0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

KUSILIMU KWA UMARA BIN AL-KATTAB (Radhi za Allah ziwe juu yake)

AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Katika hali hii ya kiza kilichofunga na mawingu ya dhulma na uovu, ulijitokeza mwanga mwingine wenye nguvu zaidi ya kumweka na Ruangaza kuliko ule wa kwanza. Simwanga mwingine, isipokuwa ni kusilimu kwa ‘Umar bin Al-Khattab (Radhi za Allah ziwe juu yake), aliyesilimu mnamo mwezi wa Dhul Hijja, mwaka wa sita wa Utume,1B9 baada ya siku tatu toka kusilimu kwa Hamza (Radhi za Allah ziwe juu yake). Katika moja ya dua zake Mtume (ﷺ) alikuwa anamuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) Aliye Mtukufu Ajaalie kusilimu kwake. Hayo yanathibilrishwa na Ttirmidhi kutoka kwa Ibn ’Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake). Ameyasahihisha maneno haya na kuyathibitisha Tabarani, kutoka kwa Ibn Masoud. na Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuwa Mtume () aliwahi kuomba: Ewe Mala wangu wa haki utukuze Uislamu kwa {inayernpenda midi kati ya Umar bin Al-Khattab flfl Abu Iahl bin Hisham”, Ikawa aliyependeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni ‘Umar bin Al-Khattab (Radhi za Allah ziwe juu yake). 1

Baada ya kufanyika kwa utafiti katika mapokezi yote mbayo yamepokewa kuhusu kusilimu kwake, imedhihirika kuwa kuingia kwa Uislamu katika moyo wake ‘ni jambo lililokuwa linaingia kidogo kidogo. Muhammad Al-Ghazali katika kitabu chake, (1) anasema,‘Umar bin Al-Khattab (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa ni mtu aliyejulikana sana kwa ukali wa tabia na nguvu za nafsi na mara nyingi kabla ya kusilimu kwake Waislamu walipata maudhi ya namna mbalimbali kutoka kwake. Sura ya wazi iliyojitokeza kwake ni kuwa alikuwa akivutwa na ‘nguvu mbili zilizokuwa na msukumo sawa katika nafsi yake. Upande mmoja ulikuwa’ni wa tabia yake ya kuheshimu mambo ya kurithi yaliyowachwa na mababu kwa karne nyingi, kupenda starehe, matamanio ya ulevi na lahwu (Mambo ya kipuuzi), mambo ambayo. alikuwa ameyazoea. Kwa upande wa pili alikuwa akivutiwa na ukakamavu wa Waislamu na uvumilivu wao katika majaribio mbalimbali yaliyohusu itikadi yao. Kama ilivyo akili yoyote ya mtu makini, kwa kuzingatia mafuzo ya Uislamu ambayo tayari alikuwa ameyasikia, mara nyingi alikuwa akipata shaka moyoni mwake ya kuwa huenda yale ambayo Uislamu unahimiza watu wayafuate yakawa ni matukufu zaidi kuliko yale anayoyapenda, na kwa ajili hiyo wakati mwingi alikuwa akihamaki na mwishowe kutuli.

Kuhusu mapokezi mbalimbali yanayosimulia kusilimu kwake, inasemwa kuwa upo usiku mmoja aliamua kulala nje ya nyumba yake. Usiku ule aliamua kwenda Haram, alipofika huko alifululiza moja kwa moja na kwenda kuingia ndani ya pazia la Al-Ka’aba. Wakati huo Mtume () alikuwa anasali na alikuwa ameanza kusoma‘ Sumtu Al-Haqqa na Umar akawa anasikiliza Qur’an na kufurahishwa sana na namna ibara zake zilivyo Alisema: Nikajisemea katika nafsi yangu ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, kwa hakika huyu ni mshairi kama wanavyosema Makuraish, nilipoleta fikra hiyo Mtume akawa ansoma:

إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٖ كَرِيمٖ َمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَاعِرٖۚ قَلِيلٗا مَّا تُؤۡمِنُون

[Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima. ya mtunga mashairi (kama mmwyosema). Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini.] (69: 40-41)

