SOMO LA FIQHI
Suali: Ni nini Maana ya najisi kiluga na kisheria?
Jawabu: Maana ya Najisi kilugha Uchafu
Na kisheria: Ni Uchafu ambao Sheria imeamuru uondolewe
Suali: Ni zipi Sampuli za Najisi ?
Jawabu : Sampuli ya vitu Najisi ni hizi zifuatazo:
1. Mkojo wa binadamu na choo chake
Kwa Hadithi ya Mbedui aliyekojoa msikitini, Mtume ﷺ akamwambia:
[إن هذه المساجد لا تصلح لشيء من هذا البول والقذر إنما هي لذكر الله والصلاة وقراءة القرآن] متفق عليه
[Hakika Hii misikiti haifai ikojolewe au ichafuliwe. Linalopasa ni kutajwa Mwenyezi Mungu, kuswaliwa na kusomwa Qur’ani] [Imepokewa na Bukhari na Muslim].
2. Damu ya Hedhi
Kwa ilivyothubutu kuwa Khaulah binti Yasaar alimjia Mtume ﷺ akasema:
[يا رسول الله ليس لي إلا ثوب واحد وأنا أحيض فيه قال : [فإذا طهرت فاغسلي موضع الدم ثم صلي فيه] رواه أحمد وأبو داود
Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi sina isipokuwa nguo moja, na ninaingia hedhini nikiwa nimeivaa. Mtume ﷺ akasema: [Ukitwahirika osha pale mahali pa damu kisha uswali ukiwa na hiyo nguo] [Imepokewa na Ahmad na Abu Daud] .
3. Mkojo na choo cha wanyama wasio liwa
Kwa hadithi iliyosimuliwa na Ibn Masuud Radhi za Allah ziwe juu yake:
عبد الله يقول أتى النبي صلى الله عليه وسلم الغائط فأمرني أن آتيه بثلاثة أحجار فوجدت حجرين والتمست الثالث فلم أجده فأخذت روثة فأتيته بها فأخذ الحجرين وألقى الروثة وقال هذا ركس رواه البخاري
Kwamba Mtume ﷺ alienda chooni akaniamuru nimletee mawe matatu. Nikapata mawe mawili, nikatafuta la tatu nisipate, nikachukua choo kikavu cha mnyama nikamletea. Akachukua mawe mawili na kile choo akakitupa na akasema [Hiki ni najisi [ Riks: najisi.] [Imepokewa na Bukhari.]
MAS’ALA
Ni hukmu gani ya Mkojo na choo cha wanyama wanaoliwa ?
Mkojo wa mnyama anayeliwa na choo chake ni twahara kwa kuwa ilithubutu kutoka kwa Anas bin Malik Radhi za Allah ziwe juu yake asema:
عن أنس قال: نزل قوم من عكل وعرينة المدينة فاجتووها فأمرهم النبي عليه السلام أن يشربوا أبوال وألبان إبل الصدقة رواه البخاري
[Kwamba kuna watu walikuja Madina, na hewa yake isiwafae – yaani walishikwa na ugonjwa huko -. Mtume ﷺ akawapeleka kwenye ngamia wa Zaka wapate kunywa mikojo na maziwa ya hao ngamia] [Imepokewa na Bukhari.]
4. Mfu
Naye ni aliyekufa mwenyewe bila kuchinjwa kisheria, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Alisema:
{قُل لَّا أَجِدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلَّا أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ} الأنعام:145
[Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho haramishwa kwa mja kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu au damu inayo mwagika au nyama ya nguruwe kwani hiyo ni uchafu] [6: 145].
Na kinaingia katika maana ya mfu kile kilichokatwa kutoka kwa mnyama aliye hai kabla hajachinjwa.
Kwa neno leke Mtume ﷺ:
قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : [ مَا قُطِعَ مِنْ الْبَهِيمَةِ وَهِيَ حَيَّةٌ فَهِيَ مَيْتَةٌ ] واوه أبو داود وصححه الألباني
[Kilichokatwa kutoka kwa mnyama alie hai basi hicho ni maiti] [Imepokewa na Abuu Daudi na kusahihiswa na Al-Baniy]
Na vinavyovuliwa katika mfu ni:
1. Mfu wa Samaki na Parare
Kwa neno lake Mtume ﷺ:
[أحلت لنا ميتتان ودمان، الحوت والجراد والكبد والطحال] رواه أحمد
[Tumehalalishiwa mfu aina mbili, na damu aina mbili. Ama aina mbili za mfu, ni samaki na parare, na ama aina mbili za damu, ni ini na wengo] [Imepokewa na Ahmad]
2. Mfu asiye na Damu inayotiririka kama vile Nzi:
Kwa kuwa Mtume ﷺ alisema:
[إذا وقع الذباب في إناء أحدكم فليغمسه كله ثم ليطرحه، فإن في أحد جناحيه شفاء وفي الآخر داءً] رواه البخاري
[Anapoingia nzi kwenye chombo cha mmoja wenu, basi na amzamishe kisha amtoe na kumtupa, kwani kwenye mojawapo ya mabawa yake kuna ponyesho na katika lingine kuna ugonjwa] [ Imepokewa na Bukhari.].
5. Nyama ya Nguruwe
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu U Aliyetukuka Amesema:
{قُل لَّا أَجِدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلَّا أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ} الأنعام:145
[Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho haramishwa kwa mja kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu au damu inayo mwagika au nyama ya nguruwe kwani hiyo ni uchmfu] [6: 145].
6. Ute wa Mbwa
Mbwa ni najisi yeye mzima. Na unajisi wa ute wake umefanywa mzito, kwa kuwa Mtume ﷺ alisema:
[طُهُورُ إِنَاءِ أحَدِكُمْ إِذَا وَلَغَ فِيهِ الكَلْبُ أنْ يَغْسِلَهُ سَبْعَ مَرَّاتٍ أُولاَهُنَّ بِالتُّرَابِ] رواه مسلم
[Kutwahirika kwa chombo cha mmoja wenu iwapo mbwa amekiramba ni kukiosha mara saba, mara mojawapo kwa mchanga] [Imepokewa na Muslim].
Na kuramba ni atiapo mbwa ulimi wake ndani ya chombo na kuutikisa, anywe au asinywe.
7. Madhii
Nayo ni maji meupe mapesi yenye kunata, yanayotoka wakati wa kucheza na mke au kufikiria kuundama, si kwa matamanio ya nguvu wala hayatoki kwa kasi, na hayafuatiwi na hali ya kulegea, na wakati mwingine mtu hahisi kamwe kuwa yametoka. Hii ni kwa kuwa Mtume ﷺ katika hadithi iliyopokelewa na Ali bin Abi Twalib Radhi za Allah ziwe juu yake alipo sema:
عن علي بن أبي طالب رضي الله عنه قال : كنت رجلا مذاءً ، فاستحييت أن أسأل رسول الله صلى الله عليه وسلم لمكان ابنته مِنِّي ، فأمرت المقداد بن الأسود فسأله ، فقال : يغسل ذكره ويتوضأ .
[Nilikuwa nikitokwa na Madhii sana nikaona haya kumuliza Mtume kwa hishima ya binti yake kwangu ni kamuamuru Miqdaad bin Al-Aswad akamuliza Akasema Mtume [Aoshe dhakari yake na atawadhe] [ Imepokewa na Bukhari na Muslim].
8. Wadii
Nayo ni maji meupe mazito yanayotoka baada ya kukojoa.
MAS’ALA
UTWAHARA WA MANII
Manii: ni maji meupe, mazito, yanayotoka kwa matamanio ya nguvu kwa kasi, na yanafuatiwa na ulegevu, na yana harufu inayofanana na yai lililoharibika.
Nayo ni twahara, kwani lau yangekuwa najisi Mtume ﷺ angeamrisha yaoshwe.
Na inatosheleza, katika kuondoa manii, kuyaosha yakiwa majimaji, na kuyakangura yakiwa makavu, kwa hadithi ya Aishah Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa alisema:
[كنت أغسل الجنابة من ثوب رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فيخرج إلى الصلاة ، وإن بقع الماء في ثوبه ] رواه البخاري
[Nilikuwa nikiosha janaba katika nguo ya Mtume wa Mungu ﷺ ( akiosha manii) kisha akitoka kwenda kuswali kwa nguo hiyo na mimi nikiona athari yamuosho katika ile nguo] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Na katika riwaya ya Muslim:
[لقد كنت أفركه من ثوب رسول الله صلى الله عليه وسلم فركاً فيُصلي فيه] رواه مسلم
[Nilikuwa nikiyakangura manii kwenye nguo ya Mtume ﷺ kisha akiswalia] [Imepokewa na Muslim.].
Kuyaosha yakiwa majimaji Kuyakangura yakiwa makavu
FAIDA
Urutuba unao toka kwenye tupu ya Mwanamke ni Twahara ama ni Najisi?
Kwa kauli ya wengi katika wanachuoni wanasema kuwa umajimaji unaotoka kwa mwanamke ni twahara kama vile Majasho,Wala si najisi, ila tu nikuwa ya tenguwa Udhu,kwa hivyo hatolazimika kuosha nguo zake bali atakuwa ni mwenye kutawadha peke yake.
MAS’ALA
POMBE
Pombe kulinywa ni miongoni mwa dhambi kubwa, na kuna khilafu kati ya wanchuni kuhusu pombe ni najisi ama ni twaha? Madhhabu ya imam shafi wanaema kuwa pombe ni najisi,isipokuwa hakuna dalili kuwa ni najisi.
Ama neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ} المائدة:90
[Enyi mlio amin!bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya shetani basi jiepusheni navyo] [5: 90]
Lililokusudiwa ni uchafu wa kimaana na sio uchafu wa kidhahiri, kama ilivyo kamari na masanamu. Hukumu inayochukuliwa hapa ni kuwa utumiaji wa mafuta mazuri yenye alkoholi unafaa, kwa kuwa alkoholi inatolewa kwenye pombe.