KISA CHENYE MAFUNZO NA MAZINGATIO MAKUBWA
Wengi kati yetu tunawalaumu watu na kuwatuhumu kwamba wao ni wenye kupuuzia ktk malezi ya watoto wao na sisi hatujui ni kwa kiwango gani wanateseka juu malezi…
Mwanamke mmoja mtu mzima nilikutana naye Hijja alinisimulia kisa kiliniathiri sanaa…
Alisema yeye ni mjane na alikuwa yupo na mtoto mwema aliyehifadhi Quraan na alikuwa anaswali Swalah za usiku tangia utoto wake…
Na kwa mwanamke huyo mtu mzima alikuwa akiwaona watoto wa jirani zake hawapo sawa na mtoto wake yeye na alikuwa akiwalaumu kwa kutokusimamia malezi ya watoto wao na alikuwa akiwaangalia kwa jicho la kama kuwadharau kwamba wao hawapo vizuri kwenye malezi ya watoto wao pamoja ya kuwa hao watoto wa jirani zake hawakuwa watoto wenye tabia mbaya…
Anaendelea kuelezea huyu mama….
Kwa kweli nilikuwa najifakharisha mimi mwenyewe kwamba nimemlea mwanangu vizuri na nilijiona ni hodari kwa sababu mtoto wangu nimemlea yatima akiwa amefiwa na baba yake tangia akiwa mdogo na nilikuwa nasema vipi sasa kwa hawa wake ambao wapo na waume zao na ikawa hawawalei watoto wao vizuri!!
Anasema..ghafla mtoto wangu alibadilika..
Sio kwamba aliacha kuswali Swalah za jamaa msikitini tu, bali aliacha kabisa kuswali…
Ikawa sasa anasuhubiana na marafiki wabaya …kisha nikajakugundua kuwa ni teja flani wa madawa ya kulevya!!
Anasema…Nilibaki miaka mitatu namnasihi na kumuongoza pia nikashirikiana na wajomba zake ktk kumnasihi bila mafanikio.
Kwa mara ya kwanza nikafahamu jinsi ya wazazi wanavyo teseka pindi wanapojaribu kila namna juu ya kuwasaidia watoto wao ili waongoke bila mafanikio pamoja na kwamba watoto wao hawakufikia uasi kama aliofikia mwanangu…
Ilifikia hadi nikiingia chumbani kwake nakusanya vidongo vya madawa ya kulevya na picha za uchi nazitoa huwa anakasirika nikifanya hivyo na kunitolea ukali na kunisukuma na hukaribia kunipiga bali aliwahi kunipiga mara moja..
Anasema, ulivunjika moyo wangu na ikawa naona aibu kuwaona wale ambao nilikuwa nawadharaulia watoto wao kwamba sasa mtoto wangu anaongelewa vibaya na ilienea kwa watu wote..
Nikajua kuwa ALLAAH Amenipa fundisho na adabu..
AlhamduliLLaah sikusitisha kumuombea du’aa mtoto wangu miaka yote mitatu ya uasi wake nilikuwa naomba du’aa na kulia kwa maumivu..
Lakini ilikuwa kama vile ALLAAH Anataka kunipa fundisho na kweli pale sasa ilipovunjia yale yaliyokuwa kwenye nafsi yangu ya kujiona kwamba mimi nimemlea mtoto wangu vizuri na kuwalaumu watu kwa kutokuwalea watoto wao vizuri na nikajua kwamba mimi silolote bali hiyo ilikuwa ni rehma ya ALLAAH na matakwa Yake ndio sababu ya kutengenea kwa mtoto wangu bali mimi ilikuwa ni sababu tu…
Na Alipozuia ALLAH rehma Yake kutoka kwa mtoto wangu alipotea na kuharibika..
Kwa kweli niliposhakuwa na yakini hiyo ya kujua kwamba ALLAAH Ndiye Muongoaji.
Siku moja nikiwa namuomba ALLAH kwenye mswala wangu na huku nikilia, aliingia chumbani kwangu..Ilikuwa ni saa tisa usiku na macho yake yakiwa mekundu kutokana na kukesha na akiwa na harufu ya mihadarati aliibusu kichwa changu na akasema: Naomba radhi zako ee mama yangu kisha akanikumbatia na kulia..
Hakuendelea na kunisimulia ila huyu mama alilia na hakusita..
Nikamwambia nini kiliendelea eh khaalah?
Akasema: ALHAMDU LILLAAH muangalie yule pale ndiye yeye aliye nileta hapa Hijja!!
ALLAAH Amenihurumia kwa mtoto wangu bali kutengenea kwake kwa sasa si kwa uhodari wa malezi yangu bali ni tawfiiq ya ALLAAH…
MAZINGATIO:
Tufahamu kwamba watoto ni rizki na neema na tabia zao ni rizki na neema na malezi yao ni rizki na neema na heshima yao ni rizki na neema na upendo wao kwetu ni rizki na neema na tawfiiq ya ALLAAH kwao ni rizki na neema na nilazima rizki kushukuriwa na ni lazima neema kuhimidiwa daima wa abadan.
(Daima zingatia haya:)
▶️ Usifedheheshe utapewa mtihani.
▶️ Usifurahikie mabaya ya ndugu zako, ALLAAH Atawaondolea na Atakupa wewe mtihani.
▶️ Mtoto anapokuwa muasi usimuapize na kumkosesha radhi na kumfukuza nyumbani bali muombee dua kwa sana na usikate tamaa kwani Muongoaji ni ALLAAH na si wewe.
Yamenukuliwa: ….