MAANA YA HIJJA
Suala: Ni nini Maana ya Hijja kilugha na Sheria?
Jawabu: Maana ya Hijja kilugha ni Kukusudia na kuelekea.
Ama maana ya Hijja kisheria
Ni kukusudia kwenda Makka katika kipindi maalumu ili kutekeleza ibada ya Hijja.
Suala: Ni ipi Hukumu ya Hijja
Jawabu: Hija ni fardhi kwa kila Muislamu mwenye uwezo, ni nguzo ya tano miongoni mwa nguzo tano za Uislam. Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Alioyetukuka:
وَلِلَّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ} آل عمران:97}
[Ni haki ya Mwenyezi Mungu kwa watu waihiji Alkaba, kwa anayeweza kwenda huko. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi Hawahitajii walimwengu] [3: 67]
Na amesema Mtume ﷺ:
[ بُنَي الإسلامُ على خَمْسٍ : شهادَةِ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمَّداً رسولُ اللهِ، وإقَامِ الصَّلاةِ، وإيتَاءِ الزَّكاةِ، وحَجِّ البَيْتِ، وصَوْمِ رَمَضَانَ رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ
[Uislamu umejengwa juu ya misingi mitano: Kukubali kuwa hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake, kusimamisha Swala, kutoa Zaka, kuikusudia Alkaba kwa Hija na kufunga mwezi wa Ramadhani] [Imepokewa na Bukhari.]
[مَنْ حَجَّ فَلَمْ يَرْفُثْ وَلَمْ يَفْسُقْ رَجَعَ كَمَا وَلَدَتْهُ أُمُّهُ ]
وفي رواية للترمذي : [ غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبه ] . صححه الألباني في صحيح الترمذي
Na amsema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ: [Mwenye kuhiji asiseme maneno machafu na asitoke kwenye utiifu wa Mwenyezi Mungu atarudi kama siku alio zaliwa na mamayake] Na katikwa riwaya ya Tirmidhiy [Atasamehewa dhambi zake zilizotangulia] [Imepokewa na Tirmidhi na kusahihishwa na Al-Baniy]
[Rafath: ni neno linalotumika kumaanisha maneno machafu.]
[Fusuuq: maasia.]
Suali: Je Ibaada ya hijja ni faradhi ya kila Mwaka?
Jawabu: Wameafikiana wanachuoni kuwa ibaada ya hijja ni faradhi ya umri mara moja.
kama ilivyo kuja kwenye Hadithi:
عن ابْنِ عَبَّاسٍ أَنَّ الأَقْرَعَ بْنَ حَابِسٍ سَأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ : يَا رَسُولَ اللَّهِ الْحَجُّ فِي كُلِّ سَنَةٍ أَوْ مَرَّةً وَاحِدَةً ؟ قَالَ : بَلْ مَرَّةً وَاحِدَةً ، فَمَنْ زَادَ فَهُوَ تَطَوُّعٌ ) رواه أَبُو دَاوُد وصححه الألباني
Kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba Aqra’i bin Habis alimuliza Mtume rehma na amani zifikie yeye akasema: Ewe Mtume wa Mwenyzi Mungu Hijja ni kila Mwaka au ni mara moja? Akasema [Ni mara moja na mwenye kuzidisha hiyo ni Sunna] [Imepokewa na Abuu Daud na kusahihishwa na Al-Baniy]