0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

JINSI YA KUTOA ZAKA YA MALI YA BIASHARA

SOMO LA FIQHI

Suali: Ni jinsi gani yatatolewa zaka za mali ya biashara?

Jawabu: Jinsi ya kutoa zaka ya Mali ya biashara ni kama ifuatavyo:
Mali yanapo pitiwa na mwaka zinakaguliwa bidhaa alizouza na kupewa bei ile ambayo kwamba iko sasa sokoni, kisha inatolewa zaka ya hayo mali kwa kutolewa bidhaa zenyewe au kima chake kwa njia ya pesa, kulingana na mahitaji ya mafakiri.

Vipi mfanyi biashara atafanya hisabu ya zaka ya mali ya biashara?
1. Atahisabu vitu vyote alivyonavyo katika bidhaa za biashara kwa kima cha wakati wa sasa.

2. Ataongeza pesa zote alizonazo, sawasawa iwe pesa zile alizitumia katika biashara ama hakuzitumia.

3. Aongeze vyote anavyodai watu katika madeni.

4. Aondowe chochote anachodaiwa.

5. Atoe Zaka kwa yatakayobakia (baada ya kufanya hivi vyote), nayo ni robi ushuri (2.5%)

Zaka inayowajibika kutolewa = (kima cha bidhaa za biashara + pesa + madeni anayodai watu – madeni anayodaiwa) x (kiwango cha kutolewa Zaka 2.5%).

– Kuhisabu zaka za biashara hutizamwa mali ya zaka yaliko atazifafanua na azitie kima siku ile yakupasa zaka akijisaidia na orodha ya hisabu ya mali bila yakuzingatia faida au hasara katika hisabu ya faida na hasara

– Vitu viliyo tayarishwa kwa ajili ya kubebea mali kama mifuko au mikebe havitiwi kima pekeyake ikiwa havikununuliwa kwa ajili ya kuviuza pekeyake, ikiwa zitatumiwa kwa kuviuza kibiashara basi vitatiwa kima vikiwa hupita kima cha mali yale. ikiwa havizidi kwa kima kama karatasi za kukunjia hivingii katika kutuwa kima.

– Kutia kima huwa kwa Mfanya biashara yeyote awe ni wakuuza jumla au rejareja kwa thamani ambayo aweza kununuliya mwisho wa mwaka kima cha mabadaliko Nacho hutofautiana na bei ya kuuza na kima cha kuuza sokoni au cha tarehe au nukuu.

– Bei zikitofautiana wakati wa kupasa zaka na wakati wakuzitoa inazingatiwa yatapewa siku ya kupasa ni sawa zizidi ama zipunguwe.

Na kuhusiana na suala la kutoa zaka kwa bidhaa zinazo safirishwa kabla ya kuzipokea, zaka za bidhaa hizi zitamuhusu yule anayezimiliki. Na umiliki wake unapatikana kwa kuzipokea bidhaa iliyonunuliwa kwa maelezo ya kuwa ipo njiani. Ikiwa imenunuliwa kwa mfano makabidhiano ya msingi yawe katika bandari (gati) la muuzaji. Umiliki halisi utapatikana kwa kupokea shehena hiyo. Na ikiwa imenunuliwa na makabidhiano ya msingi yawe katika bandari (gati) la mnunuzi basi umiliki wa mali hii unapatikana na kwa kitendo cha kufika tu shehena ya mali hiyo katika bandari (gati)..

– Mali ya biashara yakiwa ni ya pesa mbali mbali, au ni dhahabu au fedha basi hutiwa kima kwa kujuwa kiwango kinacho pasa kutowa kwa sarafu ambayo aitumia mfanya biashara na hilo ni kwa bei ilioko siku ya kupasa zaka.

– Na mizigo ya biashara ambayo mwenye kununua alitangulizia kuilipia lakini hajapokea ile mizigo basi zaka zake hazimpasi mwenye kununua bali humpasa mwenye kuuza.

FAIDA

Zaka za malighafi yakutumika kwa sanaa na vyenye kusaidia

1. Ama malighafi ya kimsingi yaliyo tayarishwa kwa ajili ya sanaa kama chuma kwa ajili ya kutengeneza magari, na mafuta ya kutengeneza sabuni, inapasa kutolewa zaka kulingana na thamani ambayo zilo nunuliwa mwisho wa mwaka, haya vilevile ni kwa wanyama na nafaka na mimea na kama hivyo.

2. Vitu vya kusaidia ambavyo haviingi kwenye orodha za kufanyia vitu vya sanaa kama vitu vya kuchomea havina zaka ni kama mali thabiti.

3. Zaka za bidhaa zisokuwa za sanaa na ambavyo havijesha kutengezwa:

4. Hutolewa Zaka zisizokuwa za sanaa

Na ambazo hazijesha kutengenezwa, zaka za mali ya biashara kulingana na thamani yake kwenye yalivo hivi sasa mwisho wa mwaka

– Kukusanyika sababu nyengine ya zaka pamoja na mali ya biashara

Yakikusanyika pamoja na mali ya biashara mali mengine yakutolewa zaka kama mali yamakulima hutolewa zaka za mali ya biashara


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.