0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

KATIKA PANGO LA HIRAA


KATIKA PANGO LA HIRAA


Wakati Mtume alipofikisha umri wa miaka arobaini, alikuwa ni mmoja miongonimwa watu waliokomaa kiakili na kifikra kati ya jamaa zake, yeye alipendelea sana kujitenga, alikuwa akichukua chakula chake na maji na kwenda kwenye pango la Hiraa katika Jabal Nuru, kiasi cha maili mbili kutoka Makka.

Jabal Nuru ni pango lililo katika mazingira mazuri, urefu wake ni kiasi cha yadi nne, na upana wake ni kiasi cha yadi 1.75. Watu wa nyumbani kwake walikuwa karibu naye, mwezi wa Ramadhani alikuwa akifanya kazi hapo na alikuwa akiwalisha maskini waliokuwa wakimwendea na akiutumia wakati wake katika ibada na kufikiria juu ya mambo yanayomzunguka katika vitu vyenye kuonekana katika ulimwengu huu, na uwezo uliojaalia vitu vyote hivyo katika maumbile ya ajabu kabisa. Hakuwa na raha kuwaona watu wake katika hali walizokuwa nazo, walikuwa wakifuata itikadi za kishirikina, itikadi iliyo mbovu na dhaifu kwa hoja. Wakati wote huo mbele yake hakukua na njia iliyo wazi au utaratibu wa maisha ulio na mipaka au mfumo maalum, wala njia yenye kunyooka ambayo ingetuliza moyo wake na kumridhisha. 

Kujitenga kwa Mtume : kulikuwa ni sehemu ya mipango ya Mwenyezi Mungu kwake, ili amuandae kwa lile jambo ambalo Alimkusudia, katika mambo makubwa. Kwa vile Mwenyezi Mungu Alikuwa Amekusudia Mtume aathiri maisha ya watu na kuwabadilisha watu katika mwelekeo mwingine, ilikuwa hakuna budi isipokuwa kwa roho hiyo kujitenga na watu kwa muda, na kujitenga na shughuli za kidunia na mazonge ya kimaisha na tamaa nyingine ndogo za watu zilizokuwa zinawashughulisha kimaisha. 

Hivi ndivyo alivyopanga Mwenyezi Mungu , Kumpangia Muhammad wakati Akimuandaa kubeba Amana kubwa ya kufikisha ujumbe ambao umegeuza hali ya dunia na kuandika historia mpya. Mtume alijitenga kwa muda wa miaka mitatu, kabla ya kupewa dhamana ya ujumbe kwa watu wote. Wakati mwingine alikuwa akijitenga kwa muda wa mwezi, akiwa peke yake na nafsi yake huru, akiyazingatia mambo yaliyo ndani ya huu ulimwengu wenye kuonekana katika siri iliyofichwa, mpaka ulipofika muda wa kushiriki katika siri hiyo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.


* Rahmaiul-Lil-t Alamivn, Juzuu 1, Uk. 4 na lbn Hisham, [uzuu I, Uk 230-235
na Fidhilal-l- Qur’an, [uzuu 2, Uk. 166

Raheeq Al Makhtum 99-100


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.