SOMO LA FIQHI
1. Kufinika kichwa cha mwanamume kwa kitu chenye kuambatana nacho.
Kwa hadithi iliyopokewa na Ibnu Umar radhi za Allah ziwe juu yake kwamba mtu alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Huyu aliye kwenye ihramu atavaa nguo gani. Mtume wa Mwenyezi ﷺ akasema:
لَا تَلْبَسُوا الْقُمُصَ، وَلَا الْعَمَائِمَ، وَلَا السَّرَاوِيلاَتِ [ هو ما يعرف بالبنطال] وَلَا الْبَرَانِسَ [ البرانس: هو كل ثوب رأسه منه ملتزق به] متفق عليه
[Msivae kanzu wala vilemba wala suruali [ Nayo ni ile inayojulikana kama bantaal.] wala kanzu zilizoshikana na kofia [ Baraanis: kila nguo ambayo kofia yake imeshikana nayo.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Na amesema ﷺ kuhusu mtu aliyekufa na yeye yuko kwenye ihramu:
[وَلَا تُخَمِّرُوا رَأْسَهُ : لا تضعوا له خمارا وهو غطاء الرأس]؛ فَإِنَّهُ يُبْعَثُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مُلَبِّيًا]. رواه البخاري
[Msimfinike kichwa chake kwa kitambara (Msimweke mtandio kichwani mwake, nao ni chenye kufunika kichwa) kwani atafufuliwa Siku ya Kiyama akileta Labbaika..] [Imepokewa na Bukhari.].
Ama ikiwa hakikushikana na kichwa kama kutumia mwavuli uo hema au sakafu ya nyumaba au gari hakuna ubaya wowote.
2. Kuvaa nguo ya kushonwa kwa mwanamume
Maana ya nguo ya kushonwa: ni iliyoshonwa kwa kadiri ya mwili au sehemu ya mwili, kama vile suruwali, kanzu, khofu (soksi nzito), soksi, soksi za mkononi na mfano wake, kwa hadithi iliyopokewa na Ibnu Umar iliyotangulia:
[لَا تَلْبَسُوا الْقُمُصَ، وَلَا الْعَمَائِمَ، وَلَا السَّرَاوِيلاَتِ، وَلَا الْبَرَانِسَ، وَلَا الْخِفَافَ] متفق عليه
[msivae kanzu, vilemba, suruali, Kanzu zilizoshikana na kofia wala khofu.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Akitopata mwenye kutaka kuhirimia Hija isipokuwa kikoi, basi inafaa avae suruali mapaka atakapopata kikoi [Kama mtu aliyesahau mavazi ya kuhirimia kwenye sanduku la safari ndegeni au melini na asiwe na kikoi, basi inafaa avue nguo zake na ahirimie akiwa amevaa suruali na alitatie shati lake liwe ni kama kishali, mpaka atapofika kwenye bandari atatoa mavazi yake ya kuhirimia na atayavaa na halazimiwi na kitu chochote.]. Na akitopata viatu, inafaa avae khofu, kwa kauli yake Mtume ﷺ:
[فَإِنْ لَمْ يَجِدْ نَعْلَيْنِ فَلْيَلْبَسْ خُفَّيْنِ، وَلْيَقْطَعْهُمَا حَتَّى يَكُونَا إِلَى الْكَعْبَيْنِ] رواه ابن خزيمة
[Akitopata viatu na avae khofu mbili na azikate mpaka zifike kwenye vifundi vya miguu] [Imepokewa na Ibnu Khuzaimah.]
3. Kuua kiwindwa wa barani au kumwinda
Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
{ لَا تَقۡتُلُواْ ٱلصَّيۡدَ وَأَنتُمۡ حُرُمٞۚ} المائدة :95
[Msiuwe viindwa na nyinyi mmehirimia Hija] [5: 95].
Yaani na nyinyi muko kwenye ihramu ya Hijja na ‘Umra.
