0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

JE ALIEFUNGUA BAADHI YA MASIKU KWA DHARURA ATAPATA FADHLA KAMA ZA YULE ALIFUNGA RAMADHANI KAMILI?

JE ALIEFUNGUA BAADHI YA MASIKU KWA DHARURA ATAPATA FADHLA KAMA ZA YULE ALIFUNGA RAMADHANI KAMILI?

Suali :

Imekuja katika sahihi mbili katika Hadithi ya Abu hureira Radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume MUHAMMAD ﷺ amesema : [Atakaefunga Ramadhan hali yakua ana imani na anatarajia malipo basi atasamehewa madhambi yake yaliyopita.]

jee yule aliyefungua baadhi ya masiku katika ramadhan kwa sababu ya udhuru jee fadhla hii ataipata ? Au fadhla hii ni kwa yule aliefunga ramadhani kamili.

Jawabu :

Ama baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumswalia Mtume Muhammad ﷺ.

Udhahiri wa Hadithi hii na ALLAH ni mjuzi zaidi ni kwamba fadhla hii inaenea hata kwa yule ambae hakufunga Ramadhani kamili .imekuja katika kitabu cha (Faidhul Qadiir) alipozungumzia hadithi hii ya :

[مَنْ صَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ]    رواه البخاري ومسلم 

[Atakaefunga Ramadhan hali yakua ana imani na anatarajia malipo basi atasamehewa madhambi yake yaliyopita] Anasema Karmaany “Na lau atawacha kufunga katika Ramadhani na nia yake ni kwamba lau sio udhuru uliompata angelifunga basi ataingia katika hukmu hii kama vile akiswali hali yakua amekaa kwa udhuru basi atapata thawabu ya mwenye kusimama”. mwisho
Na ALLAH ni mjuzi zaidi.

*Chanzo: Fatawa za Sheikh Al Munajid

Imefasiriwa na Mahamd Fadhil El Shiraziy

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.