0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MASUALA MANNE AMBAYO NI LAZIMA KILA MUISLAMU AYAJUE

الأصول الثلاثة


بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمًنِ الرَّحيم

اعْلمْ رَحِمَكَ اللهُ أَنَّهُ يَجِبُ عَلَيْنَا تَعَلُّمُ أَرْبَع مَسَائِلَ

المسألة الأُولَى: الْعِلْمُ

وَهُوَ مَعْرِفَةُ اللهِ، وَمَعْرِفَةُ نَبِيِّهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وآله وَسَلَّمَ) وَمَعْرِفَةُ دِينِ الإِسْلامِ بالأَدِلَّةِ

المسألة الثَّانِيَة :الْعَمَلُ بِهِ

المسألة الثَّالِثَةُ :الدَّعْوَةُ إِلَيْهِ

المسألة الرَّابِعَةُ :الصَّبْرُ عَلَى الأَذَى فِيهِ

وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّ‌حْمَـٰنِ الرَّ‌حِيمِ

{وَالْعَصْرِ‌ إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ‌ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ‌}

قَالَ الشَّافِعيُّ (رَحِمَهُ اللهُ): لَوْ مَا أَنْزَلَ اللهُ حُجَّةً عَلَى خَلْقِهِ إِلا هَذِهِ السُّورَةَ لَكَفَتْهُمْ

وَقَالَ البُخَارِيُّ رَحِمَهُ اللهُ: بَابُ: العِلْمُ قَبْلَ القَوْلِ وَالْعَمَلِ

وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى

{فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ وَاسْتَغْفِرْ‌ لِذَنبِكَ}

فَبَدَأَ بِالْعِلْمِ قَبْلَ القَوْلِ وَالعَمَلِ

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

Jua, Mwenyezi Mungu Akurehemu, kwamba ni wajibu wetu kujua mas-alah manne:

Suala la kwanza: Elimu:

Nayo ni elimu ya kumjua Mwenyezi Mungu, na kumjua Mtume Wake ﷺ na elimu ya kuijua Dini ya Kiislamu kwa dalili zake.

Suala la pili:  Kuifanyia kazi.

Suala la tatu: Kuilingania.

Suala la nne: Kuwa na subira katika maudhi yatakayopatikana ndani yake.

Na dalili ni neno lake Mwenyezi Mungu ﷻ :

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

[Naapa kwa Zama!Hakika binaadamu bila ya shaka yumo katika khasara,Ila wale walio amini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri.]

Amesema Imaam Ash-Shaafi’iy (Mungu amrahamu): “Lau kama Mwenyezi Mungu Asingeliteremsha hoja kwa viumbe Vyake isipokuwa Suwrah hii, basi ingeliwatosheleza.”

Na Al-Bukhari (Mungu amrahamu) amesema katika Baabul-’Ilm qablal-qawli wal-‘amal “Mlango wa elimu kabla ya kauli na ‘amali”.

Na dalili ni kauli Yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi zako]  [Muhammad:19]

Akaanza kwa elimu kwanza kabla ya kauli na ‘amali.

SIKILIZA SHEREHE YA MADA HII NA SHEIKH SHADDAD ALI

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.