0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

JE KUNA KAFARA YA MTU ALIYESHIKA QUR’ANI BILA YA TWAHARA?

JE KUNA KAFARA YA MTU ALIYESHIKA QUR’ANI BILA YA TWAHARA?

SWALI:  Je kuna Kafara ya mtu aliyeshika Qur’ani bila ya twahara:

JAWABU: Bila shaka kushika Mswahafu bila ya kuwa na twahara ni katika mambo yalio haramishwa kwa Mwenye hadathi ndogo au kubwa na hii ni kwa mujibu ya kauli ya Jamhuri ya wanachuoni. Kwa hivyo mtu anapo shika Qur’ani bila ya kuwa na twahara huwa amefanya dhambi na ni juu yake kutubia na kuleta Istighar na kuazimia kutofanya tena kosa hili mara nyingine, na mtu Akitubia hufutiwa ile dhambi kwa Idhini ya Mwenyezi mungu, kwa sababu toba ya kikweli huwa ni kafara ya ile dhambi kwa neno lake Mtume Rahma na amani zimfikie Yeye:

[التائب من الذنب كمن لا ذنب له]     أخرجه ابن ماجه

[Alitubia na Dhambi ni kama asie kuwa na dhambi]    [Imepokewa na Ibnu Maajah.]

Na jee mtu halazimika na kitu chochote? La hakuna jambo lingine lolote, wala kafara aina yoyote ile.

Na Allah ndie mjuzi zaidi.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.