0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAISHA YA MTUME MUHAMMAD ﷺ KABLA YAKUPEWA UTUME


MAISHA YA MTUME MUHAMMAD ﷺ KABLA YAKUPEWA UTUME


Mtume wakati wa ujana wake alikuwa na tabia nzuri katika jamii. Alikuwa mtu wa kuigwa kwa fikra nzuri na uoni sahihi. Alitunukiwa akili, fikra sahihi na uchaguzi sahihi wa malengo. Kukaa kwake kimya kwa muda mrefu kulimsaidia sana katika tabia ya tafakuri na kuupeleleza ukweli kwa undani. Akili yake angavu na maumbile yake vilikuwa nyenzo muhimu katika kuyaelewa maisha ya watu,mmoja mmoja na jamii nzima.

Alikuwa hanywi pombe na hali katika vile vilivyochinjwa kwa ajili ya masanamu, alikuwa hahudhurii sikukuu yoyote ya masanamu wala hafla zake. Tokea mwanzo wa makuzi yake alikuwa akijitenga na kukaa mbali na vitu vya batili vilivyokuwa vikiabudiwa. Ilifika hatua ikawa hakuna kitu chochote kilichokuwa kinamchukiza zaidi kuliko hayo masanamu na alikuwa havumilii kusikia watu wakiapa kwa Lata na Uzza.
Hapana shaka kuwa Uwezo wa Mwenyezi Mungu Ulirnzunguka kwa Kurnhifadhi, kwani wakati zinapotahariki hisia za nafsi kwa ajili ya kuona baadhi ya starehe za dunia na wakati anapokaribia kuridhia kufuata baadhi ya mambo ya kuiga ambayo si mazuri, Msaada wa Mwenyezi Mungu Uliingilia kati ili kuweka kizuizi kati yake na mambo hayo.

Ibn KAthir, amepokea kuwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) alisema:

مَا هَمَمْتُ بِشَيْءٍ مِمَّا كَانَ أَهْلُ الْجَاهِلِيَّةِ يَعْمَلُونَهُ غَيْرَ مَرَّتَيْنِ ، كُلُّ ذَلِكَ يَحُولُ اللَّهُ بَيْنِي وَبَيْنَ مَا أُرِيدُ ، ثُمَّ مَا هَمَمْتُ بَعْدَهَا بِسُوءٍ حَتَّى أَكْرَمَنِياللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ بِرِسَالَتِهِ ، فَإِنِّي قَدْ قُلْتُ لَيْلا لِغُلامٍ مِنْ قُرَيْشٍ كَانَ يَرْعَى مَعِي بِأَعْلَى مَكَّةَ : لَوْ أَنَّكَ أَبْصَرْتَ لِي غَنَمِي حَتَّى أَدْخُلَ مَكَّةَ فَأَسْمُرَ كَمَا يَسْمُرُ الشَّبَابُ ، فَقَالَ : افْعَلْ , قَالَ : ” فَخَرَجْتُ أُرِيدُ ذَلِكَ حَتَّى إِذَا جِئْتُ أَوَّلَ دَارٍ مِنْ دُورِ مَكَّةَ ، سَمِعْتُ عَزْفًا بِغَرَابِيلَ وَمَزَامِيرَ ، فَقُلْتُ : مَا هَذَا ؟ فَقَالُوا : هَذَا فُلانُ بْنُ فُلانٍ تَزَوَّجَ فُلانَةَ بِنْتَ فُلانٍ ” قَالَ : ” فَجَلَسْتُ أَنْظُرُ وَضَرَبَ اللَّهُ عَلَى أُذُنِي ، فَنِمْتُ فَمَا أَيْقَظَنِي إِلا مَسُّ الشَّمْسِ ، فَجِئْتُ صَاحِبِي ، فَقَالَ : مَا صَنَعْتَ ؟ ” قَالَ : قُلْتُ : ” مَا صَنَعْتُ شَيْئًا ، ثُمَّ أَخْبَرْتُهُ الْخَبَرَ ، ثُمَّ بِتُّ لَيْلَةً أُخْرَى مِثْلَ ذَلِكَ ، فَقَالَ : افْعَلْ ، فَخَرَجْتُ حَتَّى جِئْتُ مَكَّةَ ، وَسَمِعْتُ مِثْلَ الَّذِي سَمِعْتُ تِلْكَ اللَّيْلَةَ ، فَجَلَسْتُ أَنْظُرُ ، وَضَرَبَ اللَّهُ عَلَى أُذُنِي ، فَمَا أَيْقَظَنِي إِلا حَرُّ الشَّمْسِ ، فَرَجَعْتُ إِلَى صَاحِبِي ، فَأَخْبَرْتُهُ الْخَبَرَ ، ثُمَّ مَا هَمَمْتُ بَعْدَهَا بِسُوءٍ حَتَّى أَكْرَمَنِي اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ بِرِسَالَتِهِ

“Sikuwahi kukusudia jambo lolote katika mambo ambayo uialikutua wakifanya watu wa Jahiliyyah isipokuwa mara mbili, na katika mara zote hizo Mwenyezi Mungu (s.w.t) Aliweka kizuizi kati yangu na kati ya mambo hayo, baada ya hapo sikuyakusudia tena mpaka Mwenyezi Mungu Aliponikirimu kwa Utume Wake.Usiku mmoja niliwahi kumwambia kijana ambaye alikuwa akichunga mbuzi pamoja nami sehemu ya juu ya Makka.’Ninakuomba unianglizie mbuzi wangu ili niweze kuingia Makka nikashiriki huko katika mambo yanayofanywa usiku kama wanavyofanya vijana’, akakubali, nikatoka mpaka nilipofika katika nyumba ya mwanzo miongoni mwa nyumba za Makka; nilisikia ala za muziki zikitumbuiza. Nikasema kitu gani hiki? Wakasema: ‘Hiyo ni harusi ya fulani.’Nikakaa ninasikiliza, Mwenyezi Mungu Akayafunika masikio yangu, nikalala, niliamshwa na joto la jua la asubuhi. Nikarejea kwa rafiki yangu, akaniuliza, nikamuhadithia.Ukafuata usiku mwingine mfano wa hivyo, nikaingia Makka na nikapatwa na mambo mfano wa usiku wa kwanza, baada ya hapo sijajaribu tena katika maisha yangu. mpaka Mwenyezi Mungu  Aliponikirimu kwa Utume Wake.

Bukhari amepekea kutoka kwa Jabir bin Abdillah kuwa: “‘Wakati . ilipojengtoa Al-Ka’aba Mtume na Al-Abbas walikwenda wakiwa wanabeba mawe, Abbasi akamwambia Mtume : iwekeke shuka yako shingoni mwako itakukinga na mawe’, akaporomoka chini, yakakodoka macho yake kuelekea mbinguni, kisha akazindukana. “Shuka yangu, shuka yangu”, akaifunga juu yake shuka yake. ” au katika upokezi mwingine, ‘Hauuonekana tena utupu wake baada ya hapo. (1)

Mtume alikuwa akiongoza kwa mambo mazuri, tabia njema na sifa bora miongoni mwa jamaa zake, alikuwa akiongoza kwa upole na ukweli wa mazungurnzo, alikuwa laini wa nafsi na mwenye kujichunga zaidi na ma~bo maovu, aliwazidi pia kwa ukarimu na mambo ya kheri na alikuwa mwema mno kwa matendo na mbora wao katika kutekeleza ahadi, na mwaminifu kwa utunzaji wa amana, mpaka akafikia daraja ya kuitwa muaminifu na jamaa zake kutokana na tabia njema, na mambo yenye kuridhiwa.

Alikuwa kama alivyosema mama wa waumini, Bi Khadija (r.a.) kuwa alikuwa akiwaunganisha ndugu, na alimpa yule ambaye hakuwa na kitu, alikirimu wageni na kusaidia matatizo yao ya kweli.*


1) Sahihil Bukhari, [uzuu 1, Mlango Ujenzi wa Al-Kaaba, Uk. 540
*  Arraheeq Al Makhtum 98


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.