0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MALEZI NA DOTKOMU

MALEZI NA DOTKOMU

Sote tunafahamu matatizo yanayo kumba ulimwengu kwasababu ya utandawazi na mrupuko wa maarifa kwa sababu ya mawasiliano yalivyo kuwa rahisi kupitia runinga rununu na mitandao ya wazi. Ni vigumu sana kuhifadhi tabia za watoto katika mazingira haya.

Tutafanya vipi kama wazazi kuwahami watoto wetu na maafa kama haya.
1. Kuelewa tunaisha katika ulimwengu aina gani na zile biri zinazotukabili katika malezi kila uchao. Kwa kufahamu aina za hatari zilizoko mbele yetu zinazoengezeka kila siku kuwa ulimwengu umekuwa kama kijiji kimoja mila na desturi za watu wengine zinapiga vita maadili ya mazuri ya jamii zetu za kiislamu.
2. Kuweka kinga za kujiepusha na uchafu na fikra mbovu zinazopatikana katika mitandao na kutahadharisha watoto wetu juu ya ubaya unaoletwa na utamaduni huu ya mawasiliano ya teknilojia kuwa rahisi na khatari zake.
3. Kuwa mbadala kwa njia ya kuwashajiisha na kuwafanaya kupenda mazuri yanayopatikana ndani ya hiyo teknolojia na kuwafanya watumie maarifa yale kwa kuboresha tabia njema,kuelimika na kueleimisha wengine. Mfano wa www.eDialogue.org mtandao ambao umewezesha kusilimisha Zaidi ya watu elfu kumi na pia nyaraka wa uso wa kitabu facebook na kiwingu skype na pia nena whatsapp.zote hizi zinaweza kutumika kwa maslahi ya Da’wa.
a.kueneza Uislamu
b.kuelimisha watu
c.kukataza mabaya
d.kueneza tabia njema
e.kuunga kizazi
f.kuleta umoja wa waislamu
g.kupinga ufisadi
4. kuwepo na ufuatiliziaji na kutathmini miondoko yao ili wasiweze kuchukuliwa na wimbi la ufisadi na fikra potofu na kuingia katika makundi ya kigaidi.
5. Mzazi kuishi ulimwengu wa kileo wa teknolojia ajue yanayoendelea katika mitandao ya wazi kwa mfano facebook uso wa kitabu. Ili aweze kuona mtoto wake anafikiria vipi kuelekea wapi au kushirikiana na kina nani na anasoma nini katika mtandao.
6. Wazazi washirikiane kuanda makongamano ya watoto, safari za pamoja yenye kukusanya mapumziko pamoja na kujitolea kutumikia jamii. Khaswa katika likizo za shule.
7. Mzazi kujua rafiki wa watoto wake kujua wanaenda wapi wanafanya nini na kusoma nini na mipango gani ili aweze kumtahadharisha mtoto na marafiki wabaya.
8. Kuwa karibu na mtoto kwa kuwa rafiki wa mtoto wako na kusuhubiana nayeye kwa kumonesha mapenzi pasina kumnyima uhuru wake kama mtoto.

Imeandikwa na

Sheikh Abuu Hamza

Mombasa- Kenya.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.