MAISHA YAKE WAKATI WA MTUME ﷺ
‘Uthman alikuwa miongoni mwa marafiki wa Abu Bakar (r.a.). Walikuwa katika kikao siku moja, akawa Abu Bakar (r.a.) anamfafanulia uzuri wa Uislamu, na ubaya wa shirki. Alikuwa ‘Uthman (r.a.) si mwenye kutaradadi, akaathirika na maneno ya Abu Bakar (r.a.) kisha wakaenda pamoja kwa Mtume ﷺ, walipokutana na Mtume ﷺ alimlingania kwa Uislamu akasilimu.
Akawa miongoni mwa watu waliotangulia katika Uislamu.Wakaathirika vibaya Maquraysh kwa kusilimu ‘Uthman (r.a.). Ami yake Al-Hakam ibn Abil ‘Aas alifanya kila bidii ya kumtoa ‘Uthman (r.a.) katika kundi la walslamu, lakini hakufanikiwa, kisha akamuadhibu adhabu kali, lakini ‘Uthman (r.a.) akavumilia adhabu hizo na akawa ni mwenye msimamo. Pia mama yake alijaribu kutaka kumtoa ‘Uthman katika Uislamu, lakini hakuweza.
Mtume ﷺ alimuoza binti yake ambaye ni Ruqayyah. Maudhi ya Maquraish yalipozidi juu ya ‘Uthman (r.a.) aliamua kuhama na mkewe katika mwezi wa Mfungo Kumi, mwaka wa Tano wa Utume mpaka Habasha nchi ya Ethiopia. Kisha wakarudi Makkah na mkewe Mfungo Mosi mwaka huo huo. Kisha ‘Uthman (r.a.) akahamia Madinah baada ya kuhamia huko Mtume ﷺ, Kwa sababu hiyo akaitwa “Mwenye kuhamia mara mbili.
Mtume ﷺ alipoenda katika vita vya Badri, alimbakisha ‘Uthman (r.a.) Madinah ili kumuuguza mkewe. Akafariki mkewe kabla ya Mtume ﷺ kurudi kutoka vita vya Badri. ‘Uthman (r.a.) akahuzunika sana kwa kufariki mkewe. Na kwa nini asihuzunike ili hali umekatika ukwe kati yake na Mtume ﷺ Mtume ﷺ akamtuliza moyo ‘Uthman kwa kumuoza binti yake mwengine, Ummu-Kulthum (r.a.). Akaishi naye ‘Uthman mpaka alipofariki mwaka wa Tisa wa Hijrah.
Mtume ﷺ akamwambia ‘Uthrnan:
[والذي نفسي بيده لو كان عندي ثالثة لزوَّجتُكَها يا عثمان]
[Naapa kwa yule nafsi yangu iko mikononi mwake Lau kama ningekua na binti wa tatu ningekuozesha Ewe Uthma.]
Kwa sababu ‘Uthman alioa mabinti wawili wa Mtume ﷺ ndipo akaitwa “Dhan-Nurain” (mwenye nuru mbili).
Alikuwa ‘Uthman ana mali mengi kuliko Masahaba wote. Kwa sababu hiyo alitoa mali zaidi ya wote kwa vita vya Tabuk. Ukafikia mchango wake ngamia mia tisa, na farasi khamsini. Na alipokuja na Dinari elfu moja za dhahabu akaziweka mbele ya Mtume (s.a.w.) ambaye
akawa anazigeuza huku na huku kwa mikono yake, akisema:
[ما ضر عثمان ما عمل بعد هذا اليوم]
[Hatadhurika ‘Uthrnan na atakalofanya baada ya lea.]
Kwa sababu hiyo aliitwa “Muandalizi wa jeshi liliokuwa na uzito.” ‘Uthman (r.a.) alinunua kisima cha Rumah kwa Dirham 20,000 kutoka kwa Myahudi mmoja, kisha akakifanya waqfu. Na ilikuwa hakuna maji matamu ya kunywa Madinah isipokuwa kwenye kisima hicho. Kisha ikawa nasibu yake ni kuteka maji kama WaIslamu wengine.
Pia ‘Uthrnan (r.a.) alishiriki katika vita vyote pamoja na Mtume ﷺ isipokuwa vita vya Badri kama tulivyotangulia kueleza. Na pia alikuwa ‘Uthman (r.a.) ndiye mjumbe wa Mtume ﷺ kwa Maquraysh katika Sulhu ya AI-Hudaybiyyah. Alipokwenda Makkah kwa amri ya Mtume ﷺ akachelewa kurudi, ukaenea uvumi kuwa ‘Uthrnan (r.a.) arneuawa, walienda WaIslamu kwa Mtume ﷺ ambaye alikuwa chini ya mti wakambayi’ juu ya kupigana na Maquraysh, na wakachukua ahadi kuwa hawatakimbia wakati wa vita. Kisha Mtume ﷺ akachukua mkono wake, na akasema:
[هذه يد عثمان]
[Huu ni mkono wa ‘Uthman] akaupiga juu ya mkono wake wa kushoto, na akasema: “Na hii ni bay’ah ya ‘Uthrnan.” Ikawa ni Bay’ah ya Ar-Ridhwan. Na kwa juu ya hayo limeashiria
Neno lake Allah Aliyetukuka Allposema:
{لَّقَدْ رَضِيَ اللَّهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَنزَلَ السَّكِينَةَ عَلَيْهِمْ وَأَثَابَهُمْ فَتْحًا قَرِيبًا}
[Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewapa radhi Waumini walipo fungamana nawe chini ya mti, na alijua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa Ushindi wa karibu.]
Al Khulafaau Arrashiduun 103-105