0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

UJUMBE WA MWISHO WA MAKUREISH KWA ABU TWALIB


AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Mtume wa Mwenyezi Mungu () alitoka pamoja na iliokuwa nao katika bonde, Shi’ib Abu Twalib na akaendelea kufanya shughuli zake katika hali yake ya kawaida. nao pamoja na kuwa waliacha kuwatenga Banu Hashim, hawakuacha kuwakandamiza na kuwazuilia na njia ya Mwenyezi Mungu (). Abu Twalib aliendelea kumkinga na uadui mtoto wa ndugu yake, lakini umri wake ulishakuwa ni mkubwa unaovuka miaka themanini, hali yake haikuwa nzuri na haswa baada ya miaka mitatu ya kutengwa, ilidhoofisha viungo vyake na kudhoofisha afya yake kwa ujumla. Haukupita muda ila maradhi yalimuandama. Wakati huo Mushirikina waliogopea sifa yao kuonekana ni mbaya kwa Waarabu, iwapo baada ya kufa kwake watafanya jambo lolote baya kwa mtoto wa ndugu yake. Kwa ajili hiyo wakafanya mbinu kwa mara nyingine tena kujadiliana na Mtume () mbele ya ammi yake Abu Twalib, na watoe baadhi ya yale ambayo hawakuwa radhi kuyatoa huko nyuma kumpa Mtume (), wakaamua kupeleka ujumbe na huo ulikuwa ndiyo ujumbe wao wa mwisho kwa Abu Twalib.

Ibn Ishaq na wengine walisema: Abu Twalib alipopatwa na maradhi mazito, taarifa ziliwafikia Makuraishi, walizungumza miongoni mwao na kusema kwa, ’Hakika Hamza na Umar wamesilimu na limekwisha tangaa jambo la Muhammad katika makabila ya Makuraishi wote. Kwa hiyo, twendeni kwa Abu Twalib tumuombe amzuie mtoto wa ndugu yake na amtoe kwetu, tunaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu hatutakubali atunyanganye jambo letu.” Katika tamko jengine: “Hakika sisi tunaogopea kifo’ cha mzee huyu, na kumtokea yatakayomtoea na Waarabu kupata ya kusema: ’Wamemwacha mpaka alipo kufa ammi yake ndipo walipomfanyia uovu ”

Walikwenda kwa Abu Twalib, wakaongea naye na katika ujumbe ule walichaguliwa watu mashuhuri zaidi katika watukufu wa Kikuraishi na idadi yao ilikuwa ni ishiri na wa tano; miongoni mwao walikuwa ni: ‘Utba bin Rabia, Shayba bin Rabia, Abu Jahli bin Hisham, Umayya bin Khalaf na Abu Sufyan bin Harb. Wakasema kumwambia Abu Twalib: “Ewe Abu Twalib, wewe unafahamu nafasi yako kwetu, na wamehudhuria wanao, na tunahofia hali yako, na unalijua Iile ambalo liko baina yetu na mtoto wa ndugu yako. Kwa hiyo, mwite mchukulie kutoka kwetu na tumchukulie sisi kutoka kwake, ili ajizuie na sisi tujizuie naye na atuache sisi na dini yetu na tutamwacha yeye na Dini yake.”

Baada ya kupokea ujumbe wa Makuraishi, Abu Twalib alipeleka ujumbe kwa Mtume () na alipomjia akamwambia: “Ewe mtoto wa ndugu yangu, hawa ni mabwana katika jamaa zako wamekusanyika ili wakupe na wachukue kutoka kwako (mpate kukubaliana)”, kisha akamweleza yale ambayo wamemweleza na waliyoyapendekeza kwaké, miongopi mwa hayo ni kuwa kila kundi lisipjgane na kundi lingine. Mtume _wa Mwenyezi Mungpi () akajibu kwa kuwaambia:

أريتم إن أعطيتكم كلمة تكلمت بها وملكتم بها العرب ودانت لكم العجم

“Hivi mwaonaje kama nitawapa tamko moja tu ambalo mkulikubali mtameza kuwatawala _Waarabu wote na Waajemi kuwalipa nyie kodi?.”

