da’wa ambayo ilikuwa inaumaliza ukubwa wao wa kidini na uongozi wao wa kidunia? *


* Arraheeq Al Makhtum Uk. 145


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.