Nikaleta fikra kuwa huyu-ni kuhani, akasoma :

وَلَا بِقَوۡلِ كَاهِنٖۚ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

[Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka. Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.] (69:42-43)

’Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) akasema, Hapo Uislamu ukaingia moyoni mwangu.”1

Huu ndio ulikuwa mwanzo wa kuingia kwa mbegu ya Uislamu kafika moyo wake. Lakini kwa sababu ya kasumba na hisia za kijahjlia na kufugamana kwake na mambo ya jamii yake aliyorithi ya kutukuza dini za mababu, alishindwa Kuifuata akili yake, akaendelea kuwa ni mwenye juhudi katika kuupiga vita Uislamu, bila ya kujali hisia nzuri ambazo zilikuwa zimejificha ndani ya moyo wake Kwa sababu ya ukali na tabia yake, na kuvuka kwake mipaka katika uadui wake dhidi ya Mtumbe wa Mwenyezi Mungu (), siku moja usiku alitoka hali ya kuwa ameuvaa upanga wake akiwa amedhamiria kwenda kumtafuta Mtumbe wa Mwenyezi Mungu () na kummaliza. Akiwa njiani alikutana na Nuaym bin Abdillah An-Naham al-Adawy, au mtu katika Banu Zuhrahl‘  au mtu katika Banu Makhzoum, ambaye alimuuliza; ‘Unakusudia kwenda wapi ewe ‘Umar? Alijibu bila ya kusita, ”Ninataka kwenda kumwua Muhammad.” Akaulizwa tena; ’Unajihakikishiaje usalama wako kwa Banu Hashim na Banu Zuhra, utakapokuwa umemuua Muhammad?.’ ’Umar akajibu; ‘Ninakuona wewe kuwa ni miongoni mwa waliotoka na kuiacha dini ambayo walikuwa wakiiamini kabla “ Akaulizwa, ‘]e nikufahamishe maajabu ewe ’Umar?! Kwa hakika dada yako na shemeji yako nao pia wameiacha dini yako ambayo unaiamini.

‘Umar aliposikia hivyo ndio hasira zikamidi, akageuza njia na kuelekea nyumbani kwa dada yake, huko akakuta na Khabbab bin Al-Aratt akiwa mbele ya dada yake na mumewe, huku akiwa na ubao ambao umeandikwa Surat Twaha, akiwa anawasomesha. Huyu ndiye mtu aliyekuwa akiwasomesha Quran. Khabbab (Radhi za Allah ziwe juu yake) aliposikia mshindo wa ‘Umar alijificha ndani ya ile nyumba na Fatima dada yake ‘Umar akaufunika ule ubao. Hata hivyo, wakati ‘Umar ameikurubia hiyo nyumba alikuwa amekisikia kisomo cha Khabbab akiwasomesha, alipoingia ndani aliuliza kwa sauti ya ukali, “Ni sauti gani hii yenye kujificha ambayo nimesikia kutoka kwenu?” Wakamjibu kuwa, hapana zaidi ya mazungumzo ambayo walikuwa wakizungumza kati yao. Kwa hasira akawauliza, ”Ninasikia kuwa mumeiacha dini yetu, ni kweli?.” Shemeji yake nae akauliza, “Ewe ‘Umar hivi unaonaje ikiwa haki haiko katika dini yako?” Kwa hasira ‘Umar akamrukia shemeji yake na kuanza kumpiga kwa nguvu, dada yake akamvuta ili kumwepusha na mume wake. ‘Umar akamgeukia. dada yake na kumpiga kofi lililomchana na kumtoa damu usoni. Katika mapokezi mengine Ibn Ishaq anasema, ”Umar alimpiga dada yake, akampasua uso wake, naye akiwa ameghadhibika, akasema, ‘Ewe Umar ikiwa iko haki katika dini isiyo yako nitaifuata. Ninakiri kwa moyo na kutamka kwa ulimi kuwa hakuna Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na ninakiri kwa moyo na kutamka kwa ulimi kuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. ’Umar alikata tamaa, na alipoona damu inamtoka dada yake alijuta na kuona haya na akasema, “Ninaomba na mimi mnipe hiki kitabu mnachosoma”, Dada yake akamueleza, ”Kwa hakika wewe ni mchafu na hawakishiki isipokuwa Watu Waliotoharika, kama unataka simama na ukaoge kabla hatujakukabidhi kitabu hiki. Akasimama na akaenda kuoga, kisha akakichukua kitabu na kusoma, ’Bismillahir Rahamanir Rahiim’, akasema, ’Umar ’Hakika haya ni majina mazuri yaliyotakasika.’ Kisha akasoma Twaha mpaka alipofika katika maneno yake Mwenyezi Mungu