Katika tamko lingine lililopokelewa ni kuwa alimwambia Abu Twalib; “Ninawataka watamke tamko moja tu wutakapolitamka, Waarabu wate watakuwa china yao nu kwa tamko hilo watatoa Waajemi kodi.” Katika tamko jingine alisema; “Ewe Ammi yangu kwa nini huwalitaki katika lile ambalo ni bora sana kwao?.” Akauljza ammi yake; ”Unawalingania kwenye jambo gani?.” Mtume (ﷺ) akasema; “Niwalingania kwenye kutamka neno moja tu ambalo kwa tamko hilo Waarabu wote watakuwa chini yao na watawamiliki kwalo Waajemi.”

Kwa tamko la upokezi wa Ibn Is’haq  “Tamko maja tu ambalo mkilitoa mtawamiliki kwalo Waarabu nu Waajemi watakuwa china yenu.” Alipoyasema maneno hayo, walishangaa na wakatoshewa na hawakujua vipi watalikataa hili tamko moja lenye manufaa kwenye mpaka na kiwango hiki. Kisha Abu Jahli akasema, “Ni tamko gani hilo? Tunaapa kwa jina la baba yako, tupe tamko hilo na kumi mfano wake”, akasema:

تقولون: لاإله إلا الله وتخلعون ما تعبدون من دونه

“Mtasema Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu () na mviache vile mnavoviabudu kinyume na Mwenyezi Mungu ().”

Wakapiga makofi, kisha wakasema: ”Hivi unataka ewe Muhammad kuwafanya waungu wote kuwa Mungu mmoja tu? Hakika jambo lako linastaajabisha sana.”

Kisha baadhi yao wakasema: ”Hakika mtu huyu hatotoa chochote kuwapa mnachotaka au kuwakubalia mnayoyataka, ondokeni na endeleeni na dini ya baba zenu mpaka atakapo hukumu Mwenyezi Mungu kati yenu na kati yake.” Kisha wakatawanyika.

Kuhusiana na watu hawa Mwenyezi Mungu () Aliteremsha Maneno Yake:

صٓۚ وَٱلۡقُرۡءَانِ ذِي ٱلذِّكۡرِ بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فِي عِزَّةٖ وَشِقَاقٖ كَمۡ أَهۡلَكۡنَا مِن قَبۡلِهِم مِّن قَرۡنٖ فَنَادَواْ وَّلَاتَ حِينَ مَنَاصٖ وَعَجِبُوٓاْ أَن جَآءَهُم مُّنذِرٞ مِّنۡهُمۡۖ وَقَالَ ٱلۡكَٰفِرُونَ هَٰذَا سَٰحِرٞ كَذَّابٌ أَجَعَلَ ٱلۡأٓلِهَةَ إِلَٰهٗا وَٰحِدًاۖ إِنَّ هَٰذَا لَشَيۡءٌ عُجَابٞ
وَٱنطَلَقَ ٱلۡمَلَأُ مِنۡهُمۡ أَنِ ٱمۡشُواْ وَٱصۡبِرُواْ عَلَىٰٓ ءَالِهَتِكُمۡۖ إِنَّ هَٰذَا لَشَيۡءٞ يُرَادُ مَا سَمِعۡنَا بِهَٰذَا فِي ٱلۡمِلَّةِ ٱلۡأٓخِرَةِ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا ٱخۡتِلَٰقٌ

“S’ad, Naapa kwa Qur’ani yenye mawaidha Lakini walio kufuru wamo katika majivuno na upinzani Mataifa mangapi tumeyaangamiza kabla yao, na wakapiga kelele, lakini wakati wa kuokoka ulikwisha pita.Na walistaajabu kuwajia mwonyaji anaye tokana nao wenyewe, na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo.Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu. Na wakaondoka wakubwa wao wakiwaambia: Nendeni zenu na dumuni na miungu yenu, kwani hili ni jambo lililo pangwa. Sisi hatukusikia haya katika mila hii ya mwisho. Haya si chochote ila ni uzushi tu. (38:1-6)


1) Ibnu Hishaam Juzaa 1, Uk 417-419
2) Tafhimul Qura’n Juzuu 4 Uk. 316-418, Mukhtasir sira Uk 91
3) Arrahiiq Al Makhtuum, Uk 199-202

Begin typing your search above and press return to search.