AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Mambo yaliendelea namna hii kwa muda wa miaka mitatu kamili. Katika mwezi wa Muharram, 2 ikiwa ni mwaka wa kumi wa Utume, ilikuwa ndiyo siku ya kubatilishwa kwa mkataba na kuvunjika. Kwa sababu ya tofaufi zilizozuka kati ya Makuraishi, maana kutokea mwanzo, wapo waliounga mkono mkataba huo na wapo walioupinga. Wale waliokuwa wanapinga mkataba huo walikuwa wakiongozwa na Hisham bin ’Amru kutoka katika kabila la Banu Amir bin Luay aliyekuwa akiwaendea Banu Hashim katika bonde kwa kujificha wakati wa usiku akiwapelekea chakula, (maana yeye alikwishawahi kumuendea Zuhair bin Abi Umayya al-Makhzoumy na ambaye mama yake alikuwa ni ‘Aatikah binti Abdil-Mutwalib), na kumuuliza, “Ewe Zuhair hivi ni kweli kuwa umeridhia kula chakula na kunywa maji na hali ya kuwa wajomba zako wamo kafika hali ambayo unaijua?” Naye akajibu: ”Rehema iwe juu yako, nitafanya nini wakati mimi ni mtu mmoja tu? Ama, Ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu, laiti kungelikuwa na mtu mwingine aliye tayari, mimi ningekuwa wa kwanza kuubatilisha mkataba huu”, hapo Hisham akamwambia basi kwa hakika sasa umempata mtu uliyekuwa unamtaka, baada ya hapo wakakubaliana kuwa watafute na mtu wa tatu. 1
Akaenda kwa Mut’im bin ’Adiy, akamkumbusha udugu wa Banu Hashim na Banu Al-Mutwalib watoto wa Abdi Manafi akamlaumu juu ya kuwaunga mkono Makuraishi kwa dhulma hii, Mut’im bin ‘Adiy akasema: ”Rehema iwe juu yako, nitafanya nini? Kwa hakika si vinginevyo, ni mtu mmoja tu”, Akaambiwa “Umempata na mtu wa pili”, akauiiza, “Nani huyo?” Akajibiwa, “Ni mimi”; Mut’im akasema, “Nipatie mtu wa tatu”, _ Akajibiwa, “Nimekwishafanya hivyo”; Akauliza tena, “Ni nani huyo mtu wa tatu?” Akaelezwa, “Ni Zuhair bin Abu Umayya.” Wakakubaliana kuwa watafute na mtu wa nne, akaenda kwa Abu Al-B’ulahtari bin Hisham, akamweleza mfano wa yale aliyomweleza Mut’im. Akaulizwa, ”Je, kuna mtu yeyote ambaye atasaidia katika hili?” Akajibiwa; ”Ndiyo.” Akauliza; “Ni nani huyo?” Akajibiwa; “Ni Zuhair bin Abu Umayya na Mut’im bin “Adiy, na mimi niko pamoja nawe.” Wakakubaliana kuwa watafute na mtu wa tano, akamwendea Zamgha bin Al-Aswad bin Ali-Mutwalib bin -Assad, akazungumza naye, akamkubusha juu ya udugu wao na haki yao, akaulizwa, ”Je, yuko mtu yeyote mwingine kafika hili jambo unailoniitia?” Akajibiwa, ”Ndiyo.” Siku waliyo kubaliana ilipofika wakakutanika mahali paitwapo _Al- Hajouni, wakakubaliana kuubalilisha ule mkataba, Zuhair akasema: “Mimi nitakuwa mtu wa kwanza kuzungumza.”
Asubuhi ya siku ya pili kama ilivyokuwa kawaida yao walikwenda kwenye mabaraza yao, asubuhi hiyo Zuhair alikwenda akiwa katika vazi maalumu. Aliizunguka Al- Ka’aba mara saba, kisha akawaelekea watu waliokuwepo. Akasema, ”Enyi watu wa Makka, hivi tunaona fakhari gani kula chakula na kuvaa nguo wakati Banu Hashim wanaangamia? Hawauziwi kitu na hapanunuliwi kutoka kwao? Ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu, sitakaa chini mpaka upasuliwe ubao ulioandikwa mkataba huu ulio na dhulma na unaokata udugu.”
Abu Jahli aliyekuwa katika upande wa Msikiti alisimama na kusema, ”Umesema uwongo, Ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu kibao (ulioandikwa ule rnkataba) hakitapasuliwa.” Hapo Zam’a Bin Al-Aswad naye akasimama na kusema: “Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu, wewe ni mwongo zaidi, si wote tulioridhia wakati wa kuandikwa kwake. Abu Al-Bukhtari alisimama na kuunga mkono; ”Amesema kweli Zam’a, hatuyaridhii yale ambayo yameimdikwa, na hatuyakubali”, na hapo akasimarna Mut’im bin ’Adiy na kusema: “Mmesema kweli na amesema uwongo yule ambaye amesema kinyurne na hayo, tunajiepusha kwa Mwenyezi Mungu na kibao hicho na yaliyomo ndani yake.” Hisham bin Amity nae akaunga mkono hoja kwa kusema maneno mfano wa hayo. Abu Jahli akasema, ’Hili ni jambo lililoamuliwa usiku, mahali pengine pasipokuwa hapa.’ – Wakati maneno hayo yakisemwa Abu Twalib alikuwa amekaa upande wa msikiti, na alifika pale kwani alishajua kuwa Wahyi umeteremshiwa kwa mtoto wa nduguye kuwa: ‘Mchwa wameshautafuna ule mkataba, isipokuwa kilichobakia ni Jina la Allah (ﷻ) lililokuwa ndani ya maandishi yale.” Abu Twalib aliwakabili Makuraishi na kuwaeleza, ”Mtoto wa ndugu yangu amenieleza kadha na kadha….. (na akawaeleza kibao kuliwa na mchwa); Niko tayari kuwapa Muhammad (ﷺ) mumfanye mtakavyo yakiwa maneno aliyoyasema sio sahihi, au muendelee na kuwatenga kama ilivokuwa kwa muda wa miaka mitatu iliyopita. Watu wote wa Makka walikubaliana na pendekezo lake. Wakasema umefanya uadilifu, na baada ya mazungiunzo kati yao na Abu Jahl. Mut’im alikwenda ili aubandue ule mkataba, alitaharuki kwa kukuta kuwa wote umeshaliwa na mchwa isipokuwa pale palipoandikwa, ”Kwa Iina Lako Ewe Mela.”
Ubatilishaji wa mktaba ulikamilika na Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alitoka katika bonde, Ash-Shib, na waliokuwa pamoja naye. Mushirikinaa wakawa wameonyeshwa daljli kubwa miongoni mwa dalili za Utume wake, isipokuwa kama alivyokwisha kueleza Mwenyezi Mungu (ﷻ) kuhusiana nao:
وَإِن يَرَوۡاْ ءَايَةٗ يُعۡرِضُواْ وَيَقُولُواْ سِحۡرٞ مُّسۡتَمِرّٞ
“Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea.” (54:2)
Hawakuijali dalili hiyo na wakauongeza ukafiri juu ya ukafiri wao.