0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

KUFARIKI KWA MAMA YAKE MWENYE HURUMA SANA


KUFARIKI KWA MAMA YAKE MWENYE HURUMA SANA


 Baada ya tukio hili, Halima alipata hofu juu ya maisha ya Mtume na akaamua kumrudisha kwa mama yake. Akawa chini ya uangalizi wa mama yake mpaka alipofikisha umri wa miaka sita

Katika kuadhimisha kumbukumbu ya mume wake aliyekufa Bi Amina aliamua kuzuru kaburi lake huko Yathrib, umbali wake unafikia kilometa mia tano.Akatoka Makka akiwa pamoja na mtoto wake yatima – Muhammad – na mtumishi wake Ummu Ayman, na msimamizi wake Abdul Muttwalib. Akakaa huko kwa muda wa mwezi mmoja kisha akaamua kurejea. Wakati wakiwa njiani kurejea Makka ghafla alipatwa na maradhi, maradhi yakamzidi na akafariki dunia huko Abwaa, kati ya Makka na Madina.*


* Arraheeq Al Makhtuum 85


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.