0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAMBO YANAYOHARIBU SAUMU

MAMBO YANAYOHARIBU SAUMU

1. Kula na kunywa kwa kukusudia ndani ya mchana wa Ramadhani
Kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّى يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ}    البقرة:187

[Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni saumu mpaka usiku]    [Al-Baqarah – Aya 187]

MAS’ALA 

Je yafaa mtu kula kwasababu ya kazi?
Yoyote anayefanya kazi mahali pa mapishi ya mikate hivi na mahali pa kazi ngumungumu sio ruhusa kwao kutofunga (yaani hawafai kula mchana wa Ramadhani); kwasababu wamelazimika kama watu wengine kufunga Ramadhani.

MAELEZO 

Atakaye kula au kunywa kwa kusahau basi saumu yake imeswihi (iko sawa haina tatizo lolote), na inamlazimu kujizuia na vitu vinavyoharibu saumu pindi anapokumbuka; kwa kauli ya Mtume ﷺ:

[من نسي  وهو صائم – فأكل أو شرب فليتمّ صومه ، فإنما أطعمه الله وسقاه]     رواه مسلم

[Aliyesahau hali ya kuwa amefunga akala na kunywa, basi akamilishe saumu yake, kwani Mwenyezi Mungu amemlisha na kumnywesha (mtu huyo)]     [Imwpokewa na Muslim.].

– Kinaharibu saumu chochote kile kinachoingia tumboni kwa njia ya mdomoni au puani, na chochote kinachofahamika kuwa chakula au kinywaji, kama vile sindano za lishe/chakula. Ama sindano ambazo si za chakula, kama penicillin na mfano wake, hazifunguzi saumu, kwasababu sio chakula wala kinywaji, wala sio kwa maana ya chakula.

– Chochote kinachoingizwa mdomoni kwa ajili ya kutizama kitu na vipuliza hewa vya kutibu pumu na mfano kama huu, hakiharibu saumu.

– Wanja, na matone ya kitu majimaji kutonezwa kwenye jicho na sikio na mfano wa hivi viwili havivunji saumu, kwasababu hakuna dalili ya vitu hivi kuharibu saumu, na kwasababu jicho sio sehemu inayotegemewa kwa kuingilia chakula na kinywaji, na vile vile matone ya kitu majimaji kwenye sikio na puani, lakini ubora kwa haya matone ni kujitenga nayo, kwa jinsi alivyokataza Mtume ﷺ kuhusu kupita mpaka katika kupandisha maji puani kwa aliyefunga, [Imwpokewa na Tirmidhi.] na kwasababu ni sehemu inayopitisha chakula hadi tumboni.

– Anapotumia mtu kitu ambacho hakiliwi au kinadhuru, kama vile sigara basi atakuwa amefungua, kwasababu amekitumia kupitia sehemu inayotumika kwa chakula, nayo ni mdomo, kama nayo itakavyofahamika kuwa chakula ama kinywaji.

– Hakiharibu saumu kitu ambacho kwamba huwezi kukiepuka, kama vile vumbi la njiani, na mabaki ya chakula yaliosalia kati ya meno.

Dawa inayotumika kama chakula inaharibu saumu.Sindano ya penicillin haiharibu saumu.(Hii ni sindano ya kukinga au kutibu madhara yanayosababishwa na bacteria).Vipuliza hewa vya kutibu pumu haviharibu saumu.Wanja haiharibu saumu.Sigara zinaharibu saumu.Mabaki ya chakula yaani katika meno hayaharibu saumu.

2. Kufanya Tendo la Ndoa
Kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ}    البقرة:187

[Mmehalalishiwa usiku wa saumu kuingiliana na wake zenu]   [Al-Baqarah – Aya 187].

Na “Ar-Rafath” ni neno la kiarabu lililotumika katika Aya hii kumaanisha kuingiliana – yaani kufanya tendo la ndoa, basi yoyote atakaye ingiliana na mkewe au mumewe hali ya kuwa amefunga, saumu yake itakuwa imeharibika, na atalazimika ailipe siku hiyo, na pamoja na kuilipa ni juu yake kutoa kafara nzito, nayo ni kuacha huru mtumwa, akiwa hatopata mtumwa wa kumuacha huru, atalazimika kufunga miezi miwili mfululizo, na akiwa hawezi kufunga atalazimika kulisha masikini sitini, kama ilivyothibiti kutoka kwa Abu Hurerah radhi za Allah ziwe juu yake Anasema:

جاء رجل إلى النبي صلى الله عليه وسلم فقال: هلكت، قال: وما شأنك، قال: وقعت على امرأتي في رمضان، فقال: هل تجد ما تعتق رقبة. قال: لا، قال: فهل تستطيع أن تصوم شهرين متتابعين، قال: لا، قال: فهل تستطيع أن تطعم ستين مسكيناً، قال: لا أجد، فأتى النبي صلى الله عليه وسلم بعرق فيه تمر، فقال: خذ هذا فتصدق به، فقال: أعلى أفقر منا؟ ما بين لابتيها أفقر منا، ثم قال: خذه فأطعمه أهلك.      رواه البخاري ومسلم

[Alikuja mtu mmoja kwa Mtume ﷺ akasema nimeangamia. Mtume akamuuliza: Una nini? Akajibu: Nimemuingilia mkewangu ndani ya Ramadhani. Mtume akamuuliza: Waweza kuacha mtumwa huru?. Akajibu: Siwezi.. Mtume akamuuliza: je waweza kufunga miezi miwli mfululizo? Akasema: Siwezi. Mtume akamuuliza: Basi waweza kulisha masikini sitini?. Akasema: Siwezi. Mtume akamwambia: Kaa. Akakaa. Mtume ﷺ akaleta chombo ambacho ndani yake mna tende. Akasema: Chukua (hiki chombo) wende ukatolee sadaka. Akasema yule mtu: Je kuna fakiri zaidi yetu? (yaani maskini kuliko familia yake). Mtume akacheka mpaka yakaonekana magego ya meno yake, akasema: Lisha familia yako ( hizo tende)]    [Imwpokewa na Bukharin a Muslim.].

MAELEZO 

Na inakuwa kafara inafuata mfumo huu, hivyo basi mtu asilishe maskini isipokuwa akiwa hawezi kufunga hiyo miezi miwili mfululizo, wala asifunge isipokuwa ikiwa hawezi kuacha huru mtumwa.

JE MWANAMKE ANALAZIMIKA KUTOA KAFARA?

Na inamlazimu mwanamke kutoa kafara ikiwa ameridhiana na mumewe kufanya tendo la ndoa, na iwapo amelazimishwa na mumewe kuingiliana basi saumu yake imeharibika na itamlazimu mwanamke huyo kuilipa saumu hiyo peke yake bila ya kutoa kafara.

JE KUJITOA MANII KWA MKONO KUNALAZIMU KAFARA?

Na ni katika maana ya jimai (tendo la ndoa) kujitoa manii kwa kukusudia, Mtu akitokwa na manii kwa kubusiana, au kwa kugusa au kwa kutumia mkono, basi saumu yake itaharibika, kwa sababu hiyo ni katika shahawa inao haribu saumu, na itakuwa ni juu yake kuilipa saumu yake wala hatolazimika kutoa kafara, kwa sababu kafara imekuja kwa tendo la ndoa peke yake.

Mtu akibusu au akigusa au akifikiria akatokwa na madhii saumu yake ni swahihi. kwa kutokuwa na dadili yakuharibu saumu kwa kutokwa na madhi

Mtu anapo lala akaota, au akatokwa na manii bila ya shahawa kama kuwa mgonjwa, saumu yake ni swahihi kwa sababu hayakutoka kwa hiyari yake.

Mtu anapo amka na janaba la tendo la ndoa kabla ya alfajiri au akaota, saumu yake ni swahihi na ni juu yake kuoga ili apate kuswali alfajiri na jamaa, imethubutu kutoka kwa bibi A’isha radhi za Allah ziwe juu yake Kwamba Mtume ﷺ:

[أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم كان يُصبح جُنُبًا من جماعٍ ثم يغتَسِلُ ويصوم]     متفق عليه

[Alikuwa akiingiliwa na Alfajiri na yeye akiwa na janaba la mkewe, kisha akioga na akifunga.]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

3. kujitapisha kwa kusudi
Nao ni mtu kutoa kilichoko tumboni kutokana na chakula au kinywaji kwa njia ya mdomo kwa kusudi, ama akishindwa na akatoka bila ya khiyari yake haiathiri saumu yake kwa neno lake Mtume ﷺ:

[من ذرعه القيء فليس عليه قضاء، ومن استقاء عمدا فليقض]     رواه أبو داود والترمذي وغيرهما وصححه الحاكم

[Mwenye kushindwa na matapishi basi hana haja ya kukidhi na mwenye kujitapisha kwa kusudi basi alipe]     [Imepokewa na Abuu Daud na Tirmidhiy na kusahihishwa na Al Haakim]

4. Damu ya Heidhi na Nifasi

Wakati wowote mwanamke atakapo ona damu ya hedhi au nifasi japo kuwa ni wakati wa jioni kabla ya kutwa jua kwa mda mchache saumu yake itaharibika na atawajibika kuilipa

SUALA: JE KUUMIKA HUVUNDA SAUMU?

Kauli yenye nguvu ni kuwa kuumika hakuvundi saumu kwa sababu Mtume ﷺ Aliumika na hali yakuwa amefunga, Amepokewa kutoka kwa said Al’khudriy radhi za Allah ziwe juu yake akisema

[رخص رسول الله في القبلة للصائم والحجامة]     أخرجه الدارقطني

[Aliruhusu Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ Kubusu kwa aliyefunga na kuumika,]     [Imepokewa na Al Daarqutniy]. Lakini inachukizwa kuumika kwa ajili ya kudhofika,

[سئل أنس بن مالك هل كنتم تكرهون الحجامة للصائم؟ قال : لا ، إلا من أجل الضعف]      رواه البخاري

[Aliulizwa Anas bin Maalik radhi za Allah ziwe juu yake Mulikuwa mukichukiza kuumika kwa alie funga? Akasema la ila kwa ajili ya kudhofika.]     [Imepokewa na Bukhari]

Haidhuru mtu kutokwa na damu katika jaraha, au kung’oa jino au kutokwa na damu za puwa, au kutoa damu kwa ajili ya kujipma, au kujitolea, yote haya hayaharibu saumu.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.