إِنَّنِيٓ أَنَا ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱعۡبُدۡنِي وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ لِذِكۡرِيٓ

[Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana mungu ila Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na ushike Swala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi. ]
’Uzuri ulioje wa maneno haya na ubora wake’ ndiyo yaliyokuw_a maneno ya ’Umar baada ya kusoma Quran. ’Umar akaomba aelekezwé alipo Mtume  (), Khabbab .(r.a) aliposikia maneno ya Umar alitoka katika. chmnba alichojificha mle ndani na Akasema, “Ewe “Umar,i kwa hakiké mimi ninataréjia, kuwa wewe ndio utakuwa jibu la maombi ya Mtumbe wa Mwenyezi () aliyoyaomba usiku wa Alkhamisi kwa kusema “Mola wangu wa haki utukuze Uislamu kwa unayempenda zaidi _kati ya Umar bin Al-Khattub na Abu Iahl bin-Hashim”,  aliyasema hayo Mtumbe wa Mwenyezi Mungu () _aLipokuwa nyumba ambayo iko msingi wa’]ab_ali Swafai . ’
Baada ya kusikia yote hayo ’.Umar alichukua upanga wake akauvaa na kisha akaondoka kuelekea katika nyumba aliyokuwepo Mfume -() Alipofika akagonga mlango, kabla ya kufunguliwa mtu mmoja kwa ndani alichungulia katika upenyo wa mlango na akamwona ‘Umar akiwa ameuvaa upanga wake, mtu yule akapiga ukelele na’ kusema ‘Ni ’Umar’na upangawake’, Hamzah (Radhi za Allah ziwe juu yake) akaondosha khofu ya wenzake na’ kusema: ”Mwacheni aingie. Kama ni rafiki akaribishwe lakini kama ni adui basi atauliwa na panga lake mwenyewe.” Akamueleza Mtumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) nae akatoa amri, “MfuguIieni mlango, ikiwa amekuja kwa kheri tutampa hiya kheri na ikiwa amekuja kwa shari tutamuua kwa uprmga wake”, wakati huo Mtume () akiwa ndani anateremshiwa wahyi. Mtumc (s.a.w) akamtokea ’Umar, akakutana naye katika chumba, akaukamata mkusanyiko wa nguo zake pamoja na vichukulio vya upanga, kisha akamvuta kwa nguvu sana na kumueleza, ”Hivi bado haujakoma tu ewe’ Umar, unataka mpaka Mwenyezi Mungu (s.w.t) Akuteremshie yale yaliyo miongoni mwa fedheha na mateso yaliyowashukia watu wa Al-Walid bin Al-Mughira?.” ‘Ewe Mala Wangu wa Haki upe nguvu Uislamu kwa ’Umar bin Al-Khattab.”
Baada ya maneno hayo ya Mtume (). ’Umar akasema: ”Ninakiri kwa moyo na kutamka kwa ulimi kuwa hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kuwa wewe ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu.” ’Umar baada ya shahada hiyo akawa ameingia katika Uislamu; Mtume () na masahaba wakatoa takbira kwa furaha: Allahu Akbar.


1) Fiqhi sira Uk 92-13
1) Ibnu Jawzi Tarikh Umar Uk. 6
1) Tarikh Umar bin Khattab Uk. 7,10,11 Mukhtar sira Uk 102.103 Ibnu Hisham Juzuu 1.Uk 343-340
2) Arrahiq Al Makhtum 175-182

Begin typing your search above and press return to search.