SOMO LA FIQHI
KIWANGO CHA KUTOLEWA ZAKA YA FITRI
Pishi moja na [Pishi ni sawa na kilo mbili na gramu arubaini (2.040 grms).]. kwa kila mtu, na kiwe ni chakula cha binadamu (kula) kama mchele, na tende, na ngano, kwa Hadith ya Abu Saii’d Alkhudhry radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie asema:
[كنا نُخْرِجُ في عهد رسول الله صلى الله عليه وسلم يوم الفطر صاعاً من طعام] رواه البخاري
[Ilikuwa tunatoa katika wakati wa Mtume ﷺ siku ya Fitri pishi moja ya chakula]. [Imepokewa na Bukhari]
Na akasema: “Na kilikuwa chakula chetu ni Shayir (aina ya nafaka), na zabibu, na aqitwu (Maziwa yaliyokaushwa). na tende) [Imepokewa na Bukhari]..
Na pishi ni sawa na 3.25kg kulingana na dhehebu la hanafia, ama jumhuri ya wanavyoni ni sawa na 2.040kg.
Na hukadiriwa vile vile kwa kujaza mkono mara nne kwa mwanamume wasitani
WANAOSTAHIKI KUPEWA ZAKA YA FITRI.
Inatolewa Zaka ya Fitri kwa yale makundi manane ambayo kwamba yanapewa Zaka, kwa maana (Zaka ya Fitri) ipo ndani ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّهِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۖ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّهِ ۗ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ
[Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni waajibu ulio faridhiwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima.] [At-Tawbah: 60]