0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAANA YA UDHU NA HUMKU YAKE

SOMO LA FIQHI

Suala: Ni nini Maana ya Udhu katika Luga na katika sheria?
Jawabu: Udhu katika lugha ni Uzuri na usafi
Na Maana ya Udhu katika Sheria:

“Ni kutumia maji kwenye viungo maalumu kwa nia ya kujitwahirisha.”

Ni ipi Hukumu ya kutawadha?
Jawabu: Kutawadha: ima ni lazima na ima inapendekezwa:

A. Ni lazima kutawadha kwa mambo matatu
1. KUSWALI.

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu mtukufu aliposema:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ}  المائدة:6

[Enyi Mlioamini! Mnapo simama kwa ajili ya swala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni]   [Al Maaida: 6]

Na kwa hidithi iliyopokelea na Abuu Hurayra radhi za Allah ziwe juu yake asema kuwa Mtume amesema:

[لا يقبل الله صلاة أحدكم إذا أحدث حتى يتوضأ]    متفق عليه

[Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapokuwa na hadathi (atakapotengukiwa na udhu) mpaka atawadhe (tena) ]     [Imepokewa na Bukhariy na Muslim.]

2. KUTUFU ALKA:

Kwa kauli yake Mtume ﷺ kumwambia mwanamke aliye katika hedhi siku za haji:

[افعلي ما يفعل الحاج غير أن لا تطوفي بالبيت حتى تطهري]    رواه البخاري

[Fanya yote anayo fanya mwenye kuhiji isipokuwa usitufu mpaka utwahirike]     [Imepokewa na Bukhari.]

3. KUSHIKA MSAHAFU:

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu mtukufu:

{لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ}   الواقعة:79

[Hawaigusi isipokuwa wale waliotwahiriwa]    [Al Waaqia: 79]

B. Kutawadha kunapendekeza katika mambo mengine yasiyokuwa hayo
Kwa neno lake Mtume ﷺ aliposema:

[ولا يحافظ على الوضوء إلا مؤمن]    رواه أحمد وإبن ماجة

[Na hajilazimishi na udhu isipokuwa mwenye Imani]   [ Imepokewa na Ahmad na Ibnu Maajah].

Na kunapendekezwa zaidi kutawadha wakati wa kujadidisha udhu kwa kila Swala, kutawadha kwa kumtaja Mwenyezi Mungu na kuomba, wakati wa kusoma Qur’ani, kabla ya kulala, kabla ya kuoga, na kutokana na kumbeba maiti na baada ya kila tukio la kutangua udhu, hata kama hataki kuswali.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.