0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAKOMBO/MABAKI

Suali: Makombo ni nini?
Jawabu: Makombo ni yanayosalia chomboni baada ya kunywewa.

Suali: Ni ipi hukmu ya Makombo?

Jawabu: Asili ya makombo ni twahara isipokuwa yale ambayo kuna dalili ya kuwa ni najisi,

kama yanayofuata:

1. MAKOMBO AMBAYO NI TWAHAR

A. Makombo ya mwanadamu:
Kwa hadithi iliyopokewa na Bibi Aisha radhi za Allah ziwe juu yake asema:

[كنت أشرب وأنا حائض ، ثم أناوله النبي صلى الله عليه وسلم ، فيضع فاه على موضع فيّ فيشرب]   رواه مسلم

[Nilikuwa nikinywa hali yakuwa niko katika hedhi, kisha nikimpa Mtume akiweka kinywa chake sehemu niliokuwa nimeweka mdomo wangu kisha akinya]   [Imepokewa na Muslim.].

B. Makombo ya paka

Kwa kauli yake Mtume ﷺ kuhusu paka aliyekunywa kutoka kwenye chombo:

[إنها ليست بنجس إنما هي من الطوافين عليكم أو الطوافات]    رواه الترمذي

[Yeye si najisi, yeye ni miongoni mwa Wanaowazunguka na kuwa nanyi, wa kiume na wa kike]       [Imepokewa na Tirmidh.]

C. Makombo ya mnyama anayeliwa, mbagaa, punda, wanyama wakali na ndege wakali na mfano wa hao:
Ni twahara, kwa kuwa asili ya vitu ni twahara, na hakuna dalili ya kuwa ni najisi, na kwa kuwa Mtume ﷺ alikuwa akipanda punda na walikuwa wanapandwa wakati wake.

2. MAKOMBO YALIO NAJISI

A. Makombo ya mbwa
Kwa kauli yake Mtume ﷺ :

[طُهُورُ إِنَاءِ أحَدِكُمْ إِذَا وَلَغَ فِيهِ الكَلْبُ أنْ يَغْسِلَهُ سَبْعَ مَرَّاتٍ أُولاَهُنَّ بِالتُّرَابِ]    رواه البخاري مسلم

[Kutwahirisha kwa chombo cha mmoja wenu, kikirambwa na mbwa, ni akioshe mara saba, ya kwanza yake iwe kwa mchanga]        [Imepokewa na Bukhari na Muslim].

B. Makombo ya nguruwe
Makombo ya nguruwe ni najisi kwa neno lake Mwenyezi Mugnu mtukufu:

{أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ}     سورة الأنعام

[Au nyama ya nguruwe kwani hiyo ni uchmfu]    [6: 145].

Yaani najisi, nachochoe kinacho tokama na nguruwe ni najisi

C. Makombo ya wanyma wasioliwa

Wanazuoni wamekhtaliana juu ya makombo ya wanyama wasioliwa, Dhehebu la Imamu Maalik,na Imamu Shafi, wanaona makombo ya wanyama wasioliwa ni twahara kama vile makobo ya paka,na Dhehebu la Imamu Abuu Hanifa wamesema kuwa makombo ya mnyama asilie liwa ni najisi, na wakawato baadhi ya Wanyama,na Dhehebu la Imamu ahmad ni karibu na madhehebu ya Abuu Hanifa wakasema kuwa baadhi ya wanyama makombo yao ni twahara kama vile Panya na wadudu na wanaofana nao,na makombo ya baadhi ya wanyama ni najisi kama punda na mfano wake.

FAIDA

UTWAHARA WA MWANADAMU
Mwanadamu ni twahara, sawa awe ni muislamu, kwa neno lake Mtume ﷺ:

[إِنَّ الْمُؤْمِنَ لَا يَنْجُسُ]   رواه البخاري ومسلم

[Hakika mu’min hanijisiki]    [ Imepokewa na Bukhari na Muslim]

ao kafiri, kwa ilivo thubutu kuwa Mtume ﷺ alitawadha kwa chombo cha mushrik, ama neno lake mwenyezi Mungu :

{إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ}    التوبة:28

[Hakika mushrikina ni najisi]    [9: 28]

makusudio ni najisi ya kimaana


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.