Na kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
{وَحُرِّمَ عَلَيۡكُمۡ صَيۡدُ ٱلۡبَرِّ مَا دُمۡتُمۡ حُرُمٗ} المائدة :96
[Na mmeharamishiwa viindwa vya barani daima mnapokuwa katika hali ya ihramu] [Al Maaida: 96]
Na maana ya kiwindwa cha barani ni kinachokuwa cha mwituni miongoni mwa wanyama na ndege.
Ama mnyama wa kufugwa si kiindwa. Hivyo basi inafaa kwa aliye kwenye ihramu kuchinja kuku, wanyamahoa (mbuzi, ngo’mbe, ngamia) na mfano wao. Ama kiindwa cha baharini kinafaa, kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka :
{أُحِلَّ لَكُمۡ صَيۡدُ ٱلۡبَحۡرِ وَطَعَامُهُۥ} المائدة:96
[Mumehalalishiwa kiindwa cha baharini na chakula chake] [Al Maaida: 96].
Ama mnyama aliye haramu kuliwa kama nyoka na nge.Inafaa kwa aliye kwenye ihramu kumuua mnyama yoyote anayemshambulia iwapo hakuna njia nyingine ya kujikinga naye isipokuwa hiyo.
4. Kunyoa nywele, kuzipunguza au kuzisumua
Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
{وَلَا تَحۡلِقُواْ رُءُوسَكُمۡ حَتَّىٰ يَبۡلُغَ ٱلۡهَدۡيُ مَحِلَّهُ} البقرة:196
[Na msinyoe vichwa vyenu mpaka wafike wanyama wa kuchinjwa kwa ibada ya Hija mahali pake] [Al Baqara: 196].
Makatazo haya yanakusanya nywele za mwili wote kwa kukisia nywele za kichwa.
5. Kukata kucha
Sawa ziwe ni kucha za miguu au mikono.
6. Kujipaka Manukato mwilini na nguoni.
Imekatazwa kwa mwenye kuhirimia Hija kutia manukato mwilini mwake au kwenye nguo yake baada ya kuingia kwenye ihramu, au kuyanusa kwa kusudia, kwa hadithi iliyopokewa na Ibnu Umar radhi za Allah ziwe juu yake iliyotangulia ambayo ndani yake yamo maneno haya:
[وَلَا تَلْبَسُوا مِنَ الثِّيَابِ شَيْئًا مَسَّهُ الزَّعْفَرَانُ وَلَا الْوَرْسُ [ الورس: هو نبات أصفر طيب الريح يصبغ به] متفق عليه
[Wala msivae nguo yoyote iliyotiwa zafarani au wars [ Wars: ni mmea rangi ya manjano wenye harufu nzuri hutumiwa kwa kupaka.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
7. Kufunga ndoa
Kwa hadithi iliyopokewa na Uthman radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume wa Mwewnyezi Mungu ﷺ alisema:
[لا يَنْكِحُ المُحْرِمُ، ولا يُنْكِحُ، ولا يَخْطِب] رواه مسلم
[Aliye kwenye ihramu haoi wala haolewi wala haposi] [Imepokewa na Muslim.].
8. Kuundama
Nako ni kujamii kwenye tupu ya mbele, kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
{فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ ٱلۡحَجَّ فَلَا رَفَثَ} البقرة:197
[Yoyote anayeingia kwenye ibada ya Hija, basi asiuundame] [Al Baqara: 197]
Ibnu ‘Abbas radhi za Allah ziwe juu yake amesema: “Huko ni kujamii”. Nalo ni jambo kubwa zaidi lililoharamishwa kwa sababu ya ihramu.
9. Kustarehe kwenye sehemu isiyokuwa tupu
Kama vile kubusu na kushika, kwani hizo ni njia za kupelekea kuunadama na ni katika mambo yalio haramishiwa kwa mwenye kuhirimia.