0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

VIPINDI VYA DA’WA NA AWAMU ZAKE

AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Inawezekana kuzigawa nyakati za Da’uia (wito) ya Mtume  kwenye vipindi viwili vilivyo kamilika kama ifuatavyo: 

1). Kipindi cha Makka

kilichochukua takriban miaka kumi na mitatu.

2). Kipindi cha Madina

kilichochukuwa takriban miaka kumi kamili. 

Kila kimoja katika vipindi hivyo viwili vinakusanya awamu; kila awamu ina mambo ya pekee yaliyokuwa tofauti na mambo ya awamu nyingine, na hilo limedhihiri, baada ya uchunguzi wa kina katika mazingira ambayo Da’wa yalipitia katika vipindi hivyo viwili. Tunaweza kukigawa kipindi cha Makka katika awamu tatu. 

(1). Awamu ya Da’wa ya siri, miaka mitatu.

(2). Awamu ya kutangaza Da’wa kwa watu wa Makka tokea mwanzoni mwa mwaka wa nne wa Utume, mpaka mwisho mwa mwaka wa kumi.

(3). Awamu ya Da’wa nje ya Makka, tokea mwisho wa mwaka wa kumi wa Utume mpaka kuhama kwake Mtume  kuelekea Madina. 
Ufafanuzi na Awamu ya Madina utaelezwa peke yake.*


* Ar-Raheeq Al Makhtum 117


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.