0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MASUALA MATATU AMBAYO NILAZIMA KWA KILA MUISLAMU KUJIFUNZA NA KUYAFANYIA KAZI

الأصول الثلاثة

اعْلَمْ رَحِمَكَ اللهُ أَنَّه يَجِبُ عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ وَمُسْلِمَةٍ، تَعَلُّمُ هَذِهِ الثَّلاثِ مَسَائِل، والْعَمَلُ بِهِنّ

الأُولَى: أَنَّ اللهَ خَلَقَنَا، وَرَزَقَنَا، وَلَمْ يَتْرُكْنَا هَمَلا، بَلْ أَرْسَلَ إِلَيْنَا رَسُولاً، فَمَنْ أَطَاعَهُ دَخَلَ الجَنَّةَ، وَمَنْ عَصَاهُ دَخَلَ النَّارَ

:وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى

{إِنَّا أَرْ‌سَلْنَا إِلَيْكُمْ رَ‌سُولًا شَاهِدًا عَلَيْكُمْ كَمَا أَرْ‌سَلْنَا إِلَىٰ فِرْ‌عَوْنَ رَ‌سُولًا فَعَصَىٰ فِرْ‌عَوْنُ الرَّ‌سُولَ فَأَخَذْنَاهُ أَخْذًا وَبِيلًا}

الثَّانِيَةُ: أَنَّ الله لا يَرْضَى أَنْ يُشْرَكَ مَعَهُ أَحَدُ فِي عِبَادَتِهِ، لا مَلَكٌ مُقَرَّبٌ، وَلا نَبِيٌّ مُرْسَلٌ

:وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى

{وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّهِ أَحَدًا}

الثَّالِثَةُ ُ:  أَنَّ مَنْ أَطَاعَ الرَّسُولَ، وَوَحَّدَ اللهَ لا يَجُوزُ لَهُ مُوَالاةُ مَنْ حَادَّ اللهَ وَرَسُولَهُ، وَلَوْ كَانَ أَقْرَبَ قَرِيبٍ

:وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ ۖ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ رَضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ أُولَـٰئِكَ حِزْبُ اللَّـهِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ


Jua Mwenyezi Mungu Akurehemu, kwamba ni wajibu kwa kila Muislamu mwanamume na Muislamu mwanamke, kujifunza mas-alah haya matatu na kuyafanyia kazi:

La kwanza: Ya kwamba Mwenyezi Mungu Ametuumba, na Anaturuzuku, na Hakutuacha bure bali Ametutumia Mtume. Basi atakayemtii ataingia Peponi, na atakayemuasi ataingia motoni.

Na dalili ni neno lake Mwenyezi Mungu :

[Hakika Sisi tumemtuma kwenu Mtume aliye shahidi juu yenu, kama tuliLakini Firauni alimuasi huyo Mtume, basi tukamshika mshiko wa mateso.vyo mtuma Mtume kwa Firauni]   [Surat Al-Muzzammil: 15-16]

La pili: Kwamba Mwenyezi Mungu Haridhii kushirikishwa pamoja Naye yeyote yule katika ‘ibaadah Yake, hata ikiwa ni Malaika aliyekurubishwa, wala Nabiy aliyetumwa.

Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu

[Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu]   [Surat Al-Jinn: 18]

La Tatu: Kwamba Atakayemtii Mtume, na Akampwekesha Mwenyezi Mungu, haifai kwake kufanya urafiki na ushirikiano na yule anayempiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake hata akiwa ni jamaa wa karibu.

Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

[Huwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao ameandika katika nyoyo zao Imani, na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake. Na atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Humo watakaa daima. Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na wao wawe radhi naye. Hao ndio Hizbullahi, Kundi la Mwenyezi Mungu. Hakika Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufanikiwa]   [Suuratul Al Mujaadalah:22]

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.