0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAANA YA SWALA NA CHEO CHAKE

SOMO LA FIQHI

Suali: Ni nini Maana ya swala kilugha na kisheria

Jawabu: Maana ya Swala kilugha ni: Dua (Maombi)

Tukuiangalia Qur’ani Tukufu tutalikuta neno swala limetumika kwa maana ya dua njema na hii ndiyo maana ya swala kilugha, Mwenyezi Mungu anasema:

{خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّ صَلَاتَكَ سَكَنٌ لَّهُمْ}    التوبة:103

[Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo, na uwaombee rehema. Hakika maombi yako ni utulivu kwao.]       [Al-Tawba:103]

Ama Maana ya Swala katika Istilahi ya kifiqihi (kisheria)

Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu Subhanahu wata’aal kwa maneno na vitendo maalumu, vinavyoanzia kwa takbiri na vinavyomalizikia kwa kupiga salamu.

CHEO CHA SWALA

Suali: Swala ina hadhi gani katika Uislamu:

Jawabu: Hadhi ya Swala katika Uislamu

1. Swala ni nguzo ya pili katika nguzo za Uislamu.
Amesema Mtume :

عن عبد الله بن عمر بن الخطاب رضي الله عنهما قال : سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول : [ بني الإسلام على خمس : شهادة أن لا إله إلا الله  وأن محمدا رسول الله ، وإقام الصلاة ، وإيتاء الزكاة ، وحج البيت ، وصوم رمضان ]     رواه البخاري ومسلم

[Uislamu Umejengwa juu ya nguzo tano: kukiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja Wake na mtume Wake, na kusimamisha Swala…]      [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

2. Swala ndio amali bora kimatendo.

قال ابن مسعود رضي الله عنه: سألت رسول الله صلى الله عليه وسلم أي الأعمال أحب إلى الله؟ قال: [ الصلاة على وقتها]  الحديث أخرجه الشيخان

Amesema Ibnu Mas’uud Radhi za Allah ziwe juu yake nilimuliza Mtume ﷺ wa Mwenyezi Mungu ni Amali gani Mwenyezi Mungu anaependa zaidi? akasema [kuswali mwanzo wa wakati wake]     [Imepokewa na Tirmidhi]

3. Swala ni upambanuzi baina ya Uislamu na ukafiri.
Mtume  amesema:

[إن بين الرجل وبين الشرك والكفر: تركَ الصلاة؛]      رواه مسلم

[Baina ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha Swala]      [ Imepokewa na Muslim.]

4. Swala ni nguzo ya Juu ya Uislamu. baada ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na ndio yajenga Uislamu.
Mtume :

[رأس الأمر الإسلام ، وعموده الصلاة  ]    رواه الترمذي

[Kichwa cha jambo hili ni Uislamu na nguzo yake ni Swala]   [ Imepokewa na Al-Ttirmidhy]

5. Swala ndio ibada pekee aliyopewa Mtume Mbinguni bila ya wasita (Ukati) wa Malaika Jibrilu kwani ibada nyingine zote alipewa hapa hapa duniani kupitia kwa Malaika Jibrilu-Allah amshushie amani.

6. Swala ndio ibada ya mwanzo kabisa atakayohisabiwa na kukaguliwa mja siku ya kiyama kabla ya ibada nyinginezo,Asema Mtume  :

[إِنَّ أَوَّلَ مَا يُحَاسَبُ بِهِ الْعَبْدُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنْ عَمَلِهِ صَلَاتُهُ فَإِنْ صَلُحَتْ فَقَدْ أَفْلَحَ وَأَنْجَحَ وَإِنْ فَسَدَتْ فَقَدْ خَابَ وَخَسِرَ]    رواه أبوداود والترمذي

[Hakika jambo la kwanza atakalo hisabiwa mja siku ya kiyama katika matendo yake ni Swala,Ikitengenea basi amepasi na amefaulu,na ikiharibika basi ameangamia na kupata khasara.]   [Imepokelewa na Abuu Daud na Al-Tirmidhiy